Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Isak aitamani Barca, akiisikilizia Liverpool

TETESI Pict

Muktasari:

  • Isak ambaye mkataba wake unamalizika mwaka 2028,  anahusishwa huenda akasajiliwa na Liverpool kwa ajili ya kuziba pengo la Mohamed Salah anayeweza kuondoka mwisho wa msimu.

MSHAMBULIAJI wa Newcastle United na timu ya taifa ya Sweden, Alexander Isak, yuko tayari kujiunga na Barcelona katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi lakini kipaumbele chake cha kwanza ni kutua Liverpool ikiwa watawasilisha ofa ya kutaka kumsajili.

Isak ambaye mkataba wake unamalizika mwaka 2028,  anahusishwa huenda akasajiliwa na Liverpool kwa ajili ya kuziba pengo la Mohamed Salah anayeweza kuondoka mwisho wa msimu.

Staa huyu ambaye msimu huu amecheza mechi 33 za michuano yote, amefunga mabao 23 na kutoa asisti tano, huduma yake pia inahitajika na Arsenal ambayo inahitaji kuboresha eneo lao la ushambuliaji.

Mpango wake wa kujiunga na Barcelona unaonekana kuwa na uwezekano mdogo wa kukamilika kwa sababu kiasi cha pesa kinachohitajika na Newcastle ili kumwachia ni kikubwa.


Harry Kane

STAA wa Bayern Munich na timu ya taifa ya England, Harry Kane, 31, anadaiwa kuwa na mpango wa kutaka kurejea England katika dirisha lijalo na Liverpool ni miongoni mwa timu zinazotajwa kutaka kumsajili. Kane ambaye mkataba wake na Bayern, unatarajiwa kumalizika mwaka 2027, msimu huu amecheza mechi 37 za michuano yote na kufunga mabao 32.


Jadon Sancho

CHELSEA itatakiwa kulipa Pauni 25 milioni kwa ajili ya kumsainisha mkataba wa kudumu mshambuliaji wa Manchester United, Jadon Sancho anayecheza kwa mkopo katika kikosi chao.  Sancho mwenye umri wa miaka 24, amekuwa mmoja kati ya wachezaji tegemeo katika kikosi cha Chelsea tangu ajiunge nao kwa mkopo katika dirisha lililopita.


Rodrigo Bentancur

TOTTENHAM iko tayari kuanza mazungumzo na wawakilishi wa kiungo wao wa kimataifa wa Uruguay mwenye umri wa miaka 27, Rodrigo Bentancur, kuhusu kumuongeza mkataba mpya katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Staa huyu tayari ameshapokea ofa kutoka AC Milan ambayo inahitaji kumsajili mwisho wa msimu. Mkataba wake unamalizika mwaka 2026.


Tyler Dibling

MABOSI wa Tottenham wameanza kuangalia uwezekano wa kumsajili Southampton, Tyler Dibling, 19, ambaye ameonyesha kiwango bora akiwa na timu hiyo tangu msimu uliopita. Dibling ni miongoni mwa wachezaji tegemeo katika kikosi cha kwanza cha Soton na msimu huu amecheza mechi 30 za michuano yote na kufunga maba manne. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2027.


Noni Madueke

WINGA wa Chelsea na England, Noni Madueke, 23, yupo katika rada za AC Milan ambayo inahitaji kumsajili katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Madueke ambaye mkataba wake na Chelsea unatarajiwa kumalizika mwaka 2030, anatamani kuachana na timu hiyo kwa sababu hapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza. Msimu huu amecheza mechi 28 za michuano yote.


Raul Asencio

BEKI wa Real Madrid na Hispania, Raul Asencio, 22, yupo katika hatua za mwisho kusaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia katika viunga vya timu hiyo kwa muda mrefu zaidi. Mkataba wa sasa wa fundi huyu unatarajiwa kumalizika mwakani. Msimu huu amecheza mechi 40 za michuano yote.


Antonio Cordero

NEWCASTLE United inaongoza katika vita yao dhidi ya Real Madrid na Barcelona wakipambania  saini ya mshambuliaji wa Malaga ambaye ni raia wa Hispania, Antonio Cordero, 18. Cordero amepanga kujiunga Newcastle badala ya Barca na Madrid kwa sababu anaamini atapata nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.