Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jamus yafunguka mbinu zilizoidhibiti Simba Kigali

Muktasari:

  • Muhire amesema walitambua mapema kuwa Simba ilikuwa ikipewa nafasi kubwa ya kushinda kutokana na ubora wa kikosi, hivyo benchi la ufundi liliwaandaa kuwabana wachezaji wenye uwezo wa kuamua matokeo na kutengeneza nafasi za mabao.

KIGALI: NAHODHA wa Jamus SC ya Sudan Kusini, Kevin Muhire, amesema walilazimika kuweka ulinzi maalumu kwa baadhi ya nyota wa Simba akiwemo Clatous Chama na Inno Loemba, jambo ambalo lilichangia kupata suluhu katika mchezo wa Kombe la CECAFA Kagame uliochezwa kwenye Uwanja wa Kigali Pele, Rwanda.

Muhire amesema walitambua mapema kuwa Simba ilikuwa ikipewa nafasi kubwa ya kushinda kutokana na ubora wa kikosi, hivyo benchi la ufundi liliwaandaa kuwabana wachezaji wenye uwezo wa kuamua matokeo na kutengeneza nafasi za mabao.

"Tulijua Simba ni timu nzuri sana na ilikuwa inahitaji pointi tatu kama sisi, tulijiandaa vizuri na tukafuata mpango tuliowekewa na benchi la ufundi, lengo letu lilikuwa kuhakikisha tunapata angalau pointi moja na tulifanikiwa," amesema Muhire.

Nahodha huyo amesema Chama na Loemba ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa wamepewa uangalizi wa karibu kutokana na uwezo wao wa kutengeneza nafasi na kuunganisha mashambulizi, huku wakihakikisha washambuliaji wa Simba hawapati uhuru wa kucheza watakavyo.

"Tulijaribu kuwazuia Chama na yule namba 10  (Loemba) wasiwe huru kufanya wanachokipenda, hatukuwapa nafasi ya kucheza kwa urahisi, ndiyo maana hawakupata nafasi nyingi za kutuumiza. Simba ni timu yenye ubora, lakini nasi tulifanya kazi yetu vizuri na tukapata matokeo tuliyoyahitaji," amesema Muhire.

Baada ya michezo miwili, Simba ipo nafasi ya tatu katika Kundi B ikiwa na pointi mbili Jamus SC inaongoza kundi kwa pointi nne, huku Singida Black Stars ikiwa ya pili na pointi tatu, wakati Mogadishu City ikiburuza mkia kwa pointi moja.

Sasa matumaini ya Simba ya kutinga hatua ya nusu fainali yanategemea kwanza kuifunga Singida Black Stars katika mchezo wake wa mwisho wa makundi. Hata hivyo, ushindi pekee unaweza usitoshe, kwani pia italazimika kusubiri matokeo ya mchezo kati ya Jamus SC na Mogadishu City.