Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Iraola akabidhiwa jukumu Liverpool

NDUG 01

Muktasari:

  • Iraola, mwenye umri wa miaka 43, amesaini mkataba wa miaka miwili kuchukua nafasi ya Arne Slot, ambaye alifutwa kazi hivi karibuni ikiwa ni mwaka mmoja tu baada ya kuiongoza Liverpool kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England.

LONDON, ENGLAND: KOCHA Andoni Iraola amesema anaelewa “kile kinachotarajiwa” kwake, lakini yuko tayari kukabiliana na changamoto mpya baada ya Liverpool FC kuthibitisha kuwa ndiye kocha wao mkuu mpya.

Iraola, mwenye umri wa miaka 43, amesaini mkataba wa miaka miwili kuchukua nafasi ya Arne Slot, ambaye alifutwa kazi hivi karibuni ikiwa ni mwaka mmoja tu baada ya kuiongoza Liverpool kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England.

Kocha huyo wa zamani wa AFC Bournemouth anajiunga na Liverpool baada ya kuipa Bournemouth msimu bora zaidi katika historia yake ya ligi kuu, ambapo ilimaliza katika nafasi ya sita.

IRAOLA

Nafasi hiyo ilikuwa moja nyuma ya Liverpool na tofauti ya alama tatu pekee, huku ikiipa Bournemouth nafasi ya kushiriki Europa Ligi msimu ujao.

Mhispania huyo alitangaza mwezi Aprili kuwa angeondoka Bournemouth mwishoni mwa msimu huu, huku akihusishwa na klabu za Crystal Palace FC na AC Milan.

Sasa anaelekea Merseyside, ambapo Liverpool imefuzu kushiriki Ligi ya Mabingwa msimu ujao licha ya kumaliza msimu wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 60,idadi yao ya chini zaidi tangu msimu wa 2015/16, na ikiwa pointi 25 nyuma ya mabingwa, Arsenal FC.

IRA 02

“Kwa kweli ninafuraha, ninafuraha mno,” amesema Iraola.

“Kwa sababu unajua Liverpool ni klabu kubwa, klabu ya kiwango cha juu, moja ya klabu kubwa zaidi duniani. Huhitaji sababu nyingi kuvutiwa na Liverpool. Liverpool ni Liverpool.”

Ameongeza: “Nadhani Liverpool inanipa nafasi ya kufundisha wachezaji wa kiwango cha juu, na wachezaji wa kiwango cha juu wanakupa nafasi ya kupigania mataji. Kushinda mataji.

Bila shaka unapowasili katika klabu mpya huwezi kuahidi kila kitu. Huwezi kutoa ahadi zote. Lakini ni kweli kwamba ninaelewa ninapokuja na ninajua kile kinachotarajiwa.

IRA 03

Iraola, ambaye alikumbuka shamrashamra za mashabiki wa Anfield baada ya Federico Chiesa kufunga bao la ushindi dakika za mwisho dhidi ya Bournemouth mwezi Agosti mwaka jana, anaripotiwa kuwa na hamu ya kuwaleta wasaidizi wake wa zamani wa Bournemouth, Tommy Elphick na Shaun Cooper, kwenye benchi lake la ufundi Liverpool.

Akikumbuka safari ya Bournemouth kwenda Anfield karibu miezi 10 iliyopita, Iraola amesema: “Chiesa alifunga na uwanja mzima ulilipuka kwa furaha. Ilikuwa hali ya ajabu sana, sivyo? Sasa nataka kuhisi hali hiyo nikiwa upande wa Liverpool.

"Mwanzoni unapowasili katika klabu yoyote, nadhani lazima ujithibitishe kwanza kwa kiasi fulani. Lazima upate haki ya kuwa sehemu ya klabu hiyo. Nataka kufanya hivyo haraka iwezekanavyo ili nami niweze kusherehekea pamoja nao na kuwa sehemu kamili ya shangwe hizo.”