Slot afunguka mazito baada ya kufutwa kazi Liverpool
Muktasari:
- Slot, mmoja wa makocha wenye mafanikio makubwa Liverpool anaondoka kwenye klabu hiyo baada ya kufutwa kazi na timu hiyo Jumamosi iliyopita.
LIVERPOOL,ENGLAND: KOCHA wa zamani wa Liverpool, Arne Slot amesema anaondoka katika klabu hiyo ukiwa ni muda sahihi kwake.
Slot, mmoja wa makocha wenye mafanikio makubwa Liverpool anaondoka kwenye klabu hiyo baada ya kufutwa kazi na timu hiyo Jumamosi iliyopita.
Slot, mwenye umri wa miaka 47, alitwaa taji la Ligi Kuu England msimu wake wa kwanza, lakini alifutwa kazi baada ya Liverpool kumaliza nafasi ya tano msimu huu, pointi 25 nyuma ya mabingwa Arsenal.
Liverpool inatarajia kuanza mazungumzo rasmi na Andoni Iraola, kocha wa zamani wa Bou rnemouth, kwa ajili ya nafasi ya kocha mkuu wiki hii.
Katika barua ya hisia iliyochapishwa kwenye gazeti la Liverpool Echo, Slot amewamshukuru mashabiki kwa kumpokea kwa moyo mkunjufu na kumsaidia katika safari yake. “Hii ni jambo linalonipendeza sana,” aliandika.
“Naondoka nikiwa na imani kamili katika kile kilicho mbele. Wachezaji waliotoa mengi kwa klabu hii, waliodumisha maadili yake na kuunda kumbukumbu zisizosahaulika, wamejenga msingi utakaodumu.”
Pamoja na kufungwa mara 20 katika mashindano yote, Slot alihakikisha Liverpool inashiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msi mu ujao.
“Kuhakikisha tumeingia Ligi ya Mabingwa Ulaya ni jukumu muhimu ambalo linaiwezesha Liverpool kuendelea kushindana katika kiwango cha juu msimu ujao na baadaye,” amesema.
Slot alichukua nafasi ya Jurgen Klopp mwaka 2024, baada ya Mjerumani kuondoka baada ya miaka tisa. Alianza kwa ndoto wakati akipeleka Liverpool kwenye taji lake la 20 la ligi mbele ya mashabiki wa Anfield na michezo minne kabla ya mwisho wa msimu.
Katika barua yake, Slot pia alimkumbuka Diogo Jota, aliyefariki dunia katika ajali ya gari akiwa na ndugu yake Andre Silva. Slot amesema: “Kumpoteza Diogo hakuelezeki kwa maneno, lakini upendo, huruma na msaada wa familia ya Liverpool ulikuwa wa kipekee.”
Alimalizia kwa kusema: “Kuondoka kwangu klabuni kuna nitia hofu kid ogo, lakini najua klabu hii ita endelea kufanya watu wake wajivunie.
Katika mechi 113 alizoisimamia Liverpool, alishinda 69 alitoka sare 19 na kupoteza 28 alichukua ubingwa wa Ligi Kuu England mara moja.