Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Inter yatawala, Madrid yamaliza kazi Bernabeu

Muktasari:

  • Mwaka 2010, Mourinho aliionyesha dunia kwamba timu inaweza kutawala soka la Ulaya kwa ulinzi imara, kuwa na umiliki mdogo wa mpira na kusubiri muda sahihi wa kushambulia, baada ya kuiongoza Inter Milan kutwaa Ligi ya Mabingwa.

MADRID, HISPANIA: REAL Madrid walilazimika kupambana ili kuonyesha kiwango cha juu, wakitumia mbinu za Jose Mourinho na kuanza kampeni yao ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Inter Milan katika Uwanja wa Santiago Bernabeu.

Mwaka 2010, Mourinho aliionyesha dunia kwamba timu inaweza kutawala soka la Ulaya kwa ulinzi imara, kuwa na umiliki mdogo wa mpira na kusubiri muda sahihi wa kushambulia, baada ya kuiongoza Inter Milan kutwaa Ligi ya Mabingwa.

Ulikuwa mchezo wake wa mwisho akiwa kocha wa Inter, na miaka 16 baadaye, Mourinho amerudia mbinu hizo akiwa Real Madrid akiwaonyesha wachezaji wa zamani wa klabu hiyo kwamba mbinu zile bado zinafanya kazi.

Inter Milan walitawala umiliki wa mpira juzi na kupata nafasi nyingi zaidi za kufunga, lakini Madrid ya Mourinho ilionyesha uvumilivu na kusubiri hadi pale ilipopata nafasi za kuumiza.

Kwa upande mwingine, Inter walipaswa kujua hilo, hasa kwa sababu kocha wao Cristian Chivu alikuwa mchezaji chini ya Mourinho katika fainali ya Ligi ya Mabingwa 2010. Hata hivyo, ubora wa Real Madrid ulionekana kuwa jambo ambalo lingetokea wakati wowote.

Real Madrid iliingia kwenye mchezo huo ikiwa imetoka kupoteza kwa mara ya kwanza tangu Mourinho aanze kipindi chake kipya kwenye klabu hiyo, baada ya kufungwa 1-0 na Real Betis mwishoni mwa wiki iliyopita. Kulikuwa pia na mabadiliko kwenye kiungo cha Madrid, ambapo Trent Alexander-Arnold alipewa nafasi ya kucheza katikati ya uwanja.

Mwanzoni mwa mchezo, Inter waliwashambulia sana wenyeji wao na kupiga mashuti manne ndani ya dakika 11 za kwanza, na Marcus Thuram alikaribia kufunga kwa shuti la karibu, lakini kipa Thibaut Courtois alilidaka. Lautaro Martinez naye alimpigia shuti Courtois akiwa ndani ya eneo la hatari, lakini kipa huyo aliokoa. Ilionekana wazi kwamba mambo yalikuwa upande wa Inter, hadi pale kosa la safu ya ulinzi lilipoipa Real Madrid nafasi ya kupata bao, ambapo Brahim Diaz aliupokonya mpira kwa Yann Bisseck akampasia Kylian Mbappe aliyefunga.

Licha ya Inter kuendelea kumjaribu Courtois mara mbili katika dakika zilizofuata, Madrid waliongeza bao la pili dakika ya 23 kutokana na kosa jingine ambapo kipa Josep Martinez alicheza vibaya mpira ukatua kwa Federico Valverde aliyetumbukiza chuma ya pili.

Mabao hayo yaliathiri morali ya Inter, lakini bao walilopata kupitia Carlos Augusto dakika ya 77 liliwapa matumaini ya kulipiza kisasi mchezo ujao.