Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ile ya Mbeumo imekwisha bana!

Muktasari:

  • Staa huyo aliyekadhiwa jezi Namba 19, anaweza kucheza mechi yake ya kwanza Man United wikiendi hii wakati chama lake litakapokabiliana na West Ham United.

MANCHESTER, ENGLAND: HATIMAYE, Manchester United imempata staa wake iliyemsaka kwa muda mrefu kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi na sasa, Bryan Mbeumo atajiunga na wenzake kwa ajili ya ziara ya pre-season huko Marekani.

Staa huyo aliyekadhiwa jezi Namba 19, anaweza kucheza mechi yake ya kwanza Man United wikiendi hii wakati chama lake litakapokabiliana na West Ham United.

Baada ya kufunga mabao 20 kwenye Ligi Kuu England msimu uliopita, Mbeumo amekamilisha uhamisho wake wa Pauni 71 milioni, hivyo kwenda kumpa kocha Ruben Amorim uhakika wa mabao, ambapo ataunda safu mpya ya ushambuliaji sambamba na  Matheus Cunha, ambao watatumika namba 10 pacha kwenye 3-4-2-1.

Mabosi wa Man United wametumia muda mwingi sana kukamilisha dili hilo, likichukua wiki nane na kubaki wakiwa na hasira baada ya mabosi wa Brentford kutaka kumfanyia kitu kibaya Mbeumo kwa kumnyima uhamisho wa ndoto zake.

Tangu mara ya kwanza alipotambua Man United inamtaka, Mbeumo alielekeza moyo wake kwenda kukipiga Old Trafford, lakini, Man United imekasirika kwa sababu Brentford ilikuwa inapanga kumuuza kwingineko na kuweka dili hilo kwenye hatari ya kuvunjika. Brentford ilikuwa inampiga presha Mbeumo aende kwingineko.

Ilikuwa ikimtaka aende Newcastle United au Tottenham Hotspur. Arsenal nayo ilionesha dhamira ya kumsajili na Chelsea iliingia kwenye mpango dakika za mwisho.

Brentford pia inalalamikiwa kumpa presha Mbeumo apunguze mshahara wake ili wao wapate ada kubwa ya uhamisho, huku ikielezwa staa huyo atakwenda kulipwa mkwanja wa Pauni 200,000 kwa wiki huko Old Trafford.

Kocha mpya wa Spurs, Thomas Frank alihitaji huduma ya staa wake huyo wa zamani waende wote huko London kaskazini na mabosi wa Brentford waliona ni heri kumpeleka huko kuliko Man United. Jambo hilo liliwafanya Man United kumuahidi mshahara mkubwa Mbeumo ili kuwazidi kete wapinzani wao. Baada ya hapo, ishu ilikuwa kwenye makubaliano ya klabu, ambapo ofa ya kwanza ilikuwa Pauni 45 milioni pamoja na bonasi ya Pauni 10 milioni. Brentford ilijua itapata pesa nyingi kutoka Spurs, lakini mchezaji mwenyewe alisisitiza anataka kwenda Man United.

Hapo iliwafanya Brentford kudai kwamba inahitaji kulipwa zaidi ya Pauni 62.5 milioni, ambazo Man United ililipa huko Wolves kupata huduma ya Cunha.

Baada ya vuta nikuvute, hatimaye dili la Pauni 71 milioni lilifikiwa, licha ya Brentford kuhitaji kulipwa Pauni 70 milioni kwanza na kisha nyongeza ya Pauni 7 milioni. Lakini, sasa Man United, italipa Pauni 65 milioni kwa awamu nne na kisha bonasi ya Pauni 6 milioni.