Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ile pyee EPL... Moto huoo Man United na Arsenal

RATIBA Pict

Muktasari:

  • Mechi hiyo yenye historia ya kutosha kwenye soka la England inatarajiwa kuvutia wengi kutokana na kukutanisha vigogo wenye rekodi nzuri katika michuano hiyo. Kipute chenyewe kitapigwa, Jumapili, Agosti 17.

LONDON, ENGLAND: IMERUDI tena. Ndicho unachoweza kusema baada ya ratiba mpya ya Ligi Kuu England msimu wa 2025-26 kutangazwa, huku Manchester United na Arsenal zikimenyana kwenye wikiendi ya kwanza kabisa ya mikikimikiki hiyo ya msimu ujao.

Mechi hiyo yenye historia ya kutosha kwenye soka la England inatarajiwa kuvutia wengi kutokana na kukutanisha vigogo wenye rekodi nzuri katika michuano hiyo. Kipute chenyewe kitapigwa, Jumapili, Agosti 17.

Arsenal ilihuzunika kumaliza msimu uliopita bila taji lolote, ambapo ilishika nafasi ya pili nyuma ya Liverpool iliyobeba ubingwa wa ligi hiyo kwa tofauti ya pointi 10. Chama hilo la Mikel Arteta litakapomalizana na Man United katika wikiendi ya kwanza, litakwenda Anfield kukipiga na Liverpool kwenye wikiendi ya tatu na kufuatia kipute na Manchester City. Mechi sita za kwanza Arsenal itakipiga na Man United, Leeds United, Liverpool, Nottingham Forest, Man City na Newcastle United.

Na katika kipute cha Man United, Arteta anaweza kukutana na kikosi tofauti kabisa cha kocha Ruben Amorim, ambaye kwa sasa anapambana kuijenga upya timu yake kabla ya mechi hiyo ya Old Trafford.

Katika msimu huo mpya, Man United nayo imepangiwa ratiba inayohitaji ujanja mwingi kupenya na hivyo kumwondoa kwenye presha kubwa kocha wao Amorim. Mechi sita za kwanza za Man United, itakapomalizana na Arsenal itakipiga na Fulham, Burnley, Man City, Chelsea na Brentford.

Mabingwa watetezi, Liverpool chini ya kocha Arne Slot wataanza kampeni ya kutetea taji lao kwa kumenyana na Bournemouth, Ijumaa ya Agosti 15. Bila shaka mechi hiyo ya Anfield itavutia mashabiki wengi ambao watakwenda kuitazama timu yao inaanza vipi vita ya kutetea taji.

Lakini, wasiwasi wa mashabiki wa Liverpool upo kwenye kumpoteza mkali Mo Salah wakati wa michuano ya AFCON wakati huo wakiwa kwenye ratiba ngumu za Ligi Kuu England, ambapo timu hiyo itasafiri kwenda Emirates kukamilisha Arsenal bila ya huduma ya mkali huyo wa Misri, Januari 7.

Mo Salah anaweza kukosa pia mechi za Wolves, Leeds, Fulham na Burnley - ambapo kwenye karatasi hazionekani kama ni ratiba ya mechi tishio sana kwa wababe hao wa kocha Mdachi Slot.

Kwa Jumamosi ya kwanza ya msimu, mechi ya mapema itashuhudiwa Aston Villa ikikipiga na Newcastle United, timu mbili ambazo kwa msimu uliopita zilichuana jino kwa jino kwenye kuwania tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya, ambapo Magpies ilimaliza juu.

Mechi nyingine za siku hiyo ya Jumamosi, Brighton itakuwa nyumbani kucheza na Fulham, wakati Nottingham Forest, iliyokuwa moto msimu uliopita itakipiga na Brentford, ambao hawatakuwa na kocha Thomas Frank, aliyetimkia zake Tottenham Hotspur, ambayo pia itakuwa na kasheshe la kukipiga na Burnley siku hiyo.

Sunderland iliyorejea kwenye Ligi Kuu England mechi yake ya kwanza itakuwa nyumbani kucheza na West Ham United, huku Brighton ikicheza na Fulham na mechi ya mwisho ya Jumamosi, Man City itakuwa ugenini kukipiga na Wolves.

Kwa mechi za Jumapili, Chelsea itashuhudia ikianza msimu nyumbani Stamford Bridge kwa kukipiga na mabingwa wa Kombe la FA, Crystal Palace. Kwa msimu uliopita, timu hizo mbili zilitoka sare ya bao 1-1 katika mechi zote mbili. Baada ya mechi hiyo, ndipo kitakaposhuhudiwa kipute cha kibabe kwenye siku hiyo ya Jumapili, huko Old Trafford, ambapo Arsenal itakuwa ugenini kuwakabili mahasimu wao Man United.

Leeds United yenyewe itasubiri hadi Jumatatu kucheza na Everton huko Elland Road katika moja ya mechi zinazotazamiwa kuwa na upinzani mkali, huku David Moyes na chama lake la Everton, mechi yao ya kwanza kwenye uwanja mpya itakuwa wikiendi inayofuatia dhidi ya Brighton.