Prime
Ifahamu Suruali inayotibu misuli wachezaji

Muktasari:
- Kuzuia vitu kama hivyo. Teknolojia inatumika kupunguza machungu baada ya kutengenezwa kwa suruali maalumu za kitiba, ambazo kazi yake ni kuifanya misuli kuwa kwenye utimamu wake pindi mchezaji anapohisi maumivu au akitoka kucheza mechi iliyomhitaji kukimbia sana uwanjani. Mpango wa sasa ni suruali tiba.
LONDON, ENGLAND: SI habari nzuri kabisa kuzisikia. Una mechi muhimu, kisha unasikia timu yako itamkosa mchezaji muhimu kabisa kwenye kipute hicho kwa sababu ya tatizo la misuli.
Kuzuia vitu kama hivyo. Teknolojia inatumika kupunguza machungu baada ya kutengenezwa kwa suruali maalumu za kitiba, ambazo kazi yake ni kuifanya misuli kuwa kwenye utimamu wake pindi mchezaji anapohisi maumivu au akitoka kucheza mechi iliyomhitaji kukimbia sana uwanjani. Mpango wa sasa ni suruali tiba.
Staa wa soka, Thiago Silva alionekana kuvaa suruali hiyo, teknolojia inayoonekana kuwafikia wengi ikiwamo mabondia, wacheza kriketi na rugby.

Teknolojia hiyo imeemua maarufu na ilianza hivi. Straika kinda wa Stoke City, Ryan Brunt, alipata maumivu ya misuli ya goti wakati akiwa na umri wa miaka 16.
Madaktari wa klabu walimshauri apumzike sana, aweke barafu na matibabu mengine wakati alipoanza miezi 12 ya kujitibu ili kurudi uwanjani.
Kwenye uwanja wa mazoezi wa Stoke City nako kuliweka mashina maalumu ambazo zilitumika kufungwa kwenye miguu yake ili kuipa presha, lakini Brunt, alihitaji tiba ya haraka itakayomfanya apone kwa wepesi na kurudi uwanjani mapema.
Katika mpango wake huo wa kutaka kurudi kwenye utimamu wa mechi kwa haraka, Brunt alitumikia muda wake mwingine kuperuzi kwenye tovuti mbalimbali na ndipo hapo alipokutana na kitu kinaitwa NormaTec, ambayo ilikuwa inatengeneza viatu vya kurahisisha kupona majeraha kwa haraka.
Brunt, sasa 31, aliitaka kampuni hiyo yenye maskani yake Massachusetts kama inaweza kumtumia kifaa hicho. NormaTec ilikumbali kumtumia Brunt alichotaka.
“Ile ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kutumia NormaTec,” alisema Brunt mwaka 2018.
“Nimekuwa nikutumia kwa zaidi ya miaka minane, kila nilipohisi maumivu ya goti.”
Kifaa hicho kinachovaliwa miguuni kama suruali kinasaidia wanamichezo kupona haraka maumivu ya misuli kwa kulegeza kukaza kwa misuli hiyo na kurahisisha mzunguko wa damu.

“NormaTec ni kifaa kinachotibu kwa hewa. Ni kama kinafanya masaji. Kinafanya kuanzia kwenye kifundo cha mguu hadi kwenye goti. Inatoa asidi na sumu zote kwenye mfumo wako na kuweka oksijeni ambayo inasaidia kupona kwa haraka majeraha na uchovu.”
Baada ya Brunt kupata faida kubwa ya kitiba kutoka kwa suruali hiyo, wachezaji wenzake kibao nao wakaanza kuitumia tiba hiyo.
Wanasoka kibao wakaanza kuitumikia tiba hiyo ya kuvaa suruali maalumu. Na haikuishia kwa wanasoka tu, bali hata mabondia nao walikimbilia kwenye tiba hiyo kuweka sawa misuli yao ya miguu, akiwamo bondia maarufu wa England, Anthony Joshua.
Bondia, Joshu alivaa jezi hiyo wakati anajiandaa na pambano lake na Wladimir Klitschko la kuwania ubingwa wa WBA na IBO wakati huo.
Mastaa waliokuwa wakisumbuliwa sana na maumivu ya misuli kama Antonio Valencia, Gareth Bale, Saido Berahino na wengine akiwamo Mbrazili, Thiago Silva alitumia sana tiba hiyo ya kuvaa suruali tiba ili kujiweka kwenye utimamu wa misuli ya miguu.
Kwa bondia Joshua, mwanamichezo ambaye mchezo wake unategemea zaidi mikono kuliko miguu, NormaTec ilimwengezea kifaa kingine maalumu ili kuhakikisha anajiweka vizuri kotekote kwa kuvaa suruali hiyo. Suruali hiyo inatumia nishati ya umeme, ambapo mtumiaji ataweka vipimo anavyohitaji kulingana na anavyojisikia.

Nahodha wa zamani waChelsea, John Terry ni mchezaji mwingine ambaye alikuwa akiamini katika ubora wa matibabu ya suruali hiyo ya NormaTec. Alitumia zaidi tiba hiyo wakati alipokuwa kwenye kikosi cha Aston Villa na alikwenda nyakati ambazo miguu yake tayari ilishaanza kuchoka.
Paul Pogba aliwahi kuvaa suruali hiyo kama ambavyo aliwahi kufanya Jordan Henderson.