Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Huu hapa mzigo wa Afrika Kombe la Dunia la Klabu

AFRIKA Pict

Muktasari:

  • Hata hivyo, kuna mengi ya kutazama kuanzia ratiba, viwanja, muda na hata rekodi ya timu kutoka bara hili ambazo zimewahi kushiriki michuano hii. Hapa tumekuwekea kila kitu.

FLORIDA, MAREKANI: WANASEMA nyumbani kwanza. Licha ya utitiri wa mastaa watakaokuwepo Marekani na timu mbalimbali kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia la Klabu, mashabiki wengi kutoka Afrika watakuwa na hamu ya kuona mastaa wao na timu zao zitafanya nini.

Hata hivyo, kuna mengi ya kutazama kuanzia ratiba, viwanja, muda na hata rekodi ya timu kutoka bara hili ambazo zimewahi kushiriki michuano hii. Hapa tumekuwekea kila kitu.


KILICHOWAPA NAFASI

Timu hizi zimefuzu kutokana na ubora wao katika michuano ya kimataifa hususan Ligi ya Mabingwa Afrika na katika ngazi za viwango za CAF, Al Ahly ndiyo inayoongoza kwa pointi (140) ikiwa bingwa mara tatu wa Ligi ya Mabingwa Afrika katika miaka minne, Wydad AC inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi 108 ambazo nyingi ilizipata baada ya kushinda Ligi ya Mabingwa Afrika 2021-22, Esperance de Tunis ilifukuzu ikiwa nafasi ya tatu kwa 100 huku Mamelodi Sundowns nafasi ya nne kwa pointi 98.


REKODI ZAO


Al Ahly SC

Unaweza kuitaja kama ndiyo timu bora zaidi kwa sasa Afrika. Kijumla ndiyo ilishiriki michuano hii mara nyingi zaidi kuliko timu yoyote. Imeshiriki mara tisa, ikiwemo mwaka 2005, 2006, 2008, 2012, 2013, 2020, 2021, 2022 na 2023.

Wababe hawa kutoka Misri waliwahi kushika nafasi ya tatu mara tatu, mwaka 2006, 2020 na 2021 na imeshinda jumla ya mechi nane kati ya 22 zilizochezwa.

Hii inafanya Ahly kuwa ndiyo timu yenye mafanikio makubwa zaidi barani Afrika katika mashindano haya.


TP Mazembe

Iliandika historia kwa kuwa timu ya kwanza ya Afrika kufika fainali mwaka 2010 na ilipoteza kwa Inter Milan. Ilishiriki mwaka 2009 na 2010 na ilicheza jumla ya mechi tano, wakishinda mbili.


Raja Casablanca

Ilishiriki mwaka 2000 na 2013, lakini mwaka 2013 ilifika fainali na kupoteza kwa Bayern Munich. Ilicheza jumla ya mechi tano na imeshinda mara mbili.


Wydad Casablanca

Imewahi kushiriki mara mbili, mwaka 2017 na 2022, lakini haijawahi kushinda mechi yoyote, imepoteza mechi mbili na kupata sare moja kati ya mechi tatu ilizocheza.

Rekodi hii mbaya inatia mashaka katika michuano ya mwaka huu ingawa inaonekana kufanya usajili wa kishindo kuhakikisha inafanya vizuri.


Esperance de Tunis

Ilishiriki mwaka 2011, 2018 na 2019 na kiujumla imecheza mechi sita na ikashinda moja pekee na kupoteza tano.

Mafanikio makubwa iliyapata mwaka 2019 iliposhika nafasi ya tano baada ya kuibuka na ushindi dhidi ya Al-Sadd.


Mamelodi Sundowns

Ilishiriki mwaka 2016, ikicheza mechi mbili, ikashinda moja na kupoteza mbili. Ushindi wao ulikuwa dhidi ya Jeonbuk Hyundai Motors, lakini ilipokea  kichapo cha mabap 2-0 dhidi ya Kashima Antlers ya Japan katika mechi hiyo ya robo fainali.