Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hukumu ya Perez, Riquelme ni leo

Muktasari:

  • Klabu hiyo yenye thamani kubwa na mafanikio makubwa katika soka duniani itafanya uchaguzi wake leo ya Jumapili.

BARCELONA, HISPANIA: KWA MARA ya kwanza katika kipindi cha miaka 20, utawala wa Florentino Perez ndani ya Real Madrid utakabiliwa na changamoto kupitia sanduku la kura.

Klabu hiyo yenye thamani kubwa na mafanikio makubwa katika soka duniani itafanya uchaguzi wake leo ya Jumapili.

Perez, mwenye umri wa miaka 79, ambaye kwa zaidi ya robo karne ameifanya Real Madrid kuwa nguvu kubwa ya kimataifa ya soka, atakabiliana na mpinzani mwenye umri wa karibu nusu yake anayetoa ahadi kubwa ili kuwashawishi wanachama karibu 98,000 wa klabu hiyo wafikirie kufanya mabadiliko ya uongozi.

Enrique Riquelme, mwenye umri wa miaka 37 alikuwa mtoto wakati Perez aliposhika madaraka kwa mara ya kwanza.

Wapenzi wengi wa Madrid hawakumfahamu hadi alipojitokeza kugombea urais baada ya Perez kuitisha uchaguzi wa mapema mwezi uliopita katika mkutano wa waandishi wa habari uliotawaliwa na madai yake kwamba vyombo vya habari vya Hispania vinajaribu “kuua” sababu ya urais wake.

“Kwa nini wanataka kuniangamiza? Kwa nini? Kwa sababu kuna vijana wanaosema wanataka kugombea? Basi wagombee. Ningefurahi sana kufanya hivyo,”  alisema Perez kwa hasira Mei 12, mwaka huu.

Riquelme, ambaye ni mtendaji katika sekta ya nishati jadidifu, amefanikiwa kushangaza wengi kwa kujijengea nafasi ya ushindani wa kweli. Hilo limechangiwa na kuungwa mkono na baadhi ya nyota wa zamani wa Real Madrid pamoja na ahadi za usajili mkubwa, ikiwemo madai ya kumleta Erling Haaland kutoka Manchester City.


RIQUELME ANA MAJINA MAKUBWA, JE ANA USHAWISHI WA KUTOSHA?

Kampeni ya Riquelme ilipata nguvu baada ya kuungwa mkono na magwiji wa Madrid kama Raul Gonzalez, Iker Casillas na Fernando Hierro.

Katika mipango ya Riquelme ameweka mipango ya safu yake ya uongozi kwa Raul kuwa mkurugenzi wa michezo wa klabu, nafasi ambayo kwa sasa haipo ndani ya Real Madrid. Hierro angeongoza akademi ya vijana, huku jukumu la Casillas likiwa halijawekwa wazi.

Riquelme pia amesema anataka kumsajili kiungo wa Hispania Rodri, ambaye amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake na Manchester City.

Lakini ahadi yake kubwa zaidi imekuwa madai kwamba Haaland anataka kujiunga na Real Madrid.

“Nikichaguliwa kuwa rais wa Real Madrid, Haaland atacheza Real Madrid,” alisema Riquelme katika televisheni ya taifa ya Hispania siku ya Alhamisi.

Hata hivyo, wakala wa Haaland, Rafaela Pimenta, alikanusha taarifa hizo.

“Inafurahisha kusikia, lakini si kweli. Tunawatakia wagombea wote wawili kila la heri katika uchaguzi wa Madrid.”

Perez naye alijibu kwa kifupi: “Lazima huo ni mchezo wa kisiasa.”

Perez bado ana hadhi kubwa ndani ya Madrid


PEREZ HAKUTAKA KUBAKI NYUMA KATIKA VITA VYA AHADI.

Alitangaza kuwa wiki ijayo, baada ya uchaguzi, atatangaza usajili ambao utakuwa ghali zaidi katika historia ya Real Madrid, wenye thamani ya angalau Euro150 milioni.

Perez ana historia ya kutimiza ahadi ambazo mwanzoni zilionekana haziwezekani.

Baada ya kushinda uchaguzi wake wa kwanza mwaka 2000, Perez alianzisha sera ya ‘Galacticos’ , iliyohusisha kusajili mastaa wa gharama kubwa na wenye hadhi kubwa duniani kama Luis Figo kutoka Barcelona, jambo ambalo alilitekeleza, David Beckham na Zinedine Zidane, Ronaldo De Lima, Cristiano Ronaldo na hivi karibuni Kylian Mbappe.

Pia ameahidi kumrudisha kocha Jose Mourinho na kuwasajili Ibrahima Konate wa Liverpool FC na Denzel Dumfries wa Inter Milan.


REKODI YA MAFANIKIO SILAHA YAKE KUBWA

Katika vipindi vyake viwili vya uongozi (2000-2006 na 2009 hadi sasa), Real Madrid imeshinda mataji saba kati ya 15 ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambayo klabu hiyo imewahi kutwaa.

Pia imeshinda mataji saba ya La Liga na matatu ya Copa del Rey.

Mafanikio hayo yamekwenda sambamba na ukuaji mkubwa wa kifedha, ambapo Real Madrid imekuwa chapa ya kimataifa yenye thamani kubwa. Kwa misimu mitano mfululizo, imeongoza orodha ya Forbes ya vilabu vya soka vyenye thamani kubwa zaidi duniani.


UDHAIFU WA PEREZ

Hata hivyo, Perez hajakosa changamoto.

Mradi wake wa European Super League uliolenga kubadilisha mfumo wa soka la Ulaya na kuchukua nafasi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ulipata upinzani mkubwa kutoka kwa mashabiki, klabu dogo na UEFA.

Pia dau lake la kumleta Mbappe bado halijaleta mafanikio yaliyotarajiwa, kwani katika misimu miwili tangu nyota huyo ajiunge na Madrid, klabu hiyo haijashinda taji kubwa lolote.

Katika kipindi hicho, Perez ameachana na makocha watatu ambao ni Carlo Ancelotti, Xabi Alonso na Alvaro Arbeloa.