Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Huko Barca... Huku Rashford, kule Yamal

RASHFORD Pict

Muktasari:

  • Rashford hajaichezea Man United tangu Desemba 2024 baada ya kutibuana na kocha Amorim kutokana na kiwango chake cha mazoezi kuwa cha kichovu na hivyo kupelekwa kwa mkopo Aston Villa, ambako alionyesha kiwango kizuri kwenye nusu ya pili ya msimu uliopita.

BARCELONA, HISPANIA: BARCELONA imekamilisha dili la mkopo la kumnasa Marcus Rashford, ikimsaidia staa huyo wa England kichaka cha kwenda kujificha baada ya kupigwa chini huko Manchester United na kocha Ruben Amorim.

Rashford hajaichezea Man United tangu Desemba 2024 baada ya kutibuana na kocha Amorim kutokana na kiwango chake cha mazoezi kuwa cha kichovu na hivyo kupelekwa kwa mkopo Aston Villa, ambako alionyesha kiwango kizuri kwenye nusu ya pili ya msimu uliopita.

Lakini, sasa Rashford, 27, amepata nafasi ya kwenda kuonyesha ubora kwenye timu kubwa yenye mastaa kama Lamine Yamal na Raphinha na kunolewa na kocha mwenye viwango vya juu, Hansi Flick.

Barcelona italipa mshahara wote wa Rashford kwa kipindi chake atakachokuwa kwa mkopo kwenye timu hiyo, ambapo staa huyo amekubali kushusha mshahara wake anaolipwa Pauni 325,000 kwa wiki.

Barca itahitaji kulipa Pauni 26 milioni kumbeba jumla Rashford mwishoni mwa msimu ujao na sasa kinachoelezwa ni namna gani staa huyo atakwenda kufiti kwenye kikosi hicho cha Nou Camp kilichosheheni mastaa kibao wenye vipaji vya hali ya juu.

Rashford ameibuka kwenye mpango wa Barcelona baada ya kukwama kwenye dili lao la kumsajili Nico Williams, ambaye amesaini mkataba wa miaka 10 kwenye klabu ya Athletic Bilbao. Barca ilishinda ubingwa wa La Liga kwenye msimu wa kwanza wa kocha Flick na sasa wanahitaji kufanya kweli kwenye michuano ya Ulaya, ambapo kwenye dirisha hili ukimweka kando Rashford imefanya usajili pia wa kipa Joan Garcia na mshambuliaji wa Copenhagen, Roony Bardghji.

Mtihani wa kwanza kwa Rashford ni kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Nou Camp, ambao watu anaochuana nao ni mawinga Yamal na Raphinha.

Yamal anatajwa kama mmoja wa wachezaji bora duniani kwa sasa, ambapo kinda huyo alifunga mabao 18 na kuasisti 16 kwenye michuano yote msimu uliopita, wakati Raphinha, naye alikuwa na kiwango bora, alipofunga mabao 34 na asisti 17. Rashford naye si kama hajiwezi, amefunga mabao 138 katika mechi 426 alizochezea Man United, huku akifunga 17 katika mechi 62 alizochezea England.

REKODI ZA RASHFORD NA MAKOCHA WAKE HUKO MAN UNITED

-Ole Gunnar Solskjaer - mechi 135, mabao 55

-Jose Mourinho - mechi 125, mabao 28

-Erik ten Hag - mechi 113, mabao 42

-Ralf Rangnick - mechi 22, mabao 2

-Louis van Gaal - mechi 18, mabao 8

-Ruben Amorim - mechi 6, mabao 3

-Ruud van Nistelrooy - mechi 4, mabao 0

-Michael Carrick - mechi 3, mabao 0