Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hugo Ekitike aingia katika anga za Arsenal

TETESI Pict

Muktasari:

  • Ekitike ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika 2029,msimu uliopita alicheza mechi 48 za michuano yote na kufunga mabao 22.

ARSENAL imeingia katika vita dhidi ya Chelsea, Liverpool na Manchester United kwenye harakati za kumsajili mshambuliaji wa Eintracht Frankfurt na timu ya taifa ya Ufaransa, Hugo Ekitike mwenye umri wa miaka 23, katika dirisha hili.

Ekitike ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika 2029,msimu uliopita alicheza mechi 48 za michuano yote na kufunga mabao 22.

Mabosi wa Arsenal wanapambana kupata huduma ya mshambuliaji katika dirisha hili na wanawekeza nguvu zaidi kwa Ekitike kwa sababu Benjamin Sesko na Viktor Gyokeres waliokuwa wanatakiwa kuona kuna ugumu kuwapata.

Upande wa Ekitike, Frankfurt inadaiwa wako tayari kumuuza ikiwa tu watapata ofa sahihi.


Marc Guehi
JLIVERPOOL iko tayari kumtumia winga raia wa  Scotland mwenye umri wa miaka 19, Ben Doak, kama sehemu ya ofa kwa ajili ya kumsajili beki kisiki wa Crystal Palace na timu ya taifa ya England, Marc Guehi, mwenye umri wa miaka 24 katika dirisha hili la usajili linaloendelea huko Ulaya. Guehi ni miongoni mwa mastaa wanaowindwa na timu nyingi Ulaya.


James McAtee
BORUSSIA Dortmund, Bayer Leverkusen, Eintracht Frankfurt, RB Leipzig na Stuttgart zimeonyesha nia ya kumsajili kiungo wa Manchester City mwenye umri wa miaka 22, James McAtee, anayeichezea timu ya taifa ya vijana ya England chini ya umri wa miaka 21. Mkataba wa sasa wa McAtee unatarajiwa kumalizika mwakani. Msimu uliopita alicheza mechi 27 za michuano yote.


Moise Kean
MANCHESTER United bado ina nia ya kumsajili mshambuliaji wa Fiorentina, Moise Kean, raia wa Italia, 25, katika dirisha hili lakini itatakiwa kukamilisha dili hilo kabla ya Julai 15. Mkataba wa Kean una kipengele kinachomruhusu kuondoka ikiwa timu inayomtaka italipa Euro 52 milioni lakini kitaisha Julai 15 na baada ya hapo Fiorentina itahitaji dau lolote inalotaka.


Patrik Schick
INAELEZWA timu kibao za Ligi Kuu England na Serie A zimeulizia uwezekano wa kuipata huduma ya mshambuliaji wa Bayer Leverkusen na Jamhuri ya Czech, Patrik Schick, 29. Taarifa ya tovuti ya Skysports inadai Leverkusen haitaki kumuuza staa huyo kwa sasa kwani wanaona watakuwa wanaivunja timu nzima kwa kuwa kuna kundi kubwa la wachezaji tayari wameshaondoka.


Thomas Partey 
KIUNGO wa kimataifa wa Ghana, Thomas Partey alikuwa mchezaji huru jana baada ya mkataba na Arsenal kumalizika na kushindwa kufikia mwafaka juu ya kusaini mpya kuendelea kusalia. Partey mwenye umri wa miaka 32, ameripotiwa kutofikia mwafaka wa kusaini mkataba mpya na Arsenal kwa sababu pesa ambayo anaitaka ni kubwa tofauti na ile ambayo Arsenal ipo tayari kuitoa.


Igor Jesus
NOTTINGHAM Forest ipo karibu kumsajili mshambuliaji wa Batafogo na timu ya taifa ya Brazil  mwenye umri wa miaka 24, Igor Jesus, kwa ada ya pauni 10 milioni katika dirisha hili. Benchi la ufundi la Forest limevutiwa na kiwango cha Jesus ambaye msimu uliopita alicheza mechi 29 za michuano yote na kufunga mabao tisa katika ligi.


Tyrell Malacia
TAARIFA zinaeleza Manchester United iko tayari kukubali ofa ya chini kwa ajili ya kumuuza beki wa kimataifa wa Uholanzi, Tyrell Malacia, 25, baada ya PSV Eindhoven kuamua kutomsainisha mkataba wa  kudumu  kufuatia kuitumika kwa mkopo dirisha lililopita. Malacia mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwakani.