Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hii kali! England yaanda gwaride la ubingwa wa Kombe la Dunia

PAREDI Pict

Muktasari:

  • Siku nne kabla ya kuanza kwa Kombe la Dunia nchini Marekani, Mexico na Canada, Serikali ya Uingereza inadaiwa kuwa inafanya maandalizi ya siri ya gwaride kubwa lenye gharama ya takribani pauni 500,000 ikiwa timu ya taifa ya England itashinda Kombe la Dunia la 2026.

LONDON, ENGLAND: HII kali! Serikali ya England inaanda kimyakimya gwaride kubwa lenye thamani ya Pauni 500,000, ikiwa England itashinda Kombe la Dunia.

Siku nne kabla ya kuanza kwa Kombe la Dunia nchini Marekani, Mexico na Canada, Serikali ya Uingereza inadaiwa kuwa inafanya maandalizi ya siri ya gwaride kubwa lenye gharama ya takribani pauni 500,000 ikiwa timu ya taifa ya England itashinda Kombe la Dunia la 2026.

Maafisa wa serikali wamepewa jukumu la kuandaa sherehe za kitaifa kwa kuzingatia uwezekano wa kikosi kinachonolewa na kocha Thomas Tuchel kufika mbali na kutwaa ubingwa wa dunia.

Mipango inaendelea kwa ajili ya moja ya gwaride kubwa zaidi kuwahi kufanyika nchini Uingereza, ambalo linatarajiwa kupita katikati ya London katika wiki inayofuata fainali ya Julai 19.

Idara ya Utamaduni, Vyombo vya Habari na Michezo ya Uingereza (DCMS) tayari inaandaa tarehe ya tukio hilo siku chache baada ya fainali.

PARE 01

Hatua hii imekuja baada ya Serikali na Chama cha Soka cha England (FA) kuandaa kwa haraka gwaride la kusherehekea mafanikio ya timu ya wanawake ya England, baada ya kutetea ubingwa wao wa Euro mwaka 2025.

Inadaiwa kuwa maafisa wa Whitehall wamekuwa wakishauriana kwa njia isiyo rasmi na FA kuhusu namna bora ya kusimamia umati unaoweza kufikia mamilioni ya watu.

Tayari makumi ya maelfu ya pauni yameshatumika katika maandalizi ya awali, ikiwa ni pamoja na kununua basi la ghorofa mbili kwa ajili ya gwaride, jukwaa kubwa la sherehe na burudani za moja kwa moja.

Vyanzo vinaeleza kuwa gharama ya jumla inaweza kufikia pauni 500,000, lakini inaonekana kuwa matumizi yenye thamani kutokana na mchango wake katika kuinua ari ya taifa iwapo England itashinda Kombe la Dunia.

PARE 02

Maafisa pia wanachunguza jinsi nyota wa timu hiyo kama Harry Kane na Jude Bellingham watakavyoweza kurejea haraka kutoka Marekani ikiwa England itafanikiwa kuwa mabingwa wa dunia kwa mara ya pili tangu mwaka 1966.

Inatarajiwa kuwa kikosi hicho kitarejea nyumbani siku moja au mbili baada ya fainali, kabla ya kuwasilishwa rasmi kwa umma kama mabingwa wa dunia.

Chanzo kimoja kimesema: “Ikiwa England itashinda Kombe la Dunia na hakutakuwa na mpango wowote wa sherehe, basi Serikali na FA wataonekana kama hawakuwa wamejiandaa.”

PARE 03

Gwaride hilo linaweza kufanana na sherehe za ushindi za Lionesses mwaka jana, ambazo zilihudhuriwa na watu zaidi ya 65,000 katikati mwa London.

DCMS ilisema: “Kwa sasa, ni mapema sana kuzungumzia sherehe zinazowezekana, lakini bila shaka tutasherehekea mafanikio kwa namna inayostahili.”


England yaichapa New Zealand

Katika maandalizi ya Kombe la Dunia, Kocha Thomas Tuchel alipanga vikosi viwili tofauti katika kila kipindi cha mchezo wa kirafiki dhidi ya New Zealand uliochezwa Tampa, Marekani.

Nahodha Harry Kane aliifungia England bao lake la 79 katika mechi yake ya 113 kimataifa kwa kichwa sekunde chache kabla ya mapumziko.

PARE 04

Baada ya hapo, Tuchel alifanya mabadiliko mengi ili kuwapa nafasi karibu wachezaji wote wa kikosi chake kabla ya mechi ya kwanza ya hatua ya makundi dhidi ya Croatia itakayochezwa Dallas tarehe 17 Juni.

Winga wa miaka 17 wa Liverpool FC, Rio Ngumoha, ambaye hayupo kwenye kikosi rasmi cha wachezaji 26 wa Kombe la Dunia, alipata nafasi yake ya kwanza kuichezea England na kuwa mchezaji wa tano mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kuichezea timu hiyo.

Kutokana na hali ya joto kali ya Florida, mchezo huo ulikuwa wa kiwango cha chini kwa ushindani, lakini ulisaidia wachezaji kuzoea mazingira watakayokutana nayo wakati wa mashindano.

Tuchel hakutaka kuhatarisha wachezaji wake katika hali hiyo ya hewa, hivyo lengo kuu lilikuwa kuwapa dakika za kucheza na kuwasaidia kuzoea mazingira ya Marekani.

Beki John Stones alipata dakika 45 baada ya msimu uliokumbwa na majeraha akiwa na Manchester City, huku akitarajiwa kuwa sehemu muhimu ya mipango ya Tuchel ikiwa ataendelea kuwa fiti.

PARE 05

Morgan Rogers alipewa nafasi ya kwanza katika nafasi ya namba 10, lakini baada ya mapumziko, Jude Bellingham alipoingia uwanjani alikabidhiwa kitambaa cha unahodha na kuonyesha kuwa ndiye anayetarajiwa kucheza nafasi hiyo katika mashindano.

Kama ilivyokuwa kawaida, Harry Kane alionyesha umuhimu wake kwa England kwa kufunga bao la ushindi kupitia kichwa kizuri kilichotokana na krosi ya Djed Spence. Bao hilo lilikuwa la 67 kwake katika msimu huu kwa klabu na timu ya taifa.

Ngumoha naye alivutia katika kipindi cha pili, akionyesha dalili za kuwa na mustakabali mkubwa na kumpa Tuchel jambo la kufikiria ikiwa kutatokea majeraha kabla ya Kombe la Dunia kuanza.

Kwa msingi huo, pamoja na ushindi walioupata, ilikuwa siku yenye mafanikio kwa England katika maandalizi yao ya Kombe la Dunia.