Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hatimaye! Fury, Joshua kuzichapa Desemba 11

PAMBANO Pict

Muktasari:

  • Pambano hilo ambalo limekuwa likisubiriwa kwa miaka mingi, awali lilikuwa likielekea kufanyika New York, Marekani, lakini msimamo wa Joshua kuhusu mkataba wake umeifanya vita hiyo ya Waingereza kurejea nyumbani.

CARDIFF, WALES: HATIMAYE! Ndoto ya mashabiki wa ndondi ya kuwaona Tyson Fury na Anthony Joshua wakikutana ulingoni imekuwa kweli baada ya pambano hilo kusainiwa na kuthibitishwa kufanyika Desemba 11 mwaka huu katika Uwanja wa Principality, Cardiff, Wales.

Pambano hilo ambalo limekuwa likisubiriwa kwa miaka mingi, awali lilikuwa likielekea kufanyika New York, Marekani, lakini msimamo wa Joshua kuhusu mkataba wake umeifanya vita hiyo ya Waingereza kurejea nyumbani.

Joshua, 36, alisimamia masharti ya mkataba wake, ambao ulikuwa tofauti na ule uliosainiwa na Fury mwenye umri wa miaka 38, jambo lililosaidia kuhakikisha pambano hilo linapigwa nchini Uingereza.

Sehemu ya fedha za pambano hilo imefadhiliwa na Netflix, huku mtandao huo wa Marekani ukiandaa pambano kuu kuanza saa 2:00 usiku kwa saa za Uingereza, muda unaolenga pia kuwavutia watazamaji wa Marekani.

PAMB 03

Pambano hilo litafanyika wakati wa kipindi cha Krismasi, hali iliyozua hofu kwamba mvua au theluji inaweza kuathiri tukio hilo kubwa.

Hata hivyo, Uwanja wa Principality una paa linaloweza kufungwa kikamilifu, tofauti na Uwanja wa Wembley ambao paa lake hufunika sehemu tu. Hilo linatarajiwa kuwakinga mashabiki wanaokadiriwa kufikia 75,000 dhidi ya mvua au baridi kali wakati wa pambano hilo.

Hatimaye, mwenyekiti wa Mamlaka ya Burudani ya Saudi Arabia, Turki Alalshikh, ndiye aliyethibitisha rasmi pambano hilo kupitia mitandao ya kijamii.

Alalshikh alisema: “Kwa miaka 15 hakuna aliyefanikiwa kulifanya pambano hili.

PAMB 04

“Aprili nilisema kwamba tangazo lolote kuhusu pambano hili lingetoka kwangu. Sasa naweza kuthibitisha kwamba Fury dhidi ya Joshua itafanyika Uingereza, kama nilivyoahidi mashabiki wa ndondi wa Uingereza. Muda wa kuzungumza umekwisha.”

Baadaye Alalshikh alichapisha bango rasmi la pambano hilo lenye neno ‘FINALLY’, likithibitisha kuwa Fury na Joshua watakutana Desemba 11 katika Principality Stadium, Cardiff, huku Netflix ikiwa msambazaji wa pambano hilo.

Fury anaingia kwenye pambano hilo akiwa na imani kubwa kwamba anaweza kumwangusha Joshua mapema, hasa baada ya kushuhudia namna Joshua alivyoanza kwa nguvu katika ushindi wake wa Julai dhidi ya Kristian Prenga.

PAMB 05

Kwa upande mwingine, Joshua alikuwepo ulingoni wakati Fury aliposhinda kwa pointi dhidi ya Arslanbek Makhmudov mwezi Aprili, pambano ambalo lilimpa nafasi ya kuona mapungufu kadhaa ya mpinzani wake.

Historia ya uhasama wao ilianza miaka 16 iliyopita, wakati wawili hao walipokutana kwa mara ya kwanza katika mazoezi kwenye ukumbi wa Finchley ABC, wakati huo wakiwa bado hawajafikia umaarufu waliokuwa nao baadaye.

Fury, ambaye wakati huo alikuwa akizunguka nchini Uingereza akiwapa nafasi mabondia mbalimbali kujaribu kumwangusha kwa dau la Rolex, alikaribia kuangushwa na Joshua kwa pigo kali la ‘uppercut’ ambalo limeendelea kuwa sehemu ya historia ya uhusiano wao.

PAMB 01

Mara kadhaa wawili hao walikaribia kukutana ulingoni, lakini masuala ya fedha, maslahi binafsi na siasa za ndondi yaliendelea kuzuia pambano hilo kufanyika.

Sasa, wakiwa wamevuka kilele cha ubora wao, Fury na Joshua watapata nafasi ya kuamua nani ataondoka na ushindi dhidi ya mpinzani wao mkubwa wa kizazi hiki.

Wote wamewahi kutawala jukwaa la ndondi duniani, pia wote wameangushwa na Oleksandr Usyk, ambaye amewashinda kila mmoja mara mbili.

Joshua pia amewahi kupoteza kwa mtoano dhidi ya Andy Ruiz Jr na Daniel Dubois, huku Fury naye akikabiliwa na changamoto kubwa katika miaka ya karibuni.

Hata hivyo, Desemba 11 Cardiff itakuwa jukwaa la wawili hao kuandika sura mpya katika historia yao katika pambano ambalo mashabiki wa ndondi wamekuwa wakilisubiri kwa muda mrefu.