Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Haaland ajitenga na hukumu Man City

Muktasari:

  • Man City ilipatikana na hatia ya makosa mengi kati ya mashtaka yaliyowasilishwa dhidi yake na Ligi Kuu England kuhusu ukiukaji wa kanuni za kifedha, baada ya hukumu kutolewa Septemba, mwaka huu. Tangu wakati huo, klabu hiyo imekata rufaa dhidi ya uamuzi huo.

MANCHESTER, England: ERLING Haaland amezungumzia zaidi ya dakika mbili akitaja timu alizowahi kuzichezea katika miaka iliyohusishwa na uchunguzi wa Ligi Kuu England dhidi ya Man City, huku nyota huyo akihoji alitarajiwa kujibuje kuhusu hukumu iliyotolewa dhidi ya klabu hiyo.

Man City ilipatikana na hatia ya makosa mengi kati ya mashtaka yaliyowasilishwa dhidi yake na Ligi Kuu England kuhusu ukiukaji wa kanuni za kifedha, baada ya hukumu kutolewa Septemba, mwaka huu. Tangu wakati huo, klabu hiyo imekata rufaa dhidi ya uamuzi huo.

Tume huru iliamua kuwa Man City ilificha malipo yenye thamani ya Pauni 900 milioni ndani ya kipindi cha miaka tisa kwa kutumia mikataba ya kughushi. Man City ilibainika kuongeza kwa njia isiyo halali thamani ya mikataba ya udhamini na kuingiza fedha kwenye klabu hiyo kutoka kwa wamiliki wake wa Abu Dhabi kupitia malipo yaliyofichwa, ikiwa na lengo la kukwepa kanuni za matumizi ya fedha za Ligi Kuu England.

Haaland aliulizwa kuhusu hali ya klabu hiyo na kituo cha televisheni cha Norway, TV2, baada ya kufunga bao katika ushindi wa mabao 3-1 wa timu yake ya taifa dhidi ya Wales Jumamosi.

Jibu la awali la nyota huyo wa Man City lilidumu kwa dakika mbili na sekunde 14, huku akitaja timu alizowahi kuzichezea kuanzia 2009 hadi 2018, kipindi kinachohusishwa na mashtaka hayo.

“Mwaka 2009 nilikuwa na timu ya Bryne U9. Mwaka 2010 nilikuwa U10. Mwaka 2011 nilikuwa U11. Mwaka 2012, U12 na mwaka 2013, U13. Tuendelee? Hatuhitaji kutaja orodha nzima. Mwaka 2014 nilikuwa U14. Mwaka 2015 nilikuwa U15 na timu ya taifa,” Haaland alianza kueleza.

“Baadaye nilikuwa U16, kama sikosei. Mwaka 2016 nilipandishwa kwenye kikosi cha kwanza cha Bryne, timu ya pili na timu ya vijana. Mwaka 2017 nilihamia Molde. Mwaka 2018 nilikuwa Molde. Nilichezea kikosi cha kwanza Molde 2 na kwa kiasi fulani timu ya vijana.

“Kwa hiyo, hili (Man City) ni swali ambalo ninapata ugumu kulijibu kwa sababu ni suala la kisheria.”

“Ni kesi kati ya Ligi Kuu England na Manchester City ambayo itashughulikiwa na jopo maalumu. Je natarajiwa kulijibu? Sina uhakika kabisa.”

Haaland aliendelea kwa kutaja wachezaji wenzake kutoka Norway waliokuwa Man City katika kipindi hicho, huku akitania kwamba huenda wao wakawa katika nafasi nzuri zaidi ya kutoa ufafanuzi kuhusu suala hilo.