Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

JKT Queens yatuma ujumbe Simba, Mashujaa

JKT Pict

Muktasari:

  • Kondo amesema ushindani wa msimu huu ni mkubwa, huku akizitaja Simba Queens na Mashujaa Queens kuwa miongoni mwa wapinzani wanaopaswa kupewa uzito katika mbio za ubingwa.

KOCHA msaidizi wa JKT Queens, Azishi Kondo amesema ushindi dhidi ya Yanga Princess umeongeza hamasa kwa kikosi hicho katika mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake, lakini akasisitiza kuwa bado kina kazi ya kufanya katika mechi zinazofuata.

Kondo amesema ushindani wa msimu huu ni mkubwa, huku akizitaja Simba Queens na Mashujaa Queens kuwa miongoni mwa wapinzani wanaopaswa kupewa uzito katika mbio za ubingwa.

"Naamini kila aliyepo kwenye ligi anapambana ili kuwania ubingwa. Tumeshacheza na Yanga, ambayo ni miongoni mwa timu zinazoleta ushindani kwenye harakati hizo. Bado tuna Simba na Mashujaa Queens ambao nao wameonyesha ushindani mkubwa," amesema Kondo.

JK 02

Ameongeza kuwa baada ya kumaliza mchezo dhidi ya Yanga, sasa wanapaswa kuelekeza nguvu katika mechi zinazofuata na kujiandaa kulingana na mahitaji ya kila mpinzani.

"Kwa hiyo, tumemaliza na Yanga, tutaangalia mechi zijazo tunakwendaje ili kuhakikisha tunashinda mechi mfululizo. Kila mechi inakuja na mbinu yake, hivyo tutakwenda kujipanga," amesema.

JK 01

JKT Queens imeanza vizuri msimu huu baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Geita Queens na Bunda Girls, kabla ya kuendeleza ubora wake kwa kuichapa Yanga Princess bao 1-0.