Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga princess yamrejesha Igwe

IGWE Pict

Muktasari:

  • Kurejea kwa Igwe ni nyongeza muhimu katika safu ya ulinzi ya Yanga Princess, hasa ikizingatiwa mchango wake msimu uliopita. Beki huyo alicheza mechi 21 kati ya 22 za timu hiyo na kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa msimu iliyotolewa na klabu.

YANGA Princess imemrejesha aliyekuwa beki wake wa kati, Igwe Uzoamaka, ambaye mwishoni mwa msimu uliopita aliaga kupitia mitandao ya kijamii baada ya mkataba wake kumalizika.

Beki huyo raia wa Nigeria aliitumikia Yanga msimu uliopita, lakini msimu huu hakuonekana kikosini katika mechi tatu za mwanzo. Badala yake, alionekana jukwaani wakati Yanga ilipokutana na JKT, mechi ambayo Wananchi walipoteza kwa bao 1-0.

Baada ya kumuona akiwa jukwaani, Mwanaspoti ilimuuliza kocha wa timu hiyo, Said Maulid, ambaye alithibitisha kuwa beki huyo amerejea, ingawa hakueleza sababu za kurejea kwake.

IGW 02

"Ni kweli amerejea, hakuwa na majeraha na tutakuwa naye," amesema kocha huyo.

Hata hivyo, Mwanaspoti inafahamu kuwa baada ya mkataba wake kumalizika, Igwe hakuongezewa mkataba mwingine, hali iliyomfanya kuondoka kikosini.

Baada ya mashabiki kuibua malalamiko wakitaka kufahamu sababu za klabu kuachana naye, licha ya kuwa mhimili muhimu wa timu, Yanga ilimfuata na hatimaye kumuongezea mkataba wa msimu mmoja.

IGW 01

Kurejea kwa Igwe ni nyongeza muhimu katika safu ya ulinzi ya Yanga Princess, hasa ikizingatiwa mchango wake msimu uliopita. Beki huyo alicheza mechi 21 kati ya 22 za timu hiyo na kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa msimu iliyotolewa na klabu.

Igwe si mchezaji pekee aliyerejeshwa baada ya mashabiki kutoa maoni yao. Kiungo Agnes Pallangyo, ambaye pia hakuongezewa mkataba, alirejeshwa na sasa ameendelea na majukumu yake ndani ya kikosi hicho.