Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gusa vyuma hivi upigwe pesa ndefu

Muktasari:


  • Kati ya Bukayo Saka na Lamine Yamal, Kylian Mbappe na Erling Haaland, wapi utakubali kuvunja benki ili kunasa huduma yake?

LONDON, ENGLAND: NANI utakubali kutoa mkwanja mrefu kunasa saini yake?

Kati ya Bukayo Saka na Lamine Yamal, Kylian Mbappe na Erling Haaland, wapi utakubali kuvunja benki ili kunasa huduma yake?

Swali gumu, lakini ukweli uliopo mezani kwenye orodha ya mastaa hao wanne, wote hakuna hata mmoja unaweza kumnasa kwa pesa ndogo, wote thamani zao zipo juu sokoni. Kwa mujibu wa Transfermarkt, yamewekwa ubaoni majina ya mastaa 20 wanaotamba kwenye soka kwa sasa, ambao thamani zao ziko juu sokoni. Na kwenye orodha hiyo ya mastaa 20, kuna wachezaji tisa tu wa kutokea Ligi Kuu England, ambako wanacheza wakali, Saka na Haaland.

Lakini, kingine unachoweza kushangaa ni kuona orodha hiyo kuna staa mmoja tu kutoka kikosi cha Paris Saint-Germain, ambao ni mabingwa wa Ulaya.

Wachezaji hao thamani hizo zimekuwa kubwa zaidi dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi ukilinganisha na dirisha la majira ya kiangazi la mwaka jana.

Kwa maana hiyo, kwa timu yoyote itakayohitaji saini ya wakali hawa, italazimika kutoa mkwanja mrefu kuwanasa. Hata hivyo, bei inayotajwa kwenye thamani ya Transfermarkt sio halisi ya mchezaji anayeweza kuuzwa na klabu yake, kwamba bei yake inaweza kuwa chini au zaidi ya hapo.

Kwa mfano, straika wa Newcastle United, Alexander Isak klabu yake inamthaminisha kuwa na thamani ya Pauni 150 milioni, lakini huko kwenye Transfermarkt, imemworodhesha kuwa na thamani ya Pauni 104.7 milioni.


Hii hapa orodha ya wanasoka 20 ambao thamani zao zipo juu sana huko sokoni, ukihitaji saini zao, utalazimika kuvunja benki.


20) Desire Doue (PSG) – Pauni 78.5 milioni

19) Lautaro Martinez (Inter) – Pauni 82.9 milioni

18) Phil Foden (Man City) – Pauni 87.2 milioni

17) Alexis Mac Allister (Liverpool) – Pauni 87.2 milioni

16) Michael Olise (Bayern Munich) – Pauni 87.2 milioni

15) Julian Alvarez (Atletico Madrid) – Pauni 87.2 milioni

14) Rodri (Man City) – Pauni 96 milioni

13) Federico Valverde (Real Madrid) – Pauni 101.2 milioni

12) Alexander Isak (Newcastle) – Pauni 104.7 milioni

11) Cole Palmer (Chelsea) – Pauni 104.7 milioni

10) Declan Rice (Arsenal) – Pauni 104.7 milioni

9) Pedri (Barcelona) – Pauni 122.2 milioni

8) Jamal Musiala (Bayern Munich) – Pauni 122.2 milioni

7) Florian Wirtz (Liverpool) – Pauni 122.2 milioni

6) Bukayo Saka (Arsenal) – Pauni 130.9 milioni

5) Vinicius Junior (Real Madrid) – Pauni 148.4 milioni

4) Kylian Mbappe (Real Madrid) – Pauni 151.8 milioni

3) Erling Haaland (Man City) – Pauni 151.8 milioni

2) Jude Bellingham (Real Madrid) – Pauni 151.8 milioni

1) Lamine Yamal (Barcelona) – Pauni 174.6 milioni