Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Griezmann atwaa tuzo MLS

GRIZMAN Pict

Muktasari:

  • Mshambuliaji huyo alikuwa na mchango mkubwa katika ushindi wa mabao 4-1 wa Orlando City, akifunga mabao mawili na kutoa asisti moja kwenye Uwanja wa Inter&Co.

ORLANDO, MAREKANI: NYOTA wa kimataifa wa Ufaransa na DC United, Antoine Griezmann anaendelea kung'ara katika soka la Marekani baada ya kutangazwa kuwa Mchezaji Bora wa Siku ya Mechi ya 31 ya Ligi Kuu ya Soka Marekani (MLS) msimu huu kufuatia kiwango kingine bora alichoonyesha dhidi ya DC United.

Mshambuliaji huyo alikuwa na mchango mkubwa katika ushindi wa mabao 4-1 wa Orlando City, akifunga mabao mawili na kutoa asisti moja kwenye Uwanja wa Inter&Co.

Katika mchezo huo uchezaji wake ulikuwa uthibitisho mwingine wa athari kubwa aliyoipeleka kikosini kwake tangu alipojiunga na MLS katika dirisha kubwa la usajili msimu huu, ambapo nyota huyo aliyewahi kutwaa Kombe la Dunia akiwa na Ufaransa 2018 amefunga mabao 12 na kutoa asisti saba katika mechi 14 alizocheza. Pia, amechangia angalau bao moja, kwa kufunga au kutoa pasi ya mwisho, katika mechi 12 kati ya hizo.

GRIZ 01

Akiwa na jumla ya michango 19 iliyozalisha mabao, Griezmann amelingana na mchezaji mwenye idadi ya pili kwa wingi wa michango hiyo miongoni mwa wachezaji waliojiunga na ligi hiyo msimu huu. Nyota pekee aliye mbele yake ni Guilherme wa Houston Dynamo aliyehusika na mabao 26.

GRIZ 02

Hii ni mara ya pili kwa Griezmann kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Siku ya Mechi ya MLS msimu huu, kwani awali alishinda katika Siku ya Mechi ya 22. Pia amekuwa mchezaji wa kwanza kutoka Ufaransa kushinda tuzo hiyo mara mbili ndani ya msimu mmoja wa MLS tangu Thierry Henry alipoinyakua mara tano akiwa na New York Red Bulls 2012.