Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kamungo atimka kambini Taifa Stars

KAMUNGO Pict

Muktasari:

  • Nyota huyo mzaliwa wa DR Congo aliyekulia katika kambi ya wakimbizi Nyarugusu, Tanzania, maisha yake ya soka amekulia Marekani akitumikia klabu ya North Texas (2021-2022) ya Ligi Daraja la Tatu ambako kwenye mechi 52 alifunga mabao 22.

MSHAMBULIAJI wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Bernard Kamungo, tayari ametatua changamoto aliyokumbana nayo na tayari ameondoka kambini na kurejea Marekani kujiunga na FC Dallas, huku akitarajiwa kuungana tena kwenye majukumu ya kitaifa hadi Novemba 2026.

Chanzo cha ndani kutoka kambi ya Stars iliyopo Morocco kililiambia Mwanaspoti, mchezaji huyo tayari amekamilisha taratibu zote za kupata hati yake ya kusafiria ya Tanzania kabla ya kuondoka.

Hatua hiyo inamfanya Kamungo kukosa mechi za kirafiki zinazoendelea hivi sasa zikiwa chini ya kalenda ya FIFA, kutokana na kuhitajika kwa haraka na klabu yake.

Mtoa taarifa huyo wa ndani alieleza FC Dallas inamhitaji Kamungo kwa haraka kwa ajili ya mechi muhimu za Ligi Kuu Marekani (MLS) zinazoendelea hivi sasa.

KAMU 01

"Ni kweli Kamungo amepata passport yake na tayari ameondoka kambini kuelekea Marekani. FC Dallas wamemhitaji kwa haraka sana kwa ajili ya mechi zao za ligi kuu," kilieleza chanzo hicho.

Chanzo hicho kilieleza kuwa, nyota huyo atarejea tena Novemba mwaka huu na timu hiyo itakuwa ikikabiliwa na mechi za kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).

"Kutokana na ratiba hiyo ya klabu yake, Bernard Kamungo atarejea tena kikosini hadi Novemba kwenye mechi za kufuzu AFCON. Kwa sasa kwenye mechi hizi za kirafiki hatokuwepo kwa sababu anawahi ratiba ya klabu," kiliongeza chanzo hicho.

Kuondoka kwa mshambuliaji huyo kumekuja kutokana na kuwepo kwa sitofahamu ya siku chache zilizopita kuhusu nyaraka zake za usafiri na uraia baada ya kuwasili nchini kwa mara ya kwanza kujiunga na kikosi hicho.

KAMU 02

Nyota huyo alijumuishwa kwenye kikosi cha Taifa Stars chini ya Kocha Miguel Gamondi kwa ajili ya mechi mbili za kuwania kufuzu Afcon 2027 dhidi ya Guinea Bissau na Madagascar ingawa hakucheza mechi zote mbili kutokana na changamoto hiyo.

Nyota huyo mzaliwa wa DR Congo aliyekulia katika kambi ya wakimbizi Nyarugusu, Tanzania, maisha yake ya soka amekulia Marekani akitumikia klabu ya North Texas (2021-2022) ya Ligi Daraja la Tatu ambako kwenye mechi 52 alifunga mabao 22.