Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wafalme wa mabao Ligi ya Mabingwa Ulaya

WAFALME Pict

Muktasari:

  • Hata hivyo, wakati mechi hizo zikianza kupigwa kumbuka kwamba kuna miamba imefanya mambo mazito ikitupia nyavuni mara kibao kuliko wachezaji wengi walioshiriki na wanaocheza mashindano hayo kwa sasa. Kumbuka, ndani ya orodha hii namba moja na mbili ni Cristiano Ronaldo na Lionel Messi mtawalia waliofunga zaidi ya mabao 250 kwa pamoja.

ZURICH, USWISI: WIKI hii zilipigwa mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya, ambapo vigogo wa bara hilo walianza kuusaka ufalme ili kuipokonya taji PSG  ambayo imelibeba mara mbili mfululizo katika misimu miwili iliyopita.

Hata hivyo, wakati mechi hizo zikianza kupigwa kumbuka kwamba kuna miamba imefanya mambo mazito ikitupia nyavuni mara kibao kuliko wachezaji wengi walioshiriki na wanaocheza mashindano hayo kwa sasa. Kumbuka, ndani ya orodha hii namba moja na mbili ni Cristiano Ronaldo na Lionel Messi mtawalia waliofunga zaidi ya mabao 250 kwa pamoja.

Lakini, vivyo vivyo elewa kwamba mabao yote hayajumuishi mechi za kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya na pia mastaa 12 waliofunga mabao 50 au zaidi ni watatu tu ambao bado wanakipiga katika Bara la Ulaya kwa sasa; Erling Haaland anayeichezea Manchester City, Harry Kane straika wa Bayern Munich na Mohamed Salah aliyehamia Trabzonspor ya Uturuki.


WAFALM 01

CRISTIANO RONADO (140)

Cristiano Ronaldo ndiye mfungaji bora wa muda wote katika Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na mabao 140 katika mechi 183 alizocheza.

Kwa sasa Mreno huyo anacheza katika Klabu ya Al Nassr ya Saudi Arabia, hivyo kuna uwezekano mdogo wa kuongeza idadi hiyo, ambayo aliifikia katika vipindi tofauti akiwa Manchester United (21), Real Madrid (105) na Juventus (14).

Ronaldo pia anashikilia rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi katika msimu mmoja wa Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kufunga mara 17 akiwa Real Madrid 2013-14 wakati walipotwaa taji kwa kuifunga Atletico Madrid katika fainali. Miaka miwili baadaye, msimu wa 2015-16 alifunga mabao 16.

Mshambuliaji huyo maarufu ameshinda tuzo ya mfungaji bora wa mashindano hayo mara saba ikiwa ni rekodi katika vipindi vyote vya Klabu Bingwa na Ligi ya Mabingwa Ulaya. Alifunga katika mechi 93 tofauti za Ligi ya Mabingwa ambazo ni asilimia 51 ya mechi alizoicheza, huku katika mechi nane kati ya hizo akifunga hat-trick, rekodi ambayo anaishirikiana na Lionel Messi.

Ronaldo alifunga dhidi ya wapinzani 38 tofauti katika maisha yake ya michuano hiyo, huku mabao 10 dhidi ya Juventus yakiwa ndiyo mengi zaidi yaliyowahi kufungwa na mchezaji mmoja dhidi ya mpinzani mmoja katika historia ya mash indano hayo.


WAFALM 02

LIONEL MESSI (129)

Lionel Messi ni mfungaji wa pili kwa mabao mengi katika historia ya mashindano hayo akitupia mara 129. Hata hivyo, anashikilia rekodi ya mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi akiwa na klabu moja katika historia ya Ligi ya Mabingwa baada ya mabao 120 kati ya 129 aliyofunga akiwa Barcelona.

Aliongeza mabao mengine tisa baada ya kuhamia PSG katika Ligi Kuu Ufaransa (Ligue 1) 2021, lakini kuna uwezekano mdogo wa kupata nafasi ya kuongeza idadi hiyo baada ya kuhamia Inter Miami ya Ligi Kuu Marekani (MLS).

Messi anashikilia rekodi ya kufunga dhidi ya wapinzani 40 tofauti katika mashindano hayo, zaidi ya mchezaji mwingine yeyote akimzidi Ronaldo mwenye 38. Mabao tisa ya Messi alifunga dhidi ya Arsenal (asilimia saba), ikiwa ndiyo timu aliyoifunga mabao mengi zaidi katika Ligi ya Mabingwa.

Kwa ujumla, Messi, aliyeshinda Kombe la Dunia 2022 amefunga katika misimu 18 tofauti ya Ligi ya Mabingwa, akifunga katika kila msimu tangu 2005-06 baada ya kushindwa kufunga katika mechi moja pekee kwa Barcelona katika msimu wake wa kwanza wa 2004-05. Anashirikiana rekodi hiyo na Karim Benzema, lakini mshambuliaji huyo Mfaransa alifunga katika misimu yote 18 ya Ligi ya Mabinwa aliyocheza.

Messi anashirikiana na Cristiano Ronaldo rekodi ya kufunga hat-trick nyingi zaidi katika mashi ndano hayo (nane), lakini aliwahi kufanya jambo ambalo Mreno huyo hakuwahi kulifanya; kufunga mabao matano katika mechi moja. Alifanya hivyo wakati Barcelona i li po ifunga Bayer Leverkusen 7-1 Machi 2012, ikiwa ni sehemu ya msimu wake wa kuvunja rekodi wa 2011-12, ambapo alifunga mabao 73 katika mechi 60 za mashindano akiwa na klabu.


WAFALM 03

ROBERT LEWANDOWSKI (109)

Robert Lewandowski alifikisha mabao 100 Ligi ya Mabingwa, Novemba 26, 2025 baada ya kufunga bao akiwa Barcelona dhidi ya Brest ya Ufaransa. Kati ya mabao yake 109 ya mashindano hayo, 69 alifunga akiwa Bayern Munich baada ya kujiunga akitokea Borussia Dortmund.

Akiwa na mabao 23 kwa Barcelona, alikuwa mchezaji wa pili katika historia ya Ligi ya Mabingwa kufunga mabao 10 au zaidi kwa klabu tatu tofauti baada ya Cristiano Ronaldo.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Poland anashikilia rekodi ya Bayern ya kufunga mabao mengi zaidi katika mashindano ya Ulaya, akiwa mbele ya Gerd Muller (65).

Pia anashikilia rekodi ya klabu hiyo kufunga mabao mengi zaidi katika msimu mmoja wa mashindano hayo baada ya kufunga mara 15 msimu wa 2019-20 wakati Bayern ilipotwaa taji.

Kwa kufanya hivyo, alikuwa mchezaji wa kwanza wa Poland kumaliza akiwa mfungaji bora katika msimu wa Ligi ya Mabingwa na mashindano ya klabu Ulaya.

Hata hivyo, mabao yake ya 108 na 109 aliyafunga dhidi ya Newcastle United katika hatua ya 16 bora ya ligi hiyo msimu wa 2025-26, jambo lililomfanya avunje rekodi ya kufunga dhidi ya wapinzani wengi tofauti katika mashindano hayo (41).


WAFALM 04

KARIM BENZEMA (90)

Baada ya kuhamia Al-Ittihad ya Saudi Arabia Juni 2023, Karim Benzema alionekana kuwa na uwezekano mdogo sana wa kuongeza mabao yake 90 ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, inagwa kwa sasa ameshaachana na timu hiyo akisa malisho mapya kwa kuwa bado ni mchezaji huru.

Benzema amefunga katika misimu mingi zaidi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya bila kushindwa kufunga katika msimu wowote, baada ya kutupia katika misimu yote 18 ya mashindano hayo tangu alipoanza kucheza msimu wa 2005-06 akiwa Lyon ya Ufaransa.

Mshambuliaji huyo kimataifa wa Mfaransa alishinda kwa mara ya kwanza tuzo ya mfungaji bora wa Ligi ya Mabingwa Ulaya 2021-22, baada ya mabao yake 15 kuisaidia Real Madrid kutwaa taji, ingawa hakufunga katika ushindi wa fainali dhidi ya Liverpool jijini Paris. Mabao yake 78 aliyofunga kwa Real Madrid katika mashindano hayo yanazidiwa na Cristiano Ronaldo pekee ambaye alifunga 105.


WAFALM 05

RAUL GONZALEZ (71)

Raul, aliyewahi kuwa mchezaji wa kimataifa wa Hispania, ni mfungaji wa tatu kwa mabao mengi zaidi wa Real Madrid katika historia ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (66), huku jumla yake ya mabao 71 ikiwa ya tano kwa wachezaji wote katika mashindano hayo.

Raul alikuwa mfungaji bora wa mashindano hayo hadi Novemba 2014 alipokuja kuzidiwa na Messi na Ronaldo. Nyota huyo wa Real Madrid pia alikuwa mchezaji wa kwanza kufikisha mabao 50 ya mashindano hayo, akifanya hivyo Septemba 2005.

Pia alikuwa mchezaji wa kwanza wa Real Madrid kufikisha mabao 50 katika  mashindano ya Ulaya baada ya Alfredo Di Stefano, ambaye awali alikuwa amefunga mabao 49 katika mashindano ya Ulaya akiwa na timu hiyo.

Msimu wake wa mwisho katika mashi ndano hayo ulikuwa 2010-11 akiwa na Schalke 04, ambapo alifunga mara tano akiwa na umri wa miaka 33 yaliyomfanya kufikisha jumla ya mabao 71.


WAFALM 06

KYLIAN MBAPPE (71)

Kylian Mbappe alifikisha mabao 50 ya Ligi ya Mabingwa Ulaya katika mchezo wa Real Madrid dhidi ya Atalanta Desemba 10, 2024.

Akiwa na umri wa miaka 25 na siku 356 alipofikisha idadi hiyo, alikuwa mchezaji wa pili mwenye umri mdogo zaidi kufunga mara 50 baada ya  Messi ambaye alikuwa na miaka 24 na siku 284 alipokuwa Barcelona, Aprili 2012 dhidi ya AC Milan.

Kwa kufikisha mabao 50 ndani ya mechi 79, Mbappe pia alikuwa mchezaji wa nne aliyefikisha mabao hayo kwa haraka zaidi katika ligi hiyo akitanguliwa na Ruud van Nistelrooy (mechi 62), Lionel Messi (66) na Robert Lewandowski (77), ingawa Harry Kane naye sasa amempita katika rekodi hiyo.

Mbappe alifunga mabao 15 katika msimu wa Ligi ya Mabingwa 2025-26. Ni Cristiano Ronaldo pekee aliyewahi kufunga mabao mengi zaidi katika msimu mmoja wa ligi hiyo.


WACHEZAJI WENYE MABAO 50+


WAFALM 07

ERLING HAALAND (59)

Erling Haaland aliweka historia Septemba 2025 alipofunga bao lake la 50 katika Ligi ya Mabingwa Ulaya akifikisha idadi hiyo kwa haraka zaidi kuliko mchezaji mwingine yeyote katika mashindano hayo.

Mabao aliyofunga akiwa RB Salzburg, Borussia Dortmund na Manchester City katika mashindano hayo yalimwezesha kufikisha 50 katika mechi 49 pekee, na kuvunja rekodi ya awali iliyokuwa inashikiliwa na Van Nistelrooy ya mechi 62.

Haaland alifunga mabao mawili zaidi katika Mechi ya pili ya msimu wa 2025-26 dhidi ya Monaco, hivyo mabao yake 52 yakawa mengi zaidi yaliyofungwa na mchezaji katika mechi zake 50 za kwanza kwenye mashindano hayo akivunja rekodi ya awali ya Van Nistelrooy ya mabao 43 katika mechi 50 za kwanza.

Kisha, Haaland alifunga mabao mawili katika siku ya kwanza ya mechi za msimu wa 2026-27 na kumpita Thomas Muller kufikisha mabao 59 katika idadi hiyo hiyo ya mechi.


WAFALM 08

THOMAS MULLER (57)

Tangu Thomas Muller alipoanza kucheza mashindano hayo msimu wa 2008-09, amefunga mabao 57 na kutoa pasi 25 za mabao, ambapo nyota huyo wa zamani wa kimataifa wa Ujerumani anayekipiga kwa sasa Vancouver Whitecaps ya Canada, ameshinda Ligi ya Mabingwa Ulaya  mara mbili akiwa na Bayern Munich katika misimu ya 2012-13 na 2019-20.


WAFALM 09

RUUD VAN NISTELROOY (56)

Mshambuliaji wa kimataifa wa Uholanzi, Ruud van Nistelrooy, alifunga mabao 56 kwa ujumla katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini idadi hiyo huenda ingekuwa kubwa zaidi kama angecheza mechi nyingi za michuano hiyo mapema katika maisha yake ya soka. 

Van Nistelrooy alicheza mechi 11 pekee akiwa PSV kabla ya kutimiza miaka 25 na kucheza mechi yake ya kwanza ya mashindano hayo akiwa Manchester United.

Awali, hakukuwa na mchezaji aliyefikisha mabao 50 Ligi ya Mabingwa Ulaya haraka zaidi ya Van Nistelrooy aliyefikisha idadi hiyo katika mechi 62, lakini alikuwa na umri wa miaka 31 rekodi iliyokuja kuvunjwa na Haaland.

Van Nistelrooy alifunga mabao 35 katika ligi hiyo akiwa Manchester United ikiwa ni rekodi ya klabu hiyo mbele ya Wayne Rooney (30) na Ryan Giggs (28).


WAFALM 10

HARRY KANE (54)

Harry Kane alifunga mabao ya 49 na 50 ya Ligi ya Mabingwa Ulaya katika ushindi wa nyumbani wa Bayern Munich dhidi ya Atalanta, Machi 2026.

Kane alifikisha idadi hiyo katika mechi 66 za mashindano hayo. Ni wachezaji wawili pekee waliowahi kufikisha mabao 50 katika mechi chache zaidi; Erling Haaland (49) na Ruud van Nistelrooy (62), huku Kane akifikisha idadi hiyo katika mechi 66, sawa na Lionel Messi.


WAFALM 11

THIERRY HENRY (50)

Thierry Henry alifunga mabao 50 Ligi ya Mabingwa akiwa na klabu tatu tofauti; Arsenal (35), Barcelona (nane) na Monaco (saba).

Alianza maisha katika ligi hiyo akifunga mara sita katika mechi tano za kwanza Monaco akiwa na umri wa miaka 20 kabla ya kuhamia Arsenal 1999-2000. Mabao yake 35 akiwa na Arsenal yanamfanya kuwa mchezaji wao aliyefunga mabao mengi zaidi katika historia ya Ligi ya Mabingwa na Klabu Bingwa Ulaya.


WAFALM 12

MOHAMED SALAH (50)

Mohamed Salah alifunga bao lake la 50 katika Ligi ya Mabingwa Ulaya katika ushindi wa Liverpool dhidi ya Galatasaray Machi 2026. Kwa bao hilo, alikuwa mchezaji wa kwanza kutoka Afrika kufikisha idadi ya mabao 50 katika mashindano hayo.