Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gary Neville aipa Arsenal ubingwa EPL

GARY Pict

Muktasari:

  • Arsenal sasa wapo katika nafasi nzuri kabisa ya kubeba taji lao la kwanza la Ligi Kuu England kwa zaidi ya miaka 20 huku wakisubiri matokeo ya Manchester City ambao jana usiku walikuwa na kibarua dhidi ya Bournemouth ili kuendelea kubaki kwenye mbio za ubingwa.

LONDON, ENGLAND: NYOTA wa zamani wa Manchester United, Gary Neville amesema haoni jinsi Arsenal watakavyopoteza nafasi yao ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu, baada ya kuichapa Burnley bao 1-0.

Arsenal sasa wapo katika nafasi nzuri kabisa ya kubeba taji lao la kwanza la Ligi Kuu England kwa zaidi ya miaka 20 huku wakisubiri matokeo ya Manchester City ambao jana usiku walikuwa na kibarua dhidi ya Bournemouth ili kuendelea kubaki kwenye mbio za ubingwa.

Neville amesema Arsenal wamefika kwenye hatua muhimu baada ya miaka kadhaa ya kujenga kikosi chao na sasa wako kwenye nafasi ambayo hawawezi kuiacha ipite kirahisi.

Nyota huyo aliongeza kuwa Arsenal wamekuwa wakikaribia ubingwa mara kadhaa katika misimu ya hivi karibuni lakini wamekuwa wakipoteza nafasi hiyo mwishoni, jambo ambalo lingekuwa changamoto kubwa kama wangerudia tena kosa hilo.

“Wamekuwa wakipoteza nafasi hii mara mbili au tatu katika misimu minne iliyopita. Sasa wako kwenye wakati muhimu sana na kila kitu kiko mikononi mwao,” amesema Neville.

Aliendelea kusema iwapo Mikel Arteta ataiongoza Arsenal kutwaa ubingwa, itakuwa hatua kubwa sana katika historia ya klabu hiyo na maisha yake ya ukocha.

Neville pia alisifu uimara wa Arsenal msimu huu, hasa uwezo wao wa kulinda uongozi mdogo wa mabao kama ilivyokuwa katika mechezo uliopita wa ligi dhidi ya Burnley.