Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga kama Arsenal, ‘mchawi’ huyu hapa!

Muktasari:

  • Nikurudishe nyuma kidogo katika mechi ya tatu ya Ligi Kuu Bara kwa Yanga iliyowakutanisha na JKT Tanzania kwenye Uwanja wa KMC Complex uliopo Mwenge jijini Dar es Salaam, ambapo Wanajangwani hao waliwachakaza makamanda hao kwa kipigo cha mabao 4-0.

WAKATI mashabiki wa Yanga wakiendelea kufurahia mabao yanayofungwa na mastaa wa kikosi hicho, nyuma ya ushindi huo kuna mwamba mmoja ambaye haongei sana ila kazi zake zimeanza kupiga makelele. Unaweza kumuita ndiye mchawi wa mabao hayo.

Nikurudishe nyuma kidogo katika mechi ya tatu ya Ligi Kuu Bara kwa Yanga iliyowakutanisha na JKT Tanzania kwenye Uwanja wa KMC Complex uliopo Mwenge jijini Dar es Salaam, ambapo Wanajangwani hao waliwachakaza makamanda hao kwa kipigo cha mabao 4-0.

Mfunguzi wa kipigo hicho alikuwa Albert Kangwanda dakika ya 28, bao la pili lilifungwa na Ibrahim Bacca dakika ya 32 na kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika Chadrack Boka alitupia la tatu dakika 38. Waliporejea kutoka mapumziko, Peter Shalulile alitia kambani la nne dakika ya 63.

Mabao yote hayo yalikuwa mazuri ila bao lililofungwa na Bacca dakika ya 34 lilitokana na mbinu kali ya mpira wa kutenga alilofunga kwa kichwa kupitia shambulizi la adhabu ndogo lililoanzishwa na Kangwanda, kisha mpira kwenda kwa Duke Abuya, Mkenya huyo akamuwekea Housseine Zakouani na kupiga krosi iliyomfikia mfungaji. Baada ya bao hilo, Bacca alikwenda kumkumbatia kocha Kagisho Dikgacoi.

Msimu uliopita katika mechi 30, Yanga ilitengeneza mabao mawili pekee kupitia mipira iliyokufa likiwemo lililofungwa na Lassine Kouma dakika ya 45 kwa kichwa dhidi ya Pamba Jiji akitumia kona ya Edmund John. Yanga ikishinda 3-0.

MWAMBA HUYU HAPA

Kagisho Dikgacoi (41) ndiye kocha mpya wa mipira ya kutenga (Set-Pieces Coach) wa Yanga. Alitambulishwa Julai 2026 kujiunga na benchi la ufundi la mabingwa hao chini ya Kocha Mkuu, Manqoba Mngqithi kwa ajili ya msimu wa 2026-2027.

Ujio wa Dikgacoi tayari umeshaanza kuleta matunda kwani kazi yake imeshatengeneza mabao manne kati ya 11 ambayo Yanga imeyafunga katika mechi tatu za Ligi Kuu Bara.

Kazi yake imetengeneza bao kwenye mechi dhidi ya Namungo ugenini wakati Yanga ikishinda 3-1, lile bao alilofunga beki Chadrack Boka lilitokana na kona fupi ya Albert Kangwanda aliyoanziana na Housseine Zakouani, krosi ikamkuta Mkongomani huyo na kuweka mpira wavuni dakika ya 68.

Kama haitoshi, kwenye mechi dhidi ya Coastal Union, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ naye akaweka wavuni bao la mwisho kwenye ushindi wa timu hiyo wa mabao 4-1, akianziana kona fupi na Boka.

Kabla ya bao hilo, beki na nahodha wa Yanga, Bakari Mwamnyeto alikaribia kufunga kwa shambulizi la kona ikipigwa na Kangwanda lakini mpira ukatoka nje kidogo. Mabao mengine mawili ya mipira ya kutengwa yamepatikana dhidi ya JKT Tanzania, akianza kufunga Bacca, kisha Boka, huku aliyeanzisha shambulizi akiwa Kangwanda.

Dikgacoi ana sifa ya kuwa na uelewa mkubwa wa mbinu na uongozi uwanjani. Ana umiliki wa Leseni ya Ukocha ya CAF A ambayo inamruhusu kufundisha soka la ngazi ya juu Afrika.

Ana rekodi ya kufundisha timu nne ndani ya ligi ya Afrika Kusini ambako aliinoa Royal Eagles, Witbank Spurs ambayo alipewa ikiwa kwenye hali mbaya na aliinusuru kushuka daraja na baadaye alitua Phezulu FC na Lamontville Golden Arrows ambako alihudumu kama kocha msaidizi chini ya Manqoba.

Aliwahi kuichezea Timu ya Taifa ya Afrika Kusini maarufu Bafana Bafana mechi 54 na kufunga mabao 2. Alicheza Kombe la Dunia 2010 na kushiriki AFCON mwaka 2008 na 2013. Ndiye aliyetoa pasi ya mwisho (asisti) kwa Siphiwe Tshabalala kufunga lile bao la kwanza la kihistoria la Kombe la Dunia 2010 dhidi ya Mexico.

Akizungumzia ufundi huo, staa wa zamani wa Yanga, Ally Mayay, alisema mabao hayo yanaonyesha mabadiliko yanayotokana na ufundi hasa kazi inayofanyika eneo la uwanja wa mazoezi.

Mayay alisema soka la kisasa linahitaji ufundi wa namna hiyo ambapo klabu nyingi zilizoendelea zimekuwa zikitengeneza mabao mengi kupitia mashambulizi ya aina hiyo.

“Hii maana yake kuna kazi kubwa ya kiufundi inafanyika kwenye uwanja wa mazoezi, haya ni mabadiliko chanya ambayo yanahitajika kwenye soka letu,” alisema Mayay ambaye alikuwa anacheza nafasi ya kiungo.

“Klabu nyingi ambazo zimeendelea huko Afrika Kaskazini, zimekuwa zikitengeneza mabao mengi kama haya kupitia mipira iliyokufa, huku kwetu tulikuwa bado hatujaona nafasi ya kutumia mashambulizi kama haya kwa wingi.

“Timu kubwa kama Yanga inapimwa kwa kutumia nafasi ambazo inazitengeneza, tumekuwa tukiona mechi zao inatengeneza nafasi nyingi lakini ilishindwa kutumia, msimu huu kuna mabadiliko makubwa yanayoonekana.

“Nadhani makocha hawa wapya kabla ya kuanza kazi waliifuatilia takwimu za Yanga na kuona wapi kunapotezwa nafasi nyingi na kipi wakiboreshe, wakaamua kuja kutengeneza mabao kupitia mashambulizi ya aina hiyo.”

KAMA ARSENAL

Msimu uliopita 2025-2026, ulimwengu wa soka ulishuhudia kitu kipya katika Ligi Kuu England baada ya Arsenal kuweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kufunga mabao 19 ndani ya msimu mmoja kupitia mipira ya kona.

Si kona pekee, Arsenal ilifanya vizuri kupitia mipira ya kutenga ambapo jumla ilimaliza msimu kwa kufunga mabao 25 yaliyochangia timu hiyo kushinda ubingwa wa Premier 2025-2026 baada ya miaka 22 kupita.

Mkali wa kazi hiyo ni Mjerumani, Nicolas Jover ambaye alitua klabuni hapo Julai 6, 2021 akitokea Manchester City, huku pia akiwahi kufanya kazi Brentford, Montpellier na timu ya taifa ya Croatia.