Arsenal yashinda yakaribia ubingwa EPL
Muktasari:
- Iwapo Washika Mitutu hao wa London watashinda mchezo wao wa mwisho dhidi ya Crystal Palace, Mei 24, 2026 watakuwa ndio mabingwa wapya wa Ligi Kuu England kwani watafikisha jumla ya pointi 85 ambazo hazitafikiwa na timu yoyote.
LONDON, ENGLAND: Bao pekee alilofunga na Kai Havertz limetosha kuipa pointi tatu muhimu Klabu ya Arsenal ambayo imebakiza mechi moja kumaliza msimu wa Ligi Kuu England wa 2025/2026.
Iwapo Washika Mitutu hao wa London watashinda mchezo wao wa mwisho dhidi ya Crystal Palace, Mei 24, 2026 watakuwa ndio mabingwa wapya wa Ligi Kuu England kwani watafikisha jumla ya pointi 85 ambazo hazitafikiwa na timu yoyote.
Hata hivyo, Arsenal inaweza kutwaa ubingwa huo endapo Man City itashindwa kuibuka na ushindi dhidi ya Bournemouth leo usiku Jumanne Mei 19, 2026.
Arsenal hadi sasa ndio vinara wa Ligi Kuu England wakiwa na pointi 82 wakifuatiwa na wapinzani wao wa karibu Man City wenye pointi 77 huku wakiwa na mchezo mmoja mkononi.
Hata hivyo, baada ya mchezo huo Arsenal ilifanya sherehe ya kufunga msimu kwa kuwa huu ulikuwa mchezo wao wa mwisho nyumbani.
"Bado tuna kazi ya kufanya kwenye mchezo wa mwisho tuendelee kuiunga mkono timu yetu," alisema kocha wa Arsenal, Mikel Arteta.