Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Garnacho apiga bao la Fifa

Muktasari:

  • Garnacho na Marcus Rashford hawakujumuishwa kabisa kwenye kikosi cha Man United kilichosafiri kuifuata Man City huko Etihad. Man United ilishinda mabao 2-1, shukrani kwa mabao ya kipindi cha pili ya Bruno Fernandes, aliyefunga kwa mkwaju wa penalti na Amad Diallo.

DOHA, QATAR: ALEJANDRO Garnacho ameshinda tuzo ya Fifa ya Bao Bora la Mwaka (Fifa Puskas) siku chache baada ya kupigwa chini kwenye kikosi cha Manchester United kilichocheza na Manchester City katika kipute cha Manchester derby kilichofanyika Etihad, Jumapili iliyopita.

Garnacho na Marcus Rashford hawakujumuishwa kabisa kwenye kikosi cha Man United kilichosafiri kuifuata Man City huko Etihad. Man United ilishinda mabao 2-1, shukrani kwa mabao ya kipindi cha pili ya Bruno Fernandes, aliyefunga kwa mkwaju wa penalti na Amad Diallo.

Na kocha wa Man United, Ruben Amorim alisema kukosekana kwa wachezaji hao kwenye kikosi ni ishu ya viwango tu vyao mazoezini kuwa duni.

Lakini, Garnacho alipata kitu cha kutabasamu baada ya kunyakua tuzo ya Puskas kufuatia bao lake la staili ya kibaiskeli alilowafunga Everton, Novemba 2023.

Hata hivyo, Muargentina huyo hakuwapo Qatar kuchukua tuzo yake katika usiku ambao ulimshuhudia Vinicius Jr akishinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Fifa. Staa huyo wa Real Madrid ameshinda tuzo hiyo ya mwaka akiwapiku Rodri na Jude Bellingham.

Mbrazili, Vini Jr ametamba kwenye tuzo hiyo ya Fifa baada ya kubwagwa kwenye Ballon d’Or na kiungo wa Man City, Rodri. Tuzo za Fifa zinatolewa kwa wachezaji walioonyeshwa viwango bora kati ya Agosti 2023 na Agosti 2024 - ambapo mshindi anapatikana kwa kura za mashabiki, mwandishi wa habari mmoja kwa kila nchi na manahodha na makocha wa timu za taifa. Kila kundi kura zao zinahesabika kama asilimia 25, huku kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti akinyakua tuzo ya kocha bora baada ya kushinda mataji makubwa ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na La Liga msimu uliopita.