Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fulham yaipiku Man United mikimbio

MIKIMBIO Pict

Muktasari:

  • Takwimu nyingine za mchezo huo zinaonyesha Fulham pia walifanya vizuri zaidi katika umbali wa kukimbia, huku wakifanya sprinti 10 zaidi ya Manchester United.

LONDON, ENGLAND: MANCHESTER United imekabiliwa na maswali kuhusu kiwango cha juhudi za wachezaji wake baada ya takwimu kuonyesha kuwa walikimbia jumla ya kilomita 6.5 chini ya Fulham katika sare ya mabao 1-1 ya Ligi Kuu England, Jumapili.

Kwa mujibu wa takwimu zilizokusanywa na FotMob, wachezaji wa Manchester United walikimbia jumla ya kilomita 110.2, huku Fulham wakifikisha kilomita 116.7 katika mchezo huo uliopigwa Craven Cottage.

Kocha wa United, Michael Carrick, hata hivyo, alisisitiza baada ya mchezo kwamba hakuona tatizo katika kiwango cha harakati na juhudi za kikosi chake.

Takwimu nyingine za mchezo huo zinaonyesha Fulham pia walifanya vizuri zaidi katika umbali wa kukimbia, huku wakifanya sprinti 10 zaidi ya Manchester United.

MIKI 01

United walionekana kuwa katika hatari ya kuondoka Craven Cottage mikono mitupu, kabla ya Matheus Cunha kuokoa timu hiyo kwa bao la dakika ya 89 lililomgonga mchezaji wa Fulham na kubadili mwelekeo.

Licha ya kusawazisha, sare hiyo imeacha maswali zaidi kwa Carrick, hasa baada ya United kushindwa kupata ushindi dhidi ya Fulham ambao bado hawajashinda mchezo wowote wa Ligi Kuu England msimu huu.


NEVILLE AWAKOSOA UNITED

Gwiji wa Manchester United na mchambuzi wa Sky Sports, Gary Neville, alikosoa vikali kiwango cha timu hiyo, akisema wachezaji walionekana kukosa juhudi za kutosha, hasa katika kipindi cha pili.

MIKI 02

Neville amesema kwa kawaida huwa mwangalifu kabla ya kuikosoa timu kwa kukosa juhudi, lakini alidai kuwa Manchester United haikufanya vya kutosha katika dakika za mwanzo za kipindi cha pili na kwa sehemu kubwa ya dakika 60 za kwanza.

Amesema pia timu hiyo ilikuwa katika kiwango duni sana inapokuwa haina mpira.

Kauli hizo zimeongeza mjadala kuhusu kiwango cha Manchester United chini ya Carrick, ambaye sasa atakuwa na muda wa kutafakari mambo wakati wa mapumziko ya kimataifa.