Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal, Chelsea ngoma kati EPL

Muktasari:

  • Gunners imepoteza mchezo mmoja pekee kati ya 29 iliyocheza kwenye mechi za London Derby katika ligi hiyo (ikishinda 22, sare sita) na haijafungwa katika 16 zilizopita (imeshinda 12, sare nne).

LONDON, ENGLAND, IMEKUWA mapema sana! Ndivyo unavyoweza kusema kuhusiana na mechi ya Ligi Kuu England wakati Arsenal watakapoikaribisha Chelsea katika Uwanja wa Emirates mjini London, leo saa 12:30 jioni, ambapo ubashiri wa kompyuta za mitandaoni unaipa Arsenal ushindi wa tatu mfululizo katika Ligi Kuu England kwa asilimia 57.4.

Gunners imepoteza mchezo mmoja pekee kati ya 29 iliyocheza kwenye mechi za London Derby katika ligi hiyo (ikishinda 22, sare sita) na haijafungwa katika 16 zilizopita (imeshinda 12, sare nne).

Chelsea kwa upande wake imepoteza mechi nne za mwisho za ligi ilipocheza ugenini dhidi ya Arsenal, ikifungwa jumla ya mabao 11-2.

Ingawa msimu bado ni mapema kusema lolote kuhusiana na ubabe labda baada ya mchezo huo, ni timu nne pekee ambazo hazijapoteza pointi, huku mbili kati yake zikikabiliana kwenye Uwanja wa Emirates Jumapili.

Mabingwa watetezi Arsenal wameweka ishara ya mapema katika mbio za kutetea taji baada ya kupata ushindi katika mechi mbili dhidi ya Coventry City na Aston Villa bila kuruhusu bao.

Kwa upande mwingine, Xabi Alonso tayari ameiongoza Chelsea katika michezo miwili ya kusisimua kwenye Ligi Kuu England, ambapo The Blues iliifunga Fulham na Brighton katika michezo iliyokuwa na mabao mengi. Pia waliifunga Luton Town kwenye Carabao, hivyo kuendeleza mwanzo mzuri wa kocha huyo Mhispania.

Chelsea ilipata ushindi katika mechi zake nne za kwanza za msimu mara ya mwisho 2016-17, katika michezo minne ya mwanzo ya Antonio Conte. Pia ilishinda mechi zake tatu za kwanza za Ligi Kuu 2018-19 chini ya Maurizio Sarri na kwa maana nyingine Alonso atakuwa akilenga kuiga mafanikio hayo na kutuma ujumbe kuhusu nia ya Chelsea katika msimu huu.

Hata hivyo, upande wa ulinzi unaweza kuwa tayari unampa Alonso wasiwasi, kwani Chelsea imetumia mechi 18 za ligi bila kupata clean sheet, ikiwa ni mfululizo mrefu zaidi bila kutoruhusu bao katika mashindano ya ligi tangu ilipocheza mechi 31 mfululizo bila kufungwa kati ya Novemba 1960 na Agosti 1961.

Kipa mpya Emiliano Martínez aliingizwa moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza dhidi ya Brighton katika mchezo uliopita, baada ya kutangazwa saa chache kabla ya mchezo kuanza. Sasa atakuwa akitumaini kutoruhusu bao dhidi ya klabu yake ya zamani. Hata hivyo, upande wa ushambuliaji, Chelsea imekuwa bora, huku Joao Pedro, Morgan Rogers na Cole Palmer wakionekana kuzoeana vizuri.

Arsenal pia ina ubora katika safu ya ushambuliaji kuisumbua Chelsea, huku Bukayo Saka akianza msimu kwa kiwango bora. Amefunga katika kila moja ya mechi zake mbili za mwisho za ligi. Mara ya mwisho alipofunga katika mechi nyingi mfululizo ilikuwa kati ya Januari na Februari 2024, alipofunga katika mechi tano mfululizo.


VIKOSI VINAVYOTARAJIWA

Arsenal: David Raya, Ben White, Ezri Konsa, Gabriel Magalhães, Riccardo Calafiori, Declan Rice, Myles Lewis-Skelly, Martin Ødegaard, Bukayo Saka, Christos Tzolis, Kai Havertz.

Chelsea: Emiliano Martínez, Wesley Fofana, Maxence Lacroix, Levi Colwill, Pedro Neto, Malo Gusto, Roméo Lavia, Jorrel Hato, Cole Palmer, Morgan Rogers, Joao Pedro.

Kocha: Xabi Alonso.


MAN UTD, EVERTON MZIGONI

Mapema, kocha wa zamani wa Manchester United, David Moyes atarikabisha chama lake katika mchezo wa mapema utakaopigw akuanzia saa 10:00 jioni, ikiwa ni mechi mojawapo ya kibabe wikiendi hii. Itakumbukwa mechi kati ya Everton na Manchester United huwa sio rahisi licha ya Man United kuonekana kuwa bora katika miaka ya karibuni uwanjani.