Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fainali ya rekodi, historia WAFCON

Muktasari:

  • Mashindano hayo ambayo kwa mwaka huu yalipigwa Morocco kuanzia Julai 26 na kutamatika leo Agosti 16 kwenye fainali bora itakayowakutanisha Cameroon dhidi ya Malawi.

NI leo saa 2:00 usiku katika Dimba la Moulay El Hassan mjini Rabat, Morocco itakwenda kushuhudiwa fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wanawake (WAFCON) baada ya kushubiri kwa  siku 21.

Mashindano hayo ambayo kwa mwaka huu yalipigwa Morocco kuanzia Julai 26 na kutamatika leo Agosti 16 kwenye fainali bora itakayowakutanisha Cameroon dhidi ya Malawi.

Ni vita ya historia, heshima na uthibitisho wa mabadiliko makubwa yanayoendelea kwenye soka la wanawake barani Afrika.

Zaidi ya yote ni vita ya maokoto kwani mwaka huu pesa za mshindi wa kwanza zimeongezeka kwa asilimia kubwa. Bingwa mwaka huu ataondoka na zaidi ya Sh5.1 bilioni, huku mshindi wa pili akipata takribani Sh1.9 bilioni.

Ni fainali ya kipekee kwa sababu Malawi, ambayo ni mara yake ya kwanza kushiriki fainali hizo, imefika hatua ambayo hata mataifa yenye historia kubwa yalishindwa kufika.

Hii ni fainali ya 14 ya mashindano hayo yaliyoanzishwa mwaka 1991 wakati huo yakijulikana kama Michuano ya Afrika kwa wanawake (African Womens Championship) kabla ya kubadilishwa jina mwaka 2015 na kuitwa Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wanawake.

Katika mashindano hayo Nigeria ndio timu pekee iliyocheza fainali nyingi ikicheza 10 na kushinda mataji 10 (1998,2000

2002, 2004, 2006, 2010, 2014, 2016, 2018, 2024), Equitorial Guinea (2008,2012), ikitwaa mataji mawili na Afrika Kusini taji moja (2022).


SAFARI YA MALAWI

Kwenye timu 16 zilizoshiriki mashindano hayo Malawi, Cape Verde na Tanzania ndio timu pekee zilikuwa hazipewi nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwenye WAFCON kutokana na rekodi zao.

Malawi ilianza kuonyesha dalili mapema baada ya kuichakaza mabingwa wenye historia ya kutwaa mataji 10 ya WAFCON mabao 3-2 kwenye mechi ya kwanza ya kundi C. Ikashinda tena mabao 3-1 dhidi ya Misri na kupoteza mechi ya mwisho dhidi ya Zambia kwa bao 1-0.

Kilichoendeleza kuwashangaza mashabiki timu hiyo ikaitoa Ghana kwenye mechi ya robo fainali kwa mabaoi 2-1 kabla ya kufika nusu fainali ambako iliondoa Algeria na kushinda 3-1, matokeo yaliyoipeleka fainali ya kwanza na kuipa tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia. Mafanikio ya timu hiyo yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na ndugu wawili wanaocheza nafasi ya ushambuliaji, Tabitha na Temwa Chawinga.

Ndugu hao wamefunga jumla ya mabao tisa kwenye mechi tano za mashindano hayo, Temwa akiongoza kwa kuweka kambani mabao matano huku Tabitha akifunga manne. Hivyo, Cameroon inajua wazi kuwa inakutana na timu yenye kasi, kujiamini na wachezaji wanaoweza kubadilisha mchezo kwa  muda mfupi.


CAMEROON, FAINALI YA NNE

Kwa Indomitable Lionesses hii ni fainali ya tano sasa katika historia yake na zote haijawahi kuchukua kombe.

Cameroon ilipoteza fainali zote nne zilizopita dhidi ya bingwa mtetezi, Nigeria mwaka 1991 ikapoteza kwa mabao 2–0 mwaka 2004 ilitandikwa mabao 5-0, mwaka 2014 ikapoteza tena 2-0 na 2016 ikadundwa kwa bao 1-0.

Mwaka huu Indomitable Lionesses ilimaliza kinara wa kundi D ikikusanya pointi saba, ilianza kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mali, ikashinda bao 1-0 dhidi ya Ghana na kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Cape Verde.

Ilipotinga hatua ya robo fainali iliiondoa bingwa mtetezi kwa bao 1-0 kisha kutinga nusu fainali ilipowatoa wenyeji Morocco kwa mikwaju ya penati 3-1 kufuatia suluhu ya bila kufungana.

Katika mechi tano za mashindano hayo Cameroon imeruhusu bao moja ikifunga mabao saba.

Hiyo ina maana kuwa ni timu  iliyo imara kiulinzi na kwamba Malawi itapaswa kuwa na ubunifu kuvunja safu hiyo.

Timu hiyo inawategemea zaidi kipa wake Michaely Bihina mwenye miaka 22 amekuwa mmoja wa wachezaji wanaozungumziwa zaidi katika mashindano hayo.

Baada ya kufanya saves tisa dhidi ya Nigeria, Bihina aliokoa penalti muhimu dhidi ya Morocco.

Hivyo Malawi inaingia kwenye fainali hiyo ikiwa inafahamu wazi kuwa ugumu wakataokutana nao kwenye safu ya ulinzi kabla ya kumfikia Bihina.


NINI KINATARAJIWA?

Kwanza, kasi ya Malawi dhidi ya uzoefu wa Cameroon. Malawi imeonyesha katika mashindano haya kuwa inaweza kushambulia kwa kasi na kutumia nafasi. Ushindi dhidi ya Nigeria ni ushahidi mkubwa wa uwezo huo.

Cameroon itatumia uzoefu  wa mechi kubwa, hasa kutokana na kuwa imewahi kucheza fainali nne za WAFCON dhidi ya mpinzani mgumu.

Pili, eneo la kiungo linaweza kuwa muhimu. Timu itakayoweza kutawala eneo hilo itaweza kudhibiti kasi ya mchezo na kuwapa washambuliaji nafasi za kutengeneza hatari.

Tatu, uzoefu wa Cameroon katika mechi zenye presha unaweza kuwa silaha kubwa, lakini Malawi tayari imeonyesha inaweza kuhimili presha ya timu kubwa. Baada ya kuifunga Nigeria, Ghana na Algeria, haitakuwa rahisi kuingiwa na hofu mbele ya Cameroon.


FAINALI YA DOLA

Mbali na heshima, fainali hii ina thamani kubwa kifedha.

CAF imeongeza zawadi ya mshindi wa WAFCON hadi Dola 2 milioni ikiwa ni mara mbili ya kiasi cha awali. Jumla ya fedha za zawadi katika mashindano hayo imefikia Dola 5.8 milioni, huku mshindi wa pili akitarajiwa kukunja mkwanja unaofikia Dola 750,000.

Hii ni sehemu ya mabadiliko makubwa yanayoonekana kwenye soka la wanawake Afrika. Mashindano yameongezwa kutoka timu 12 hadi 16, huku timu nne zilizofika nusu fainali zikipata tiketi ya Kombe la Dunia la Wanawake 2027.