Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Everton yamnasa nyota wa Arsenal

EVERTON Pict

Muktasari:

  • Hata hivyo, ripoti mbalimbali nchini England zinaeleza kuwa Everton imelipa takribani Pauni 7milioni kumnasa kiungo huyo wa kimataifa wa Denmark mwenye umri wa miaka 32.

LONDON, ENGLAND: EVERTON imeendelea kujiimarisha kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu England baada ya kukamilisha usajili wa kiungo Christian Norgaard kutoka Arsenal kwa mkataba wa miaka miwili, huku ada ya uhamisho ikisalia kuwa siri.

Hata hivyo, ripoti mbalimbali nchini England zinaeleza kuwa Everton imelipa takribani Pauni 7milioni kumnasa kiungo huyo wa kimataifa wa Denmark mwenye umri wa miaka 32.

Norgaard alijiunga na Arsenal mwaka jana akitokea Brentford kwa ada iliyokadiriwa kufikia Pauni15 milioni, lakini alishindwa kupata nafasi ya kudumu kikosini.

Katika msimu uliopita alicheza mechi 20 katika mashindano yote akiwa na Arsenal, huku saba pekee zikiwa za Ligi Kuu England, msimu ambao 'The Gunners' walitwaa ubingwa wao wa kwanza wa ligi baada ya kusubiri kwa miaka 22.

EVER 01

Kiungo huyo aliachwa nje ya kikosi cha Arsenal kilichocheza mechi ya kirafiki dhidi ya Real Betis Jumatano, jambo lililoashiria kuwa alikuwa mbioni kuondoka klabuni hapo.

Baada ya kukamilisha usajili huo, Norgaard amesema mazungumzo yake na kocha David Moyes ndiyo yaliyomshawishi kuhamia Goodison Park.

"Nilivutiwa sana na mradi wa Everton baada ya kuzungumza na kocha. Kufika hapa kumenifanya niamini zaidi kuwa nimefanya uamuzi sahihi," amesema.

Ameongeza kuwa anaamini Everton ipo kwenye mwelekeo mzuri wa maendeleo.

"Ninaona klabu inakwenda kwenye njia sahihi na msimu uliopita ulithibitisha hilo. Walikuwa na kikosi kizuri na ilikuwa vigumu sana kucheza dhidi yao," ameongeza.

Kabla ya kuhamia Arsenal, Norgaard alidumu Brentford kwa miaka sita, akicheza mechi 196 na kuwa nahodha wa timu hiyo kutokana na kiwango chake bora.

EVER 02

Usajili wake ni sehemu ya mkakati wa Moyes kuongeza uzoefu kikosini baada ya kuondoka kwa beki mkongwe Seamus Coleman (37) na kiungo Idrissa Gueye (36).

Majira haya ya kiangazi Everton pia imemsajili kiungo Hayden Hackney kutoka Middlesbrough kwa Pauni milioni 16.5, pamoja na winga Tyrique George (20) kutoka Chelsea kwa Pauni milioni 18, baada ya nyota huyo kucheza kwa mkopo katika klabu hiyo nusu ya pili ya msimu uliopita.

Aidha, Everton imepata pigo baada ya kiungo James Garner kufanyiwa upasuaji wa nyonga mwezi uliopita, hali inayotarajiwa kumfanya akose mwanzo wa msimu mpya.

Everton itaanza kampeni yake ya Ligi Kuu England kwa kuikaribisha Crystal Palace nyumbani Agosti 22, ikiwa na matumaini ya kuanza msimu kwa ushindi.