Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Estevao Willian: Dakika 23 Chelsea mechi tano EPL

Muktasari:

  • Msimu uliopita katika kikosi hicho ubora wake ulikuwa wa juu na kuchagulia kama namba tatu kwa viungo bora nyuma ya Enzo Fernandez na Moises Caicedo, lakini muda mwigi pia aliutumia akicheza kama mshambuliaji akitokea pembeni. Estevao hucheza namba sita, saba, nane na  11.

LONDON, ENGLAND: KUMEKUWA na taarifa zinazoongezeka kwamba kiungo namba tatu kwa ubora msimu uliopita katika kikosi cha Chelsea, Estevao Willian anazidi kukerwa na muda mdogo wa kucheza, hali ambayo imeifanya Barcelona kuanza kumfuatilia kwa karibu na lolote linadaiwa linaweza kutokea katika dirisha dogo la usajili la Januari 2027

Msimu uliopita katika kikosi hicho ubora wake ulikuwa wa juu na kuchagulia kama namba tatu kwa viungo bora nyuma ya Enzo Fernandez na Moises Caicedo, lakini muda mwigi pia aliutumia akicheza kama mshambuliaji akitokea pembeni. Estevao hucheza namba sita, saba, nane na  11.

Nyota huyo amejijengea sifa ya kuwa miongoni mwa vipaji bora zaidi vya kizazi chake nchini Brazil baada ya kung’ara katika akademi ya Palmeiras, huku Chelsea ikitumia takriban Euro 45 milioni mwaka 2024 kushinda mbio za kumsajili.

Baada ya kutimiza miaka 18, Estevao alijiunga na Chelsea katika majira ya kiangazi ya 2025 na alifanya vizuri katika miezi yake ya mwanzo, lakini maendeleo yake yameonekana kusuasua. Jeraha la misuli ya nyuma ya paja lilimkwamisha katika msimu wake wa kwanza akiwa Chelsea, huku akipata nafasi chache sana chini ya kocha Xabi Alonso msimu huu; amecheza dakika 23 kwenye mechi tano.


Thamani ya soko

Kocha Alonso amekuwa akizungumza kwa kumsifia Estevao mwenye thamani ya Euro 80 milioni kwa sasa sokoni kutokana na kipaji chake, lakini mchezaji huyo amepewa nafasi ya kuanza katika mechi mbili pekee, zote kwenye Kombe la Ligi, na alitolewa wakati wa mapumziko katika ushindi dhidi ya Leeds United.

Mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Brazil haendani kikamilifu na mfumo wa 3-4-3 unaopendelewa na Alonso, jambo ambalo, pamoja na kukosa muda wa kutosha wa kucheza, limezua minong’ono kuhusu mustakabali wake.

Barcelona ilimfuatilia kwa karibu Estevao kabla ya mchezaji huyo kuchagua kwenda England, ambapo mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo, Deco, aliripotiwa kuendelea kuwasiliana na wawakilishi wa mchezaji huyo nchini Hispania. Chelsea haina mpango wa kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19, lakini endapo hali yake ya sasa itaendelea, ni rahisi kuelewa kwa nini Estevao anaweza kuwa na wasiwasi kuhusu mustakabali wake.


Estevão vs dakika alizocheza

Akizungumza akiwa kwenye majukumu ya timu ya taifa kuhusu hali yake ndani ya kikosi cha Chelsea, Estevao alijibu kidiplomasia alipotakiwa kuzungumzia uhusiano wake na kocha.

“Kila kocha ana namna yake ya kucheza na bila shaka, ninafanya kazi kila siku na kutoa kila kitu. Tuna wachezaji wengi wenye kiwango kikubwa Chelsea. Mimi najikita katika kile ninachoweza kukidhibiti na kukifanya. Napopata nafasi, najaribu kutoa kiwango changu bora,” alisema.

Taarifa kutoka Hispania zinadai kwamba Estevao anaamini anaweza kucheza kama mmoja wa viungo washambuliaji wa Alonso, lakini nafasi hiyo kwa sasa inamilikiwa na Cole Palmer.

Alonso ametumia wachezaji 23 katika mechi tano za Chelsea za Ligi Kuu England, lakini ni wawili pekee waliocheza dakika chache kuliko Estevao ambaye amecheza dakika 23 tu kupitia kuingia kwa muda mfupi katika mechi, hivyo kukerwa kwake kunaweza kueleweka.

Chelsea pia haishiriki mashindano ya Ulaya msimu huu, jambo litakalopunguza zaidi nafasi za Estevao kupata muda wa kucheza. Hali ya kifedha ya Barcelona inafanya mpango wowote wa baadaye wa kumsajili Estevao kuonekana kuwa mgumu, lakini mchezaji mwenye kipaji kikubwa kama chake kutumika katika nafasi ya mchezaji wa akiba ni jambo linaloweza kuibua maswali kuhusu maendeleo yake.