Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Enzo aingia ‘top 4’ ya usajili wa gharama

Muktasari:

  • Ingawa dili hilo lilisubiriwa hadi siku za mwisho za dirisha la usajili, Chelsea hatimaye imekubali kumruhusu kiungo huyo kuondoka baada ya kutaka kujiunga tena na kocha wake wa zamani, Enzo Maresca.

MANCHESTER, ENGLAND: HATIMAYE imekuwa rasmi. Baada ya kuhusishwa na Manchester City kwa wiki kadhaa, kiungo wa Chelsea, Enzo Fernandez, amekamilisha uhamisho wake.

Ingawa dili hilo lilisubiriwa hadi siku za mwisho za dirisha la usajili, Chelsea hatimaye imekubali kumruhusu kiungo huyo kuondoka baada ya kutaka kujiunga tena na kocha wake wa zamani, Enzo Maresca.

Fernandez sasa ataungana tena na Maresca, ambaye aliwahi kuwa kocha wake Chelsea kwa msimu mmoja na nusu kabla ya kuondoka Stamford Bridge.

Kwa upande wa Chelsea, kuondoka kwa Fernandez hakutoi pengo lisilozibika, kwani kocha Xabi Alonso bado ana chaguo kadhaa za viungo wenye vipaji ndani ya kikosi chake.

Endapo Alonso ataona kuna haja ya kuongeza nguvu katika eneo hilo, Chelsea pia ina uwezo mkubwa wa kifedha kufanya usajili mwingine.

Uhamisho wa Fernandez kwenda Manchester City pia umeweka jina lake kwenye historia ya usajili wa soka duniani.

City imetumia takribani Euro milioni 146 kumnunua kiungo huyo, kiasi ambacho kitamfanya kuwa mchezaji wa nne ghali zaidi katika historia ya soka kwa mujibu wa takwimu za Transfermarkt.

Rekodi hiyo bado inaongozwa na Neymar, ambaye alihama Barcelona kwenda Paris Saint-Germain kwa Euro milioni 222 mwaka 2017.

Fernandez pia si mgeni katika orodha ya usajili wa gharama kubwa.

Chelsea ilimsajili kutoka Benfica Januari 2023 kwa ada ya takribani Euro milioni 121, hivyo uhamisho wake wa kwenda Manchester City umeongeza zaidi thamani ya biashara yake katika soko la usajili.

Kuondoka kwa Fernandez kunaweza pia kumpa nafasi kubwa zaidi raia mwenzake wa Argentina, Valentin Barco, ambaye Chelsea ilimsajili msimu huu kutoka Strasbourg.

Barco anatarajiwa kupata muda zaidi wa kucheza katika kikosi cha Alonso baada ya Fernandez kuondoka Stamford Bridge.

Kwa Manchester City, usajili huo unampa Maresca mchezaji anayemfahamu vizuri na ambaye anaweza kuwa sehemu muhimu ya mpango wake wa kuijenga upya timu hiyo.

USAJILI GHARAMA ZAIDI KATIKA HISTORIA

1. Neymar — Barcelona → PSG: euro 222 milioni

2. Kylian Mbappe — Monaco → PSG: euro180 milioni

3. Ousmane Dembele — Borussia Dortmund → Barcelona: euro148 milioni

4. Enzo Fernandez — Chelsea → Manchester City: euro146 milioni

5. Alexander Isak — Newcastle United → Liverpool: euro145 milioni

6. Morgan Rogers — Aston Villa → Chelsea: euro138 milioni

7. Elliot Anderson — Nottingham Forest → Manchester City: euro135 milioni

8. Philippe Coutinho — Liverpool → Barcelona: euro135 milioni

9. Joao Felix — Benfica → Atletico Madrid: euro127.2 milioni

10. Jude Bellingham — Borussia Dortmund → Real Madrid: euro127 milioni