Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man City yafunga kibabe dirisha la usajili EPL

ZUGO Pict

Muktasari:

  • Enzo Fernandez ndiye mchezaji ghali zaidi aliyesajiliwa England katika dirisha lililofungwa la majira ya kiangazi ambapo Man City imetumia Pauni 125 milioni (Sh447 bilioni).

Dirisha kubwa la usajili la majira ya kiangazi barani Ulaya,  limefungwa jana saa 6:00 usiku huku kwa Ligi Kuu England (EPL), Manchester City ikionekana imetumia kiasi kikubwa cha fedha.

Man City imetumia kiasi cha Pauni 458 milioni (Sh1.6 trilioni) katika usajili wake huku manunuzi ya kiungo Enzo Fernandez kutoka Chelsea yakichangia kwa kiasi kikubwa kuifanya Man City itumie fedha nyingi.

Timu hiyo imewasajili Ayyoub Bouaddi, Jeremy Monga, Fernandez, Elliot Anderson, Iliman Ndiaye, Pierce Charles, Geronimo Rulli, Mathys Detourbet na Allan Elias.

Enzo Fernandez ndiye mchezaji ghali zaidi aliyesajiliwa England katika dirisha lililofungwa la majira ya kiangazi ambapo Man City imetumia Pauni 125 milioni (Sh447 bilioni).

Chelsea inashika nafasi ya pili kwa kutumia kiasi kikubwa cha fedha katika usajili ikitumia kiasi cha Pauni 349 milioni (Sh1.3 trilioni) na iliyopo nafasi ya tatu ni Tottenham Hotspur iliyotumia Pauni 302 milioni (Sh1.1 trilioni).

Ni dirisha lililoweka rekodi mpya ya matumizi makubwa ya fedha kwa timu za Ligi Kuu England kulinganisha na mengine hapo nyuma.

Jumla ya Pauni 3.46 bilioni (Sh12.4 bilioni) imetumika na klabu 20 za EPL katika kufanya usajili wa kuimarisha vikosi vyao kwenye dirisha lililofikia tamati.

Kiasi hicho kinavunja rekodi ya dirisha kubwa la usajili la majira ya kiangazi mwaka jana ambapo kilitumika kiasi cha Pauni 3.14 milioni (Sh11 trilioni).

Hull City ndio timu iliyosajili idadi kubwa ya wachezaji kulinganisha na nyingine katika Ligi Kuu England ambapo imenasa wachezaji wapya 18.