Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Edu Gaspar aondoka Nottingham Forest

EDU Pict

Muktasari:

  • Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 48 hakuwahi kuonekana katika mchezo wa Forest tangu Februari, huku taarifa zikieleza kuwa mwezi uliofuata alipewa maagizo ya kutofika katika uwanja wa mazoezi wala Uwanja wa City Ground.

NOTTINGHAM, ENGLAND: MKURUGEZI wa zamani wa masuala ya soka wa Nottingham Forest, Edu Gaspar, ameondoka rasmi katika klabu hiyo baada ya mkataba wake kusitishwa, miezi sita tangu alipoelezwa kutofika tena katika maeneo ya klabu.

Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 48 hakuwahi kuonekana katika mchezo wa Forest tangu Februari, huku taarifa zikieleza kuwa mwezi uliofuata alipewa maagizo ya kutofika katika uwanja wa mazoezi wala Uwanja wa City Ground.

Kuondoka kwa Edu hakukuwa jambo la kushangaza baada ya agizo hilo, na sasa klabu imethibitisha rasmi kusitisha mkataba wake.

Edu alijiunga na Forest Julai 2025 akitokea Arsenal, ambako alikuwa na nafasi muhimu katika mabadiliko ya klabu hiyo chini ya kocha Mikel Arteta.

ED 01

Mmiliki wa Forest, Evangelos Marinakis, alimpa Edu jukumu la kusimamia masuala yote yanayohusu soka, yakiwamo usajili wa wachezaji, maendeleo ya kikosi, mikakati ya timu na ukuzaji wa vipaji.

Majukumu yake pia yalihusisha klabu nyingine zinazomilikiwa na Marinakis, ikiwamo Olympiacos ya Ugiriki na Rio Ave ya Ureno.


MGOGORO NA NUNO

Inadaiwa Edu alitofautiana na aliyekuwa kocha wa Forest, Nuno Espirito Santo, wiki chache tu baada ya kuwasili kwake City Ground.

Mvutano huo ulitajwa kuwa miongoni mwa sababu zilizochangia Nuno kuondoka klabuni hapo.

Kocha huyo Mreno aliwahi kuikosoa hadharani sera ya Forest ya usajili, huku akionekana kupata ugumu kufanya kazi chini ya mfumo mpya ulioanzishwa baada ya kuwasili kwa Edu.

ED 02

Nuno alifutwa kazi baada ya mechi tatu tu za msimu, licha ya kuiwezesha Forest kufuzu kushiriki Europa League miezi michache kabla.

Kuondoka kwake kulikuwa mwanzo wa msimu wenye misukosuko kwa Forest, ambao walipitia makocha wanne katika msimu mmoja. Baada ya Nuno, waliongozwa kwa vipindi vifupi na Ange Postecoglou, Sean Dyche na Vitor Pereira.


HATATAFUTWA MRITHI

Edu hatarajiwi kupewa mrithi wa moja kwa moja katika klabu hiyo, kwani Ofisa Mkuu wa Masuala ya Soka wa Forest, George Syrianos, tayari amechukua majukumu aliyokuwa akiyafanya Mbrazil huyo.

Kabla ya kujiunga na Forest, Edu alikuwa Mkurugenzi wa Michezo wa Arsenal kwa miaka mitano na nusu. Alifanya uamuzi wa kushangaza kuondoka Arsenal Novemba 2024 na baadaye akaondoka rasmi Aprili 2025, baada ya kumaliza kipindi cha mapumziko.

ED 03

Edu pia alikuwa kiungo wa zamani wa Arsenal na alikuwa sehemu ya kikosi maarufu cha “Invincibles” kilichomaliza msimu wa Premier League bila kupoteza mchezo.

Kwa sasa, Forest iko chini ya kocha Oliver Glasner na imeanza msimu mpya wa Premier League kwa sare mbili na kupoteza mchezo mmoja katika mechi zake tatu za mwanzo.