Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Eberechi Eze anavyoleta utamu Arsenal

EZE Pict

Muktasari:

  • Arsenal imefikia makubaliano ya kimsingi ya kumsajili Eberechi Eze kutoka Crystal Palace, ikifanikiwa kumchukua mbele ya mahasimu wao Spurs, ambao walionekana kabisa kuwa kwenye hatua za mwisho kumsajili.

LONDON, ENGLAND: MIKEL Arteta amefanya umafia dhidi ya mahasimu wao wa London Kaskazini baada ya Arsenal kufanikiwa kunasa saini ya mshambuliaji ambaye alikuwa akielekea kwa wapinzani wao Tottenham Hotspur.

Arsenal imefikia makubaliano ya kimsingi ya kumsajili Eberechi Eze kutoka Crystal Palace, ikifanikiwa kumchukua mbele ya mahasimu wao Spurs, ambao walionekana kabisa kuwa kwenye hatua za mwisho kumsajili.

Arsenal imekuwa ikilialia kutokuwa na ubunifu wa kutosha kwenye eneo la ushambuliaji kwa misimu kadhaa ya hivi karibuni, hivyo hakuna shaka yoyote kwamba Eze atakwenda kuongeza kitu kikubwa kwenye kikosi hicho baada ya kuhusika kwenye mabao 16 ya Ligi Kuu England msimu uliopita.

Eze bila shaka atakweda kumaliza tatizo hilo, lakini kuna jambo moja hapa: Atakwenda kucheza nafasi gani?

Kutokana na Bukayo Saka kucheza wingi ya kulia na uwepo wa straika mpya wa Pauni 63.5 milioni, Viktor Gyokeres kwenye eneo la mshambuliaji wa kati, Arsenal eneo ambalo bado lina udhaifu mkubwa kwa sasa ni wingi ya kushoto.

Eze anaweza kucheza eneo hilo, lakini si eneo lake pekee la ubora analoweza kuitumikia Arsenal, wakati kocha Arteta atakapomtumia.

Lakini, kama Eze atataka kucheza kwenye eneo lake analolimudu zaidi la kiungo wa kati, hiyo ina maana Arteta atalazimika kumweka benchi mmoja wa mastaa wake wakubwa kwenye kikosi hicho.

Hata hivyo, hizi hapa Arsenal tatu tofauti, ambazo kocha Arteta anaweza kupanga kikosi chake kutokana na ujio huo wa Eze kwenye chama la Emirates.

EZ 01
  1. Eze kwenye wingi ya kushoto

Katika kuongeza makali ya kikosi cha kwanza cha Arsenal kilichopo kwa sasa, kumtumia Eze kwenye wingi ya kushoto ni kitu kinachoonekana kupewa nafasi kubwa kwa sasa. Eze, 27, ni ingizo bora kabisa kwa kuwalinganisha na Gabriel Martinelli na Leandro Trossard, ambao mara nyingi wamekuwa wakitumika kwenye nafasi hiyo ya wingi ya kushoto. Wakati huo huo, mashabiki wa Arsenal watakuwa wakijiuliza juu ya usajili wa winga Noni Madueke kutoka Chelsea.

Hata hivyo, Eze katika mechi tatu alizocheza kama winga wa kushoto huko Palace msimu uliopita, hakufunga wala kuasisti bao lolote.

Kocha Arteta atachagua kumtumia Eze wingi ya kushoto ili asitibue safu yake ya viungo wa kati watatu, Declan Rice, Martin Odegaard na Martin Zubimendi.

EZ 02

2. Eze kwenye kiungo ya kati

Kutumia zaidi ya Pauni 60 milioni kusajili mchezaji kisha unakwenda kumpanga kwenye namba ambayo hawezi kuimudu vyema huo ni ujinga, hivyo ujio wa Eze huko Emirates utakwenda kutibua hali ya mambo kwenye viungo wa kati kutokana na eneo hilo kuwa mwafaka kwa Mwingereza huyo. Kumtumia Eze kwenye kiungo ya kati hiyo itamfanya Arteta kuugua kichwa kwa sababu atalazimika kumchomoa staa wake mmoja kwenye eneo hilo.

Mmoja kati ya Rice, Zubimendi au Odegaard atalazimika kukaa benchi ili kutoa nafasi kwa Eze kuingia kwenye eneo hilo la kati ya uwanja ili afanye maajabu yake ya kutengeneza nafasi za mashambulizi ya kibabe.

Arteta anaweza kumshusha chini kabisa Rice, huku Odegaard anaweza kubebwa na unahodha wake, hivyo staa wa Pauni 56 milioni, Zubimendi benchi litamhusu.

EZ 03
  1. Eze kwenye fomesheni ya 3-4-3

Kuna namna moja ambayo Arteta anaweza kuwa na wachezaji wake wote muhimu ndani ya uwanja kwa wakati mmoja, lakini jambo hilo litamlazimu kubadili staili ya uchezaji iliyozoeleka na miamba hiyo ya Emirates. Hapo ina maana, kocha Arteta atalazimika kwenda na mfumo wa kutumia mabeki wa kati watatu, ili kumtumia Eze kwenye moja ya washambuliaji watatu, huku viungo wote Rice, Odegaard na Zubimendi wakipata nafasi ya kucheza.

Kwenye mfumo huo, Saka na Madueke watatumika kama wing-backs, wakikaa kwenye mstari wa wachezaji wanne wa kati, sambamba na viungo wawili, Rice na Zubimendi. Odegaard na Eze watachangia Namba 10, wakicheza nyuma ya straika Gyokeres, katika kikosi hicho tishio kwelikweli.

Mastaa watatu watakuwa kwenye safu ya ulinzi ni Riccardo Calafiori, William Saliba na Gabriel Magalhaes. Arteta akianza hivyo, Arsenal itakuwa balaa.