Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Duh! Rashford asiende Barcelona

RASHFORD Pict

Muktasari:

  • Taarifa zinaeleza kuwa miamba hiyo ya Hispania inapanga kumwania mshambuliaji huyo wa Man United ambaye hayupo tena kwenye mipango ya kocha Ruben Amorim.

MANCHESTER, ENGLAND: GWIJI wa zamani wa Manchester United, Teddy Sheringham amedai kuwa mshambuliaji wa timu hiyo Marcus Rashford “hastahili” kupata uhamisho wa majira haya ya kiangazi kwenda Barcelona.

Taarifa zinaeleza kuwa miamba hiyo ya Hispania inapanga kumwania mshambuliaji huyo wa Man United ambaye hayupo tena kwenye mipango ya kocha Ruben Amorim.

Rashford, ambaye anaweza kucheza nafasi mbalimbali za ushambuliaji, amerudi hivi karibuni kutoka kwa mkopo Aston Villa, aliyojiunga nayo katika dirisha lililopita ikiwa ni baada ya kuweka wazi kwamba alikuwa tayari kwa changamoto mpya.

Amekuwa akiendelea na mazoezi kwenye kituo cha Carrington huku akitafuta klabu mpya, na baadhi ya ripoti zinadai Liverpool inahusishwa na usajili wake.

Klabu nyingi tayari zimeonyesha nia kwa Rashford lakini hadi sasa hakuna ofa ya pesa iliyowasilishwa, huku Manchester United wakiripotiwa kuhitaji Pauni 40 milioni.

SunSport inaeleza kuwa mshambuliaji huyo anahitaji kuondoka hata kwa mkopo tena ikiwa haitatokea timu itakayokuwa tayari kumnunua.

Kwa muda mrefu Rashford amekuwa na ndoto ya kuvaa jezi ya Barcelona na kucheza Nou Camp na ndoto hiyo huenda ikatimia, kwani Barcelona wanatafuta mchezaji mpya atakayecheza wingi ya kushoto katika safu yao ya ushambuliaji.

Awali, walimtaka Nico Williams, lakini alisaini mkataba mpya na Athletic Bilbao, pia wakahamia kwa Luis Diaz, ambaye sasa anawaniwa na Bayern Munich kwa dau kubwa. Hivyo Rashford anaonekana kuwa chaguo pekee la timu hiyo kwa sasa.

Hata hivyo, mshambuliaji wa zamani wa Man United, Sheringham, anaamini kwamba Rashford hastahili dili la aina hiyo kutokana na tabia zake za hivi karibuni.

Sheringham, aliyefunga bao la kusawazisha katika dakika ya 91 kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa mwaka 1999 kabla ya Ole Gunnar Solskjaer kufunga la ushindi, anasema msimamo wa Rashford wa kutaka kuondoka Man United anaona kwake haikuwa sahihi ni kama alionyesha dharau.

Pia anakiri kuwa kutokana na hali ya sasa ya Man United, uhamisho wake wa kwenda Barcelona itakuwa ni hatua ya juu lakini anahisi Rashford hastahili nafasi hiyo, na anatumai dili hilo halitakamilika.

Sheringham aliambia Sky Bet: "Ukimtazama Marcus Rashford alipo sasa, kama mchezaji wa soka wa kulipwa, unapoanza ukiwa kijana ndoto ni kufika kileleni na kuchezea klabu kama Manchester United, na ukiwa hapo, unatakiwa kuthamini nafasi hiyo. Huitupi mbali kwa kusema unataka kuondoka. Kwa mtazamo wangu, kutoka Man United kwenda Barcelona ni hatua ya juu ambayo hajaitendea haki."

"Najihisi kuumizwa sana na jambo hili tofauti kabisa na enzi zangu ambapo nilihangaika sana kupata heshima ya kucheza katika klabu kubwa kama hiyo. Kusikia mtu akizungumza namna Rashford anavyosema, kwamba anataka kuondoka sikupendezwa hata kidogo. Sikuwa shabiki wa Aubameyang alipofanya hivyo kule Arsenal, niliona ni jambo la kusikitisha. Natumai Rashford hatopata uhamisho anaoutamani."