Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Douglas Luiz awekwa kwenye rada Man United

Muktasari:

  • Hata hivyo, saini yake itawaingiza kwenye vita kali Man United kutokana na mkali huyo wa zamani wa Aston Villa kuwamo pia kwenye rada za Everton.

MANCHESTER United inaripotiwa kuhitaji huduma ya kiungo wa Juventus na timu ya taifa ya Brazil, Douglas Luiz kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi.

Hata hivyo, saini yake itawaingiza kwenye vita kali Man United kutokana na mkali huyo wa zamani wa Aston Villa kuwamo pia kwenye rada za Everton.

Luiz, 27, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika 2029, ambapo msimu uliopita alicheza mechi 27 za michuano yote na hakufunga wala kuasisti.

Licha ya kuwapo kwa ushindani kutoka kwa Everton inayonolewa na kocha wa zamani wa Man United, David Moyes, ripoti zinafichua miamba hiyo ya Old Trafford ndiyo yenye nafasi kubwa ya kupata huduma yake, ikimhitaji kwa mkopo kwanza ambapo itaweka kipengele cha kumchukua jumla mwisho wa msimu ikivutiwa na ubora wake.

Hata hivyo, kwa sasa Juventus inataka kwanza kuangalia timu itakayokuwa tayari kumnunua jumla badala ya kumtoa kwa mkopo na kama itashindikana hilo kutokea ndio itakapoamua njia mbadala.

Staa huyu wa zamani wa Aston Villa amekuwa akihusishwa kurudi England tangu mwaka jana na kwa mujibu wa taarifa kutoka Italia, benchi la ufundi la Juventus halihitaji kuendelea naye kwa msimu ujao na tayari limeshatoa mapendekezo ya wachezaji ambao inahitaji wasajiliwe kama mbadala wake.

Kocha wa Man United, Ruben Amorim anahitaji sana huduma ya Luiz kuelekea msimu ujao ambapo amepanga kujenga upya kikosi baada ya kufanya vibaya msimu uliopita.


Hugo Ekitike

LIVERPOOL imeingia katika vita dhidi ya Newcastle United kwa ajili ya kuipata saini ya mshambuliaji wa Eintracht Frankfurt, Hugo Ekitike, mwenye umri wa miaka 23, katika dirisha hili.

Mabosi wa Liverpool wameamua kuingia katika vita hiyo baada ya  kuambiwa kuwa mshambuliaji wa kimataifa wa Sweden, Alexander Isak, 25, anauzwa kwa Pauni 150 milioni katika dirisha hili, dau ambalo ni maji yenye kina kirefu kwao.

Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2029. Msimu uliopita alicheza mechi 48 za michuano yote na kufunga mabao 22.


Ollie Watkins

LIVERPOOL imeendelea kuwasiliana na timu mbalimbali kwa ajili ya kusajili washambuliaji ambapo kwa mujibu wa ripoti kutoka Daily Mail, majogoo hao wapo katika mazungumzo na timu nne ikiwemo Aston Villa kwa ajili ya Ollie Watkins, 29, Napoli kuhusu Victor Osimhen, Brentford kwa ajili ya Yoane Wissa na Real Madrid kuhusu Rodrygo, 24.

Mastaa hawa wote wapo katika machaguo ya kocha Arne Slot ingawa chaguo lake la kwanza kabisa ni kunasa huduma ya straika Hugo Ekitike na ikishindiakana ndio watahangaika kwa wachezaji hao wengine.


Darwin Nunez

NAPOLI imeachana na mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Liverpool na timu ya taifa ya Uruguay, Darwin Nunez, 26, katika dirisha hili ikielezwa moja kati ya sababu zilizochangia ni kiasi cha pesa ambacho Liverpool inakihitaji kama ada yake ya uhamisho.

Nunez ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika 2028, msimu uliopita alicheza mechi 47 za michuano yote, amefunga mabao saba na kutoa asisti saba.


Luis Diaz

LICHA ya Liverpool kukataa ofa ya Pauni 58.6 milioni kutoka Bayern Munich inayohitaji saini ya winga wa timu hiyo na Colombia, Luis Diaz, 28, staa huyo ameweka wazi kuwa  anataka kuondoka katika dirisha hili uhamisho wa majira ya kiangazi huko Ulaya.

Inaelezwa Diaz amevutiwa na ofa ya Bayern na anataka kwenda kujaribu changamoto mpya Ujerumani akiwa na wababe hao wa Allianz Arena.

Msimu uliopita Diaz alicheza mechi 57 za michuano yote, alifunga mabao 17 na kutoa asisti nane. Mkataba wake unatarajiwa kumalizika 2027.


Sean Longstaff

LEEDS United imefikia makubaliano ya awali ya kumsajili kiungo wa Newcastle United, Sean Longstaff, mwenye umri wa miaka 27, katika dirisha hili.

Katika msimu uliopita Longstaff alicheza mechi 32 za michuano yote na anataka kuondoka kwa sababu hapati nafasi ya kutosha kwenye kikosi cha Newcastle wakati Leeds imemhakikishia kuwa atakuwa sehemu ya kikosi chao cha kwanza.

Newcastle ipo tayari kumwachia ili kuzidi kuongeza pesa ambazo itazitumia katika usajili wa wachezaji inaowahitaji katika dirisha hili.


Koni de Winter  

TOTTENHAM Hospur ipo katika vita kali dhidi ya Inter Milan kwa ajili ya kuipata saini ya beki kisiki wa Genoa na Ubelgiji, Koni de Winter, 23, katika dirisha hili.

Inter ndio ilikuwa ya kwanza kuanza mazungumzo na Genoa kwa ajili ya kuipata huduma yake, lakini kuingia kwa Spurs katika harakati hizo kumefanya dili kuwa gumu na thamani ya mchezaji kuongeza.

Kwa sasa Genoa ipo tayari kumwachia staa huyu, lakini inahitaji takribani Euro 40 milioni kama ada yake ya uhamisho.


Illia Zabarnyi

MABOSI wa Bournemouth wameweka wazi kuwa wanahitaji kiasi kisichopungua Pauni 59 milioni kama ada ya uhamisho ya beki wao wa kati kutoka Ukraine, Illia Zabarnyi, 22, katika dirisha hili.

Staa huyu ambaye anahusishwa na Paris Saint-Germain, amevutia vigogo wengi Ulaya kutokana na kiwango bora alichoonyesha msimu uliopita.

Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika 2029, msimu uliopita alicheza mechi 39 za michuano yote.