Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Siku za Martinelli zinahesabika Arsenal

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali, Martinelli alishindwa kupata nafasi ya kudumu katika kikosi cha Arsenal msimu uliopita, baada ya Leandro Trossard kupewa nafasi zaidi na kocha Mikel Arteta.

Winga wa Arsenal, Gabriel Martinelli, anaweza kuondoka katika klabu hiyo katika dirisha hili la usajili kutokana na kupoteza nafasi yake katika kikosi cha kwanza.

Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali, Martinelli alishindwa kupata nafasi ya kudumu katika kikosi cha Arsenal msimu uliopita, baada ya Leandro Trossard kupewa nafasi zaidi na kocha Mikel Arteta.

Hali hiyo imezidi kuwa ngumu kwa Mbrazil huyo baada ya Arsenal kumsajili winga wa Ugiriki, Christos Tzolis, kutoka Club Brugge kwa ada ya Pauni milioni 34.

Usajili huo umeongeza ushindani katika safu ya ushambuliaji ya Arsenal na huenda ukamfanya Martinelli kutafakari mustakabali wake Emirates.

Martinelli amekuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Arsenal katika misimu iliyopita, lakini kuongezeka kwa chaguo kwenye nafasi yake kunaweza kumlazimisha kutafuta changamoto mpya.

Kwa sasa hakuna makubaliano rasmi kuhusu uhamisho wake, lakini uwezekano wa kuondoka Arsenal katika dirisha hili haujaondolewa.

Moja ya klabu zinazomwania nyota huyo ni Galatasaray ya Uturuki na inachosubiria ni kama Arsenal itamalizana na Martinelli na kumwachia.

Msimu uliopita nyota huyo alicheza mechi 30 za Ligi Kuu England na kufunga bao moja na kutoa pasi nne za mabao.


Curtis Jones

INTER Milan inaendelea kumfukuzia kiungo wa Liverpool, Curtis Jones, lakini italazimika kuongeza dau baada ya Liverpool kuweka thamani ya euro milioni 40. Jones hakuwamo kwenye kikosi cha Liverpool wiki hii, hali iliyoongeza tetesi kuhusu mustakabali wake. Inter iliwahi kujaribu kumsajili Januari, lakini ofa yake ilikataliwa na Liverpool.


Zachary Athekame

AC Milan imefikia makubaliano ya kumtoa kwa mkopo beki Zachary Athekame kwenda Olympique Lyonnais ya Ufaransa msimu ujao. Dili hilo halina kipengele cha Lyon kumsajili moja kwa moja baada ya mkopo kumalizika. Athekame anatarajiwa kuondoka Milan baada ya kushindwa kuonyesha kiwango kilichotarajiwa


Nahuel Molina

BEKI wa Atletico Madrid, Nahuel Molina, anatarajiwa kusafiri kwenda Italia kwa ajili ya vipimo vya afya kabla ya kukamilisha uhamisho wake kwenda AS Roma. Roma itamlipa Atletico euro milioni 13 kama ada ya awali, huku kukiwa na nyongeza ya euro milioni nne kulingana na vigezo vya mkataba, hivyo dili kufikia euro milioni 17.


Adam Wharton

MANCHESTER United imeanza kumfukuzia kiungo wa Crystal Palace, Adam Wharton, huku ikiwa tayari kujaribu nguvu zake dirisha hili. United inataka kumuongeza ili kuimarisha safu ya kiungo, lakini Palace imeweka bei kubwa. Klabu hiyo inataka karibu euro milioni 100 kwa mchezaji huyo anayeweza kucheza nafasi ya kiungo mkabaji.


Joaquin Seys

ARSENAL na Manchester United zimeingia kwenye mbio za kumsajili beki wa pembeni wa Club Brugge, Joaquin Seys. Klabu hizo zinatafuta kuongeza chaguo katika nafasi ya beki wa kushoto na zimemuweka Seys kwenye orodha yao. Club Brugge inataka euro milioni 35, sawa na karibu pauni milioni 30, ili kumruhusu nyota huyo kuondoka.


Robbie Ure

SEVILLA iko hatua za mwisho kumsajili mshambuliaji wa Scotland U21, Robbie Ure, kutoka IK Sirius ya Sweden. Dili hilo linaweza kufikia Euro 9.2 milioni, huku Ure, 22, akitarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya kabla ya kusaini mkataba wa miaka mitano. Sevilla inaamini nyota huyo ataongeza nguvu katika safu yake ya ushambuliaji.


Trevoh Chalobah

BEKI wa Chelsea, Trevoh Chalobah, amejiunga na Como ya Italia kwa uhamisho wenye thamani ya zaidi ya pauni milioni 30. Chalobah, 27, amesaini mkataba wa miaka mitano na klabu hiyo inayofundishwa na Cesc Fabregas. Como ilifuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kumaliza nafasi ya nne kwenye Serie A msimu uliopita.


Endrick

ASTON Villa inaongoza mbio za kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Real Madrid, Endrick, anayehitaji nafasi zaidi ya kucheza kikosi cha kwanza. Wawakilishi wa nyota huyo wa Brazil wamewasiliana na klabu kadhaa za Ligi Kuu England. Endrick sasa anatafakari mustakabali wake Santiago Bernabeu kuelekea msimu mpya.


Harry Kane

MSHAMBULIAJI wa England, Harry Kane, 33, anatarajiwa kuongeza mkataba wake na Bayern Munich hadi mwaka 2029, licha ya kuhusishwa na Barcelona. Kane anaonekana kuwa tayari kuendelea na maisha mjini Munich, ambako amekuwa akivunja rekodi za mabao. Bayern, amefunga mabao 146 katika mechi 147.