Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Donnarumma Manchester United, mikono salama

Muktasari:

  • Donnarumma, 26, hatima ya maisha yake imekuwa kwenye utata mkubwa huko Parc des Princes baada ya kugoma kufikia mwafaka juu ya mkataba mpya.

PARIS, UFARANSA: HABARI ndo hiyo. Manchester United inapiga hesabu kali za kumnasa kipa kiboko kwa kudaka, Gianluigi Donnarumma baada ya klabu yake ya Paris Saint-Germain kukubali ofa ya Pauni 34.9 milioni ya kumsajili kipa mpya.

Donnarumma, 26, hatima ya maisha yake imekuwa kwenye utata mkubwa huko Parc des Princes baada ya kugoma kufikia mwafaka juu ya mkataba mpya.

Mkataba wa sasa wa kipa huyo wa kimataifa wa Italia huko kwenye kikosi cha PSG utafika tamati mwishoni mwa msimu ujao na mabingwa hao wa Ulaya hawataki kumpoteza bila ya kupata chochote kitu.

Kutokana na hilo, kikosi hicho kinachonolewa na Mhispaniola, Luis Enrique sasa kimefungua milango ya kupokea ofa kwa ajili ya Donnarumma baada ya kumpata mbadala wake kwa kufikia makubaliano na Klabu ya Lille juu ya kumsajili kipa Lucas Chevalier. Makubaliano hayo ya PSG yanaweza kuifanya Man United kuingia sokoni kumnyakua Donnarumma, hasa ukizingatiwa kwamba kocha Ruben Amorim anahitaji kipa mpya kwenye goli lake msimu ujao.

Man United inafahamika wazi kuwa kwenye mchakato wa kumfukuzia kipa wa Royal Antwerp, Senne Lammens, ikiamini kwamba atatua kumpa Andre Onana wakati mgumu kwenye ushindani wa namba, lakini kupatikana kwa Donnarumma litakuwa chaguo mwafaka zaidi kwa miamba hiyo ya Old Trafford.

Licha ya Onana kutokuwa na mpango wa kuhama Old Trafford, kiwango cha kipa huyo Mcamerooni kimekuwa tatizo kubwa kwa kocha Amorim. Kocha huyo wa Man United alimshambulia moja kwa moja kipa huyo mwishoni mwa msimu uliopita kutokana na kufanya makosa mengi yaliyoigharimu timu.

Na sasa, badala ya kwenda kumsajili kipa anayechipukia kama Lammens, wakati mzoefu kama Donnarumma yupo sokoni utakuwa usajili bora utakaokwenda kuongeza kitu kwenye vyumba vya kubadilishia na alijadili na wachezaji wenzake wa Italia juu ya mpango wa kuhamia England.

Gazeti la L’Equipe la Ufaransa linaripoti kwamba PSG inajiandaa kumpokea Chevalier, kitu ambacho kimefanya klabu hasimu za Manchester - Man United na Manchester City kuanza kumsaka Donnarumma.

Chelsea nayo inahitaji saini ya kipa huyo sambamba na Galatasaray ya Uturuki. Na haitashangaza kama Man City itaingia nzima nzima kwenye dili la kumtaka Donnarumma baada ya mpango wake wa kumnyakua kipa James Trafford kwa ada ya Pauni 27 milioni kukwama.

Napoli pia imekuwa ikihusishwa na Donnarumma, lakini wakala wake, Enzo Raiola ambaye ni mpwa wa wakala mahiri, Mino amezipuuza taarifa hizo za kuhusu mkali huyo kuwindwa huko Naples.

“Nimekuwa na uhusiano mzuri na mkurugenzi Giovanni Manna (Napoli), lakini hatujawahi kumjadili Gigio,” alisema Raiola.