Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dili la Jadon Sancho kutua AS Roma lafikia patamu

TETESI Pict

Muktasari:

  • Kwa sasa Man United inangoja uamuzi wa mwisho kutoka kwa mchezaji mwenyewe ikiwa atahitaji kujiunga na timu hiyo au laa.

MANCHESTER United ipo tayari kukubali ofa ya AS Roma ya kuwauzia staa wao  Jadon Sancho mwenye umri wa miaka 25 kwa mkopo wenye sharti la kumnunua moja kwa moja mwishoni mwa msimu.

Kwa sasa Man United inangoja uamuzi wa mwisho kutoka kwa mchezaji mwenyewe ikiwa atahitaji kujiunga na timu hiyo au laa.

Mkataba wa sasa wa Sancho na Man United unamalizika mwaka 2026 na ni miongoni mwa mastaa ambao mashetani hao wekundu wamewaweka sokoni dirisha hili.

Roma ambayo inajenga kikosi kwa ajili ya kuonyesha ushindani zaidi katika michuano ya kimataifa ambako wanacheza Europa League msimu huu, ipo pia katika harakati za kusajili wachezaji mbalimbali wa Ligi Kuu England.

Sancho msimu uliopita alicheza kwa mkopo Chelsea, akihusishwa pia kurejea Borussia Dortmund lakini inaonekana changamoto ilikuwa ni pesa kwani timu hiyo iliyokuwa inataka kumchukua kwa mkopo, lakini Man United ilihitaji Dortmund kulipa mshahara wake wote jambo lililokuwa gumu.


 Tyler Dibling

EVERTON bado inapambana kumsajili winga wa Southampton, Tyler Dibling, 19, dirisha hili la majira ya kiangazi. Hadi sasa Southampton imekataa ofa tatu ikiwemo ya mwisho ya Pauni 37 milioni iliyowasilishwa hivi karibuni na Everton. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka  2028. Mabosi wa Soton wapo tayari kumruhusu fundi huyu kuondoka lakini wanataka ofa nono zaidi ambayo itawawezesha kupata mbadala wake.


Ederson

GALATASARAY imewasilisha ofa ya awali ya Pauni 8.6m kwa ajili ya kumsajili kipa wa Manchester City, Ederson mwenue umri wa miaka 31. Mkataba wa sasa Ederson unatarajiwa kumalizika mwaka 2026, lakini Man City inataka kumuuza ili kumsajili kipa wa PSG, Gianluig Donnarumma. Inaelezwa wababe hao wanahitaji karibia Pauni 20 milioni kama ada yake ya uhamisho ingawa inaweza kupokea Pauni 15 milioni.


Lee Kang-in

ARSENAL, Man United na Napoli zipo katika vita kali ya kuiwania saini ya kiungo wa PSG na timu ya taifa ya  Korea Kusini, Lee Kang-in, 24, katika dirisha hili. Kang-in anadaiwa kuomba mwenyewe kuondoka kwa sababu hapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza cha PSG. Mkataba wa staa huyu unatarajiwa kumalizika mwaka 2028. Inaelezwa PSG inaweza kumuuza kwa Euro 25 milioni.


Carlos Baleba

REAL Madrid inaendelea kufuatilia maendeleo ya kiungo wa Crystal Palace, Adam Wharton, 21. Wharton aliingia katika rada za vigogo baada ya kiwango bora alichoonyesha akiwa na kikosi cha Palace msimu uliopita ambapo alicheza mechi 29 za Ligi Kuu England na alifunga mabao matatu na kutoa asisti tano. Mabosi wa Palace wanaripotiwa kuwa hawapo tayari kumwachia kwa sasa kwani itakuwa inaharibu mipango ya kocha wao msimu ujao.


Alejandro Garnacho

MABOSI wa Chelsea wanasubiri kuona ikiwa watawauza washambuliaji waliopo katika timu kwa sasa kabla ya kumsajili Alejandro Garnacho kutoka Manchester United pamoja na winga wa RB Leipzig katika dirisha hili. Chelsea inapambana kuwauza mastaa wake Nicolas Jackson pamoja na Christopher Nkunku ambao hadi sasa timu nyingi zimeonyesha nia ya kuwasajili lakini bado hakuna mwafaka uliofikiwa.

Mkataba wa Garnacho unatarajiwa kumalizika mwaka  2028. Mkataba wa  Simons unamalizika mwaka 2027.


Leon Bailey

AS Roma imefikia makubaliano na Aston Villa kumsajili winga wa timu hiyo, Leon Bailey, 28, kwa mkopo wa msimu mmoja wenye ada ya Pauni 1.7 milioni, pia kuna kipengele cha kumnunua mazima kwa Pauni 20 milioni ifikapo mwisho wa msimu huu. Mkataba wa sasa wa  Bailey na Aston Villa  unamalizika mwaka 2027, msimu uliopita alicheza mechi 38 za michuano yote.


 Arnaud Kalimuendo

KOCHA wa Manchester United, Ruben Amorim bado anahitaji saini ya kiungo wa  Brighton na timu ya taifa ya Cameroon, Carlos Baleba licha ya vigogo wa timu hiyo kudai Pauni 100 milioni ili kumuuza katika dirisha hili. Amorim amewaambia mabosi wa Man United kwamba baada ya kushindikana sasa, staa huyo asajiliwe hata dirisha la majira ya kiangazi mwakani.