Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dili la Guimaraes lakaribia

ARSENAL Pict

Muktasari:

  • Kiungo huyo wa Brazil ameiambia Newcastle kuwa anataka kuzungumza na mabingwa hao wa Ligi Kuu England iwapo klabu hizo zitafikia makubaliano ya ada ya uhamisho ili aanze kazi ya kuitumikia timu hiyo.

NEWCASTLE, ENGLAND: ARSENAL ipo tayari kuwasilisha ofa ya pauni milioni 70 muda wowote kwa ajili ya nahodha wa Newcastle United, Bruno Guimaraes.

Kiungo huyo wa Brazil ameiambia Newcastle kuwa anataka kuzungumza na mabingwa hao wa Ligi Kuu England iwapo klabu hizo zitafikia makubaliano ya ada ya uhamisho ili aanze kazi ya kuitumikia timu hiyo.

Hata hivyo, Newcastle imesisitiza kuwa mchezaji huyo hauzwi na imekuwa ikikerwa na mazungumzo yanayofanywa kupitia mawakala wake badala ya kupokea ofa rasmi.

ARS 01

Licha ya kujua kuwa Guimaraes anatamani kujiunga na Arsenal, Newcastle inahitaji fedha nyingi zaidi ili kumruhusu aondoke.

Kuna taarifa pia kwamba klabu nyingine za Premier League zinamfuatilia kiungo huyo mwenye miaka 28.

Arsenal imeambiwa wazi kuwa kama inamtaka Guimaraes inapaswa kuwasilisha ofa rasmi badala ya kuendelea na mazungumzo yasiyo rasmi.

Msimu uliopita Guimaraes alicheza mechi 41 akiwa na Newcastle na kufunga mabao tisa.

ARSENAL Pict

Mkataba wake umebakiza miaka miwili lakini Newcastle ina kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi.

Kocha Mikel Arteta anataka kuimarisha safu ya kiungo kabla ya kuanza kutetea ubingwa wa Premier League, huku Guimaraes akiwa lengo lake kuu.

Baada ya kuitumikia Newcastle kwa misimu mitano, kiungo huyo anataka changamoto mpya.

Vyanzo mbalimbali vinasema kuwa dili hilo linaweza kukamilika kabla ya Jumatatu ijayo ili mchezaji huyo ajiandae