Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dili la Alvarez lafikia hapa

Muktasari:

  • Atletico ipo tayari kumuuza nyota huyo wa Argentina kabla ya dirisha la usajili kufungwa Jumanne ijayo, lakini imeweka dau la pauni 128 milioni (zaidi ya shilingi bilioni 280) kama bei ya kumwachia.

MADRID, HISPANIA: KLABU ya Atletico Madrid imeripotiwa kumpa mshambuliaji wake, Julian Alvarez, hadi kesho Jumapili kufanya uamuzi kuhusu mustakabali wake, huku Arsenal ikitajwa kuwa mstari wa mbele kuwania saini yake.

Atletico ipo tayari kumuuza nyota huyo wa Argentina kabla ya dirisha la usajili kufungwa Jumanne ijayo, lakini imeweka dau la pauni 128 milioni (zaidi ya shilingi bilioni 280) kama bei ya kumwachia.

Kwa mujibu wa taarifa, Arsenal imekuwa ikifuatilia kwa karibu maendeleo ya Alvarez, huku kocha Mikel Arteta akitajwa kumhitaji mshambuliaji huyo katika kikosi chake.

Hata hivyo, Arsenal si klabu pekee inayomtaka Alvarez, kwani taarifa za hivi karibuni zinadai kuwa Manchester City imefanya mazungumzo ya kutaka kumrejesha mshambuliaji huyo ambaye aliwahi kuitumikia kabla ya kujiunga na Atletico.

Alvarez, mwenye umri wa miaka 26, amekuwa akitafakari mustakabali wake na hali hiyo imezua sintofahamu ndani ya Atletico. Mshambuliaji huyo pia amekosa mazoezi kwa siku nne wiki hii akiwa na wachezaji wenzake.

Taarifa kutoka Sky Sports zinadai kuwa viongozi wa Atletico wamechoshwa na hali hiyo na wamempa Alvarez hadi leo kufanya uamuzi wa mwisho.

ALISHATOA MSIMAMO

Alvarez alionekana kuwa tayari kuondoka Atletico tangu Juni, alipokiri kwamba alizungumza na viongozi wa klabu kuhusu suala hilo na kuona uhamisho ukiwa ndiyo suluhisho bora kwa pande zote.

Alvarez alisema: “Nilizungumza na watu wa Atletico ambao nilihitaji kuzungumza nao, na jambo bora kwa kila mtu ni uhamisho.

“Nataka kutimiza ndoto yangu. Si wakati wa kuzungumza kuhusu hili, lakini pia siwezi kulificha. Ninajaribu kuwa mtu mwaminifu.”

Kutokana na hali hiyo, Alvarez anatarajiwa kukosa mchezo wa Atletico dhidi ya Sevilla utakaopigwa leo katika Uwanja wa Ramon Sanchez Pizjuan.

ARTETA KIMYA

Iwapo Arsenal itafanikiwa kumnasa Alvarez, itakuwa ni usajili mkubwa kwa Arteta, ambaye hata hivyo amekataa kuingia moja kwa moja katika mjadala kuhusu uwezekano wa kumnunua mshambuliaji huyo.

Arteta alisema: “Ni rahisi sana. Chochote unachosoma, kama una swali njoo ugonge mlango wangu, nitakuambia kama ni kweli au la.

Kocha huyo alisema wachezaji wake wanafahamu kuwa kuna taarifa nyingi za tetesi kuhusu usajili, akisisitiza kuwa huwa anawasiliana nao moja kwa moja pale klabu inapopanga kuongeza ushindani katika nafasi zao.

“Kama watahisi kuna shaka kuhusu tunachowafikiria, au kama tunataka kumsajili mchezaji, huwa nawaambia moja kwa moja.

“Nawaambia mipango yetu na sababu zake. Bado tunawaamini, lakini ushindani utaongezeka. Napendelea kufanya hivyo,” alisema Arteta.

Arsenal itarejea dimbani Jumatatu ya mapumziko ya kitaifa nchini England, ikisafiri hadi Villa Park kucheza dhidi ya Aston Villa.