Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dili la Alexander-Arnold bado la moto

Arnord Pict

Muktasari:

  • Kwa sasa moja kati ya stori kubwa inayobamba katika viunga vya Anfield ni mustakabali wa mastaa watatu ambao mbali ya Trent pia kuna Mohamed Salah na Virgil van Dijk.

LIVERPOOL, ENGLAND: WAKATI hatma ya beki Trent Alexander-Arnold ikiwa haijulikani na mkataba wake unaelekea ukingoni huku Real Madrid ikitajwa kwamba inafanya mazungumzo na wawakilishi wake kwa ajili ya kumsajili mwisho wa msimu, timu nyingine pia imeibuka na kuanza mchakato wa kimya kimya ili kumpata staa huyo wa Liverpool.

Kwa sasa moja kati ya stori kubwa inayobamba katika viunga vya Anfield ni mustakabali wa mastaa watatu ambao mbali ya Trent pia kuna Mohamed Salah na Virgil van Dijk.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka England, tayari Trent ameshafanya uamuzi kwamba atajiunga na Real Madrid lakini anataka kuona kama Liverpool itafikia matakwa yake kabla ya kufanya uamuzi wa mwisho, ingawa jambo hilo pia linaweza kuingia ugumu kutokana na Bayern Munich nayo kuingia katika vita hiyo na kuanza kumshawishi.

Licha ya ukweli kwamba, Trent hana mpango wa kuondoka Liverpool katika dirisha hili, gazeti la Kicker kutoka Ujerumani linadai  Bayern imepanga kuhakikisha inamsajili na huenda ikamtumia pia Harry Kane kama sehemu ya kumshawishi ili kuhakikisha wanampata mwisho wa msimu huu.

Bayern inataka kumtumia Kane kwa sababu ana ukaribu na staa huyo, pia ni mtu anayeweza kumsikiliza kwani ni kapteni wake wa timu ya taifa ya England.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 anatajwa kama mojawapo ya malengo ya Bayern kama mbadala wa Joshua Kimmich ambaye kuna uwezekano akaondoka kwenye timu hiyo mwisho wa msimu huu ambapo mkataba wake utamalizika.

Hata hivyo,  wababe hao kutoka Ujerumani wanatambua kuwa endapo Alexander-Arnold atahitaji kuondoka Liverpool basi chaguo lake la kwanza ni Real Madrid.

Kuingia kwa Bayern katika dili hili kunaipa ugumu zaidi Liverpool kwenye mpango wao wa kutaka kumsainisha mkataba mpya kwani timu hizi zinaonekana kutaka kumpa ofa kubwa zaidi jambo litakalosababisha wao wapande juu zaidi kwenye ofa yao ili kumbakisha.

 Alipowahi kuulizwa kuhusu hatma yake katika kikosi cha Liverpool, Trent alisema: “Nimesaini mkataba wa nyongeza mara nne au tano, na hakuna hata mara moja nilitangazwa hadharani kabla sijasaini, hivyo na sasa pia sitofanya hivyo.”

Tovuti ya Liverpool Echo, Desemba mwaka jana iliripoti kuwa staa huyu bado hajafanya uamuzi wowote juu ya hatma yake na Liverpool, pia ametoa masharti mawili kwa mabosi wa Liverpool ili asaini mkataba mpya.

Mwandishi wa habari wa  talkSPORT, Ben Jacobs alisema: “Nimesikia kwamba, ingawa Trent hataki kuondoka katikati ya msimu, amewaambia Liverpool kwamba anataka kusaini mkataba usiopungua miaka mitatu na pia awe kapteni wa timu hiyo kwa muda mrefu.”

Jacobs anasema pia hilo ni moja ya mambo yanayochelewesha makubaliano ya mkataba mpya kati ya Liverpool na mastaa wengine ambao mikataba yao inatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu.