Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dili jipya la Curry Warrios sio mchezo

Muktasari:

  • Timu hiyo ilithibitisha kuongeza mkataba huo juzi Ijumaa, lakini haikutoa maelezo zaidi na kwa mujibu wa ESPN, mkataba huo unatajwa kuwa na kipengele kinachompa Curry chaguo la kuendelea na msimu wa 2028-29.

CALIFORNIA, MAREKANI: SUPASTAA wa kikapu Marekani, Stephen Curry amekubaliana na mkataba wa kuongeza miaka miwili wenye thamani ya Dola 116 milioni na Golden State Warriors ya mjini San Francisco, California, hatua inayolenga kumuweka MVP huyo mara mbili wa NBA na nyota mtarajiwa wa Hall of Fame katika timu iliyomchagua kwenye drafti hadi msimu wake wa 20.

Timu hiyo ilithibitisha kuongeza mkataba huo juzi Ijumaa, lakini haikutoa maelezo zaidi na kwa mujibu wa ESPN, mkataba huo unatajwa kuwa na kipengele kinachompa Curry chaguo la kuendelea na msimu wa 2028-29.

Curry angeweza kuongeza kiwango cha juu cha miaka miwili kwenye mkataba wake uliopo kutokana na kanuni ya 38 katika makubaliano ya pamoja ya NBA kati ya timu na chama cha wachezaji.

Kutokana na kitendo chake cha kuongeza mkataba kinaufanya sasa kufikia jumla ya Dola 178.6 milioni hadi mwisho wa msimu wa 2028-29. Huo utakuwa msimu wa 20 wa Curry akiwa Warriors na  kuwa miongoni mwa wachezaji 12 pekee katika historia ya NBA waliocheza misimu 20 au zaidi. Ni watatu tu kina Dirk Nowitzki, Kobe Bryant na Udonis Haslem waliotumia muda wao wote kucheza katika klabu moja.

Kwa takriban miongo miwili katika timu hiyo, Curry kwa kiasi kikubwa ameifufua Warriors akiirejesha katika enzo za majina makubwa yaliyoichezea Wilt Chamberlain na Rick Barry. Hata hivyo, tofauti na hao, ni Curry aliyebadilisha namna ambavyo klabu hiyo ingeweza kuonekana kuwa katika kiwango bora ambacho imefikia.

Katika mchakato huo amesaidia kubadilisha mchezo wa kikapu katika enzi ya kisasa, mfumo wa mashambulizi na kulazimisha mabadiliko makubwa katika mikakati na mbinu za ulinzi. Yote hayo yametokana na usahihi wake ambao haujawahi kuonekana, idadi kubwa ya mikwaju, kasi na uwezo wake wa kutupia mipira ya pointi tatu.

Katika misimu yake miwili ya kwanza alifunga wastani wa pointi 18 kwa asilimia 47 kwa kila mchezo. Hata hivyo, baada ya majeraha ya mara kwa mara kwenye kifundo cha mguu wa kulia kulifanya akose michezo 40 katika msimu wake wa tatu na kufanyiwa upasuaji uliomaliza msimu.