Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dembele kuikwepa laana ya Ballon d’Or kombe la dunia?

Muktasari:

  • Historia inaonyesha katika miaka zaidi 70, hakuna mchezaji aliyekwenda katika mashindano hayo akiwa mshindi wa mchezaji bora wa dunia Ballon d’Or na kuisaidia timu yake kutwaa Kombe la Dunia na yeye akatetea tuzo yake.

DALLAS, MAREKANI: MSHAMBULIAJI Ousmane Dembele anatazamwa kama ataweza kuvunja mwiko wa kile kinachoitwa ‘laana ya Ballon d’Or’ ya miaka 70, ambayo hata mastaa kama Lionel Messi na Cristiano Ronaldo walishindwa kuikwepa.

Historia inaonyesha katika miaka zaidi 70, hakuna mchezaji aliyekwenda katika mashindano hayo akiwa mshindi wa mchezaji bora wa dunia Ballon d’Or na kuisaidia timu yake kutwaa Kombe la Dunia na yeye akatetea tuzo yake.

Katika kukwepa laana hiyo, Dembele anatakiwa kuhakikisha anakuwa na namba ya uhakika katika kikosi cha kwanza cha Ufaransa na kuonyesha kiwango bora.

Mshambuliaji huyo wa Paris Saint-Germain alianza katika safu ya ushambuliaji ya nyota wanne pamoja na Michael Olise, Desire Doue na Kylian Mbappe katika mechi dhidi ya Senegal.

Lakini Dembele alikuwa miongoni mwa walioonyesha kiwango cha chini zaidi katika safu hiyo. Alitolewa dakika ya 80 baada ya kupiga shuti moja lililokosa lango, kuwa na kiwango kidogo sana cha nafasi za kufunga (xG 0.03), kutotengeneza nafasi yoyote ya mabao, kutopiga chenga yoyote na kutogusa mpira ndani ya eneo la hatari la wapinzani.

Mbadala wake, Bradley Barcola, alifunga bao dakika mbili tu baada ya kuingia uwanjani.

Ripoti zinaeleza makocha wa Ufaransa hawakuridhishwa na kiwango cha Dembele, huku mashabiki wengi wa Ufaransa pia wakionekana kutoridhishwa na mchango wake katika timu ya taifa. Katika mechi 60 alizoichezea Ufaransa, amefunga mabao saba pekee.

Barcola sasa anatarajiwa kuanza katika mechi dhidi ya Iraq huko Philadelphia, na huenda akachukua nafasi ya Dembele au Doue.

Dembele alitwaa tuzo ya Ballon d’Or mwaka 2025 baada ya kuiongoza PSG kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa UEFA.

Hata hivyo, historia inaonyesha hakuna hata mmoja kati ya washindi 17 waliokuwa wanashikilia Ballon d’Or aliyewahi kushinda Kombe la Dunia akiwa bingwa mtetezi wa tuzo hiyo.

Miongoni mwa nyota waliokumbwa na hali hiyo ni Johan Cruyff, Ronaldo Nazario, Messi na Cristiano Ronaldo.

Kwa mfano, Messi alishinda Ballon d’Or mwaka 2021, lakini kabla ya Kombe la Dunia la 2022 tuzo ya mwaka huo ilitolewa kwa Karim Benzema. Benzema baadaye alikosa mashindano hayo kutokana na majeraha wakati Argentina ilipoibuka mabingwa.

Sasa macho mengi yako kwa Dembele, ambaye ni mshindi wa Ballon d’Or wa hivi karibuni. Ikiwa Ufaransa itashinda Kombe la Dunia 2026 huku Dembele akiwa mshindi mtetezi wa tuzo hiyo, atakuwa mchezaji wa kwanza katika historia kuvunja rasmi “laana” hiyo ya zaidi ya miaka 70.


UTATA WASHINDI Ballon d’Or

Hayo ni baadhi ya matukio yanayotajwa mara kwa mara katika mjadala wa washindi wenye utata wa tuzo ya Ballon d’Or.

Hata hivyo, ni muhimu kutambua kwamba hakuna jibu sahihi kabisa kwa sababu tuzo hiyo hupigiwa kura na waandishi wa habari, na vigezo vinaweza kutafsiriwa tofauti. Washindi wanaotajwa zaidi kuwa wenye utata.


Pavel Nedved (2003)

Nedved alikuwa na msimu bora akiwa na Juventus, lakini mashabiki wengi waliamini kuwa: Thierry Henry alistahili zaidi kutokana na mabao na pasi nyingi za mabao akiwa na Arsenal. Pamoja na Paolo Maldini alikuwa na msimu bora.


Luka Modric (2018)

Modric alivunja utawala wa miaka 10 wa Messi na Ronaldo baada ya kuiongoza Real Madrid kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulatya pamoja na Kuifikisha Croatia fainali ya Kombe la Dunia.

Wakosoaji walidai kuwa Cristiano Ronaldo alikuwa na takwimu bora zaidi. Wengine walimtaja Antoine Griezmann alishinda Kombe la Dunia na Ufaransa pamoja na Mfaransa mwenzake Kylian Mbappe alikuwa na mchango mkubwa katika ushindi huo. Miaka ya utawala wa Messi na Ronaldo (2008–2017)


Lionel Messi (2010)

Baada ya Kombe la Dunia la Afrika Kusini na Hispania kutwaa taji la kwanza dunia watu wengi waliamini waliostahili tuzo hiyo ni Andres Iniesta au Xavi walipaswa kushinda tuzo hiyo 2010.

Mbali ya Wahispania hao mwingine alikuwa Wesley Sneijder katika mwaka ambao wengi huutaja kama moja ya “makosa makubwa” ya Ballon d’Or: Akiiongoza Inter Milan kushinda mataji matatu ‘treble’ na kuisaidia Uholanzi kufika fainali ya Kombe la Dunia. Cha kushangaza, hata hakuingia katika tatu bora za mwisho.

Franck Ribery (2013): Nyota Ribery aliongoza Bayern Munich kushinda mataji matatu ‘treble’ ya kihistoria, lakini tuzo ikaenda kwa Cristiano Ronaldo.

Manuel Neuer (2014): Kipa Neuer alishinda Kombe la Dunia 2014 akiwa na Ujerumani.

Neuer alibadilisha kabisa namna ya nafasi ya kipa ilivyoonekana kisasa, lakini alipitwa tena na Ronaldo, jambo lililozua mjadala.


Kesi ya Robert Lewandowski (2020)

Hii ndiyo kesi inayokubalika zaidi kuwa ya bahati mbaya katika historia ya tuzo hiyo.

Mshambuliaji Lewandowski alifunga mabao 55 katika mechi 47, aliiongoza Bayern Munich kushinda treble. Lakini kutokana na janga la COVID-19, tuzo ya Ballon d’Or ya 2020 ilifutwa kabisa. Hata Lionel Messi aliposhinda tuzo ya 2021, alisema hadharani kwamba Lewandowski alistahili kutambuliwa kwa mafanikio yake ya mwaka 2020.


Rodri dhidi ya Vinicius Junior (2024): Huu ndio mjadala mkubwa zaidi.

Hoja za Rodri alishinda Ligi Kuu ya England na Manchester City, alishinda UEFA Euro 2024 na Hispania.Pia alikuwa kiungo muhimu sana katika mafanikio ya timu zake.

Hoja za Vinicius:Aliongoza Real Madrid kutwaa La Liga na Ligi ya Mabingwa.

Alikuwa na mabao na mchango mkubwa katika mechi muhimu. Wengi waliona alikuwa mchezaji mwenye athari kubwa zaidi binafsi.