Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Deco atajwa sababu ya Xavi kuondoka

BARCELONA, HISPANIA. WAKATI Deco alipoanza kusikika kama mtu anayetarajiwa kuchukua nafasi ya Mkurugenzi wa Soka pale Barcelona, Mateu Alemany, wadau mbalimbali wa soka nchini humo walikuwa na hofu juu ya uhusiano kati yake na kocha wa kikosi hicho, Xavi Hernandez. Ndani ya mwaka mmoja tu tayari mmoja anampisha mwenzake.

Hatimaye Xavi anaondoka kutokana na matokeo ya uwanjani, lakini kwa mujibu wa Guillem Balague ambaye ni miongoni mwa waandishi maarufu wa habari za michezo Hispania inaelezwa Deco yupo nyuma ya pazia.

Balague alisema wakati Deco anaondoka klabuni kama mchezaji, yeye na Xavi walikuwa hawana maelewano mazuri na Pep Guardiola alipofika, alifanya kuondoka kwa Deco na Ronaldinho kuwa kipaumbele chake.

Mwandishi huyo, anaieleza BBC kwamba Xavi amejihisi kuwa peke yake katika klabu hiyo tangu kuteuliwa kwa Deco, na kuondoka kwa Alemany. Mbaya zaidi ni kwamba Deco anaondoka kutokana na mwenendo wa timu hiyo na inaelezwa kwamba, Deco ‘haogopi kueleza shaka yake’ kuhusu Xavi.

Haya yanajiri muda mfupi baada ya Deco kufanya mahojiano akidai kwamba Barcelona walihitaji kuachana na mtindo wao wa zamani.