Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dakika 90 za Aliou Dieng dhidi ya Barca

DIENG Pict

Muktasari:

  • Dieng aliyetua Valencia msimu huu akitokea Al Ahly ya Misri, katika mchezo huo ambao ulikuwa wa kwanza kumaliza dakika tisini katika La Liga, amefanikiwa kushinda asilimia 73 ya mapambano aliyokabiliana nayo uwanjani.

LICHA ya Valencia kupokea kipigo kizito cha mabao 5-0 katika mechi ya Ligi Kuu ya Hispania, La Liga dhidi ya Barcelona, lakini kiungo mkabaji raia wa Mali, Aliou Dieng, ameonyesha utulivu na ufanisi mkubwa katika dakika zote tisini alizocheza.


Dieng aliyetua Valencia msimu huu akitokea Al Ahly ya Misri, katika mchezo huo ambao ulikuwa wa kwanza kumaliza dakika tisini katika La Liga, amefanikiwa kushinda asilimia 73 ya mapambano aliyokabiliana nayo uwanjani.

Kiungo huyo kutokana na kile alichokifanya ndani ya dakika 90 za mchezo huo, amepewa maksi 6.8 kati ya 10, huku akishinda mapambano 8 kati ya 11, sawa na asilimia 73.

DIE 01

Katika upande wa umiliki wa mpira, kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28, alifanikiwa kutoa pasi 19 kati ya 20, sawa na asilimia 95 ya usahihi. Pia alifanikiwa kupiga chenga tatu kati ya nne alizojaribu, sawa na asilimia 75.

Kwenye eneo la ulinzi, Dieng alishinda mipira ya chini yote 8 kati ya 11, akashinda takolini mbili kati ya tatu, akaokoa shambulizi moja na kuurudisha mpira kwenye umiliki mara tano, huku akizuia shambulizi moja.

DIE 02

Kwa upande wa nidhamu, Dieng alifanya faulo moja na kusababisha wapinzani wake kufanya faulo mbili dhidi yake.

Dieng kwake hiyo ilikuwa ni mechi ya nne ya La Liga msimu huu baada ya kwanza dhidi ya Celta Vigo iliyomalizika bila bao (0-0) akicheza kwa dakika 21.

DIE 03

Mechi iliyofuatia dhidi ya Real Betis ambayo Valencia ilifungwa 1-0, alitumika kwa dakika mbili, huku dhidi ya Deportivo ambayo pia walifungwa 3-1, alicheza kwa dakika 24.

Baada ya mechi hizo tatu za kwanza kutokea benchi, dhidi ya Barcelona akaanza na kumaliza dakika zote tisini, lakini akashindwa kutoa mchango wa kuinusuru Valencia na kipigo.