Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwamba Aziz Ki taratibu tujiandae kumpokea Bara

HISIA Pict


HISIA zangu zinaniambia shemeji yetu Aziz Ki ameanza safari ya kurudi ‘nyumbani’ kwake Tanzania taratibu. Uswahilini huwa tunasema mdogo mdogo. Hakukaa hata mwaka mmoja ndani ya klabu ya Wydad Casablanca na jamaa wakaamua kumuuza.


Niliwahi kuwaambia rafiki zangu wa karibu kwamba sikumuona Aziz Ki akidumu sana katika soka la Morocco. Kuna sababu nyingi. Kwanza kabisa ni namna ambavyo Waarabu wana wachezaji wengi kama Aziz. Eneo la kiungo cha ushambuliaji sio shida zao.


Wana shida zaidi na kiungo mmoja wa ulinzi wa aina ya Himid Mao. Ndio maana pale Al Ahly kuna Alou Dieng. Ndio maana hawa akina Balla Conte, Allasana Kante wana soko kubwa huko Uarabuni. Wengine wanahitajika sana ni washambuliaji kama akina Mayele.

Viungo washambuliaji Waarabu wapo wengi. Ndio maana hata Berkane hawakuona sana makali ya Clatous Chama wakati ule walipomchukua. Wanao wachezaji wengi watundu katika eneo hilo. Wanao hata katika timu za vijana.

Kama hauonyeshi uwezo wa juu kupitiliza basi Waarabu hawawezi kukuvumilia. Chama hakuchukua muda wakaturudishia. Aziz hakuchukua muda sana Wydad wakaamua kumuuza kwenda Libya. Kama angeonyesha makali sidhani kama wangemuuza.

HISI 01

Kitu kingine ni kwamba sikumuona Aziz akiwika katika Ligi Kuu Morocco kama ilivyokuwa hapa. Mpira wa Waarabu una mahitaji mengi ndani na nje ya uwanja. Unahitaji nidhamu ya hali ya juu kuliko mpira wetu ambao umekusanya timu nyingi dhaifu.

Mfano wa wapinzani wa kila wikiendi wa Wydad ni kama ulivyowaona Far Rabat waliocheza na Yanga wikiendi iliyopita. Ni mwendo wa mpira wa kasi na mbio nyingi. Mpira unachezwa katika ‘tempo’ ya hali ya juu. Aziz ni mchezaji wa matukio zaidi.

Hapa kwetu ilikuwa rahisi kwake kwa sababu leo Yanga wangecheza na Namungo na kumiliki mpira kwa asilimia 99. Keshokutwa wangecheza na Coastal Union na kumiliki mpira wote. Kule Morocco licha ya Wydad kuwa wakubwa, lakini mpira wao dhidi ya wapinzani ni kuhenya kwa dakika zote.

Aziz ana ‘kauvivu’ fulani ambako nilijua asingemudu sana mpira wa Waarabu wa kule. Huku kwetu alitusisimua katika matukio ya mashuti. Kona nzuri. Faulo nzuri. Mashuti ya mbali. Pasi za mwisho katika eneo la mwisho ambalo Yanga mara zote walifika kwa urahisi kwa sababu kama nilivyosema, muda mwingi katika mpira wetu wanamiliki sana mpira.

HISI 02

Simon Msuva ndiye mchezaji aliyetoka katika ligi yetu na akaimiliki sana Ligi Kuu Morocco kwa sababu sio mvivu. Muda wote wa dakika 90 Msuva anakuwa bize uwanjani. Anakimbia kila sekunde kuanzia katika kushambulia na kukabia juu.

Ukipima aina ya mpira wa Chama na Msuva utagundua kwanini Msuva alikaa Morocco kwa muda mrefu. Ukipima aina ya mpira wa Aziz na Msuva utagundua kwanini Msuva alikaa Morocco kwa muda mrefu. Sio suala la kipaji tu, kuna suala la kujituma na kuwa mtumwa.

Wachezaji wengi wa ligi yetu wanaocheza katika timu kubwa huwa wanaonyesha ubora bila kufikia asilimia 90 ya uwezo wao. Unaweza ukatumia asilimia 40 ya ubora wako kushinda mechi dhidi ya Kagera Sugar au Fountain Gate.

HISI 03

Hata katika siku mbaya Pacome Zouzoua anaweza kufunga mabao mawili dhidi ya Coastal Union akaimbwa sana. Kuna pengo kubwa kati ya walionacho na wasionacho katika mpira wetu. Ni tofauti na kule Morocco.

Morocco leo unacheza na Raja Casablanca ni pambano gumu. Jumatano unacheza na Far Rabat ni pambano gumu. Jumamosi nyingine unacheza na Berkane ni pambano gumu. Ukikutana na Fus Rabat ni pambano gumu. Ukicheza na Difaa El Jadida ni pambano gumu.

Huku una mechi mbili tu ngumu. Dhidi ya Simba na dhidi ya Azam. Mechi nyingine zote unatarajiwa kushinda. Kidogo Singida Black Stars nao wameongeza upinzani, lakini hawa kina Mbeya City unatarajiwa kushinda nyumbani na ugenini.

Kitu kingine ambacho namuona Aziz akirudi ‘nyumbani’ kwao Tanzania ni aina ya maisha yetu. Kwa Aziz Tanzania ni kama nyumbani. Ni kama yupo Burkina Faso au Ivory Coast. Kila anakopita anapokewa vizuri na Watanzania wakarimu.

HISI 04

Kila anakopita anashingiliwa. Lakini maisha yetu ya usiku yana raha zaidi. Ni tofauti na kule kwa Waarabu ambako hawataki kukuona unasterehe katika maisha yako. Nimewahi kumtembelea Msuva wakati anacheza Difaa Jadida na maisha ya usiku hayawi rahisi kwa mwanasoka. Waarabu wanataka kukuona umekaa ndani tu umetulia.

Hapa wachezaji wetu wanafaidi maisha ya usiku. Wanafaidi maisha nje ya mpira. Wanafaidi kila kitu kuanzia chakula na mengineyo. Haishangazi kuona kuna wachezaji wengi wa kigeni ambao waliwahi kuchomoka Tanzania, lakini wakajikuta wamerudi.

Wengine walikuwa mastaa wakubwa, lakini baadaye walirudi na kucheza timu za kawaida tu. Wengine walienda kucheza hadi Ihefu. Makocha nao wamekuwa wakirudi mara kwa mara. Wanafurahia maisha ya Tanzania. Kuna makocha ambao waliwahi kufundisha timu kubwa wakaondoka, lakini wakajikuta wamerudi katika timu ndogo. Ndio utamu wa maisha ya Tanzania.

Namuona Aziz katika mpira wetu kwa mara nyingine muda si mrefu kuanzia sasa. Na zaidi ni kwamba mpira wetu wenyewe una vipesa ambavyo vinawaridhisha wachezaji wengi wa nje. Kando ya Afrika Kaskazini na kule Afrika Kusini, nawaona wachezaji wengi wakipendelea kucheza hapa. Na siku hizi tunapokea hata wachezaji wenye viwango vya juu kabisa.