Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dah! Chelsea itakuwaje sasa

Chelsea Pict

Muktasari:

  • Chelsea ambayo mchezo ujao itakutana na Brighton kwenye dimba la AMEX, inatarajiwa kuwa na zaidi ya wiki mbili ngumu kutokana na pengo la Jackson.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Chelsea, Enzo Maresca amepata pigo kubwa baada ya mshambuliaji wake Nicolas Jackson kupata majeraha makubwa yatakayomweka nje ya uwanja kwa muda mrefu tofauti na ilivyoripotiwa hapo awali.

Chelsea ambayo mchezo ujao itakutana na Brighton kwenye dimba la AMEX, inatarajiwa kuwa na zaidi ya wiki mbili ngumu kutokana na pengo la Jackson.

Jackson alilazimika kutoka uwanjani kwenye ushindi wa 2-1 dhidi ya West Ham Februari 03, kutokana na jeraha la paja.

Kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa The Telegraph, Jackson amefanyiwa uchunguzi umeobaini jeraha lake la misuli ya paja lake ni baya zaidi kuliko ilivyofikiriwa hapo awali.

Chelsea walikuwa na matumaini Jackson hatokosekana uwanjani kwa muda mrefu, lakini uchunguzi wa mwisho umebaini tatizo lake ni kubwa.

Tangu kuanza kwa msimu huu Jackson amefunga mabao tisa na anatarajiwa kukaa nje hadi mwishoni mwa mwezi Machi, jambo linalomaanisha atakosa michezo dhidi ya Brighton, Aston Villa, Southampton, Leicester na Arsenal.

Matumaini ya benchi ka ufundi la Chelsea ni atarudi kiwanjani dhidi ya Spurs Aprili 02, lakini hilo halina uhakika.

Mbali ya Jackson, Chelsea wana mshambuliaji mwingine, Marcu Guiu, ambaye pia yuko nje kwa majeraha aliyoapata katika mchezo huo dhidi ya West Ham.

Kuumia kwa wachezaji hao wawili kunamwacha Maresca na chaguo la kumtumia aidha  Christopher Nkunku au Cole Palmer ambaye mara kadhaa ndio amekuwa akimtumia katika eneo hilo.

Majeraha haya yanaonekana kuwa pigo kubwa kwa Chelsea katika kipindi hiki wanachopambana kuhakikisha wanafuzu Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

Baada ya michezo 24, Chelsea inashika nafasi ya nne kwa alama 43, mbili mbele ya Manchester City, inayoshika nafasi ya tano.