Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Curry: Rekodi ya mipira 4,000 nyavuni

Muktasari:

  • Ni vigumu kuzungumzia mchezo wa kikapu bila kumtaja Curry. Jamaa alibadilisha jinsi mchezo unavyochezwa, akaifanya mipira ya mitupo mitatu kuwa silaha kuu ya ushindi na sasa ameweka rekodi inayothibitisha umahiri. 

CALIFORNIA, MAREKANI : WIKIENDI hii imekuwa ya kuvutia katika historia ya NBA. Mashabiki wa Golden State Warriors waliokuwa wamefurika kwenye Uwanja wa Chase Center walishuhudia tukio la kihistoria kwa Stephen Curry kufunga mpira wenye alama tatu (3-pointers) wa 4,000 katika maisha yake, jambo ambalo hakuna mchezaji mwingine aliyewahi kulifanya. 

Ni vigumu kuzungumzia mchezo wa kikapu bila kumtaja Curry. Jamaa alibadilisha jinsi mchezo unavyochezwa, akaifanya mipira ya mitupo mitatu kuwa silaha kuu ya ushindi na sasa ameweka rekodi inayothibitisha umahiri. 

Lakini je safari yake ilikuwaje? Na je maana ya kufikia namba hizo ni ipi kwa NBA na kizazi kijacho?

Mwaka 2009, Curry alikuwa kijana wa miaka 21 alipofunga mpira wake wa kwanza wa mitupo mitatu akiwa mchezaji wa Warriors. Wakati huo, hakuna aliyefikiria kwamba angekuwa mchezaji mwenye ushawishi mkubwa zaidi katika historia ligi hiyo pendwa ya kikapu. 

Aliposajiliwa NBA baadhi ya wachambuzi walimtazama kwa mashaka. Waliamini alikuwa mfupi, hana nguvu nyingi na huenda asingecheza katika kiwango cha juu. Lakini hakuwahi kujali mawazo ya watu wengine alijua kitu kimoja - kwamba anaweza kupiga mipira mitatu  kutoka popote uwanjani. Ndiyo maana, mwaka baada ya mwaka alijitengenezea jina lake kwa kutumia ushupavu, nidhamu na ustadi wa juu wa kushambulia kutoka nje ya eneo la pointi tatu. 

Miaka 16 baadaye, Curry amefikisha mipira 4,000 ya mitupo mitatu rekodi ambayo haijawahi kuwekwa na mchezaji yeyote katika historia ya NBA. 


MCHEZO WA KIHISTORIA

Kabla ya mchezo dhidi ya Sacramento Kings, Curry alikuwa na mipira 3,998 ya mitupo mitatu katika rekodi. Alihitaji mipira miwili kufikia rekodi ya 4,000 na kila shabiki aliyekuwepo Chase Center alijua kitu kikubwa kinakaribia kutokea. 

Katika robo ya kwanza dakika ya 5:35, Curry alipokea pasi kutoka kwa Jonathan Kuminga na kwa wepesi akatupa mpira kwa ustadi wake wa kawaida. Ulikuwa mpira wa 3,999. Mashabiki walishangilia kwa nguvu wakijua kuwa wanakaribia kushuhudia historia. 

Mpira wa kihistoria ulifika katika robo ya tatu dakika ya 8:19. Katika hali ya sintofahamu Moses Moody alipata mpira na kumrudishia Curry. Huku akiwa kwenye kona ya uwanja akafanya harakati zake za kawaida ‘pump fake’ kumhadaa mlinzi, akachukua nafasi na kutupia shuti. Mpira ulizama ndani ya kikapu.

Mashabiki walilipuka kwa shangwe. Ulikuwa mpira wa 4,000 wa Curry na uwanja mzima ukasimama kumpigia makofi. 

Baada ya mchezo Curry alizungumza na waandishi wa habari akisema: “Ni hisia ya kipekee kufikia hatua hii mbele ya mashabiki wangu wa nyumbani. Kila mtu anajua jinsi ninavyothamini mashabiki wa Warriors. Hili ni jambo maalum sana kwangu.” 


REKODI KWA NBA

Kufikia rekodi hiyo si jambo dogo. Hii ni hatua inayothibitisha kuwa Curry si tu mchezaji wa kawaida, bali ni mchezaji aliyeleta mapinduzi katika NBA. 

Kwa zaidi ya miongo miwili, wachezaji wa NBA walikuwa wakizingatia sana mashambulizi ya ndani ya uwanja, wakitegemea sana wachezaji warefu wenye nguvu. Lakini Curry alibadilisha hilo kabisa alionyesha kuwa mpira wa kikapu unaweza kuwa mchezo wa umbali, na mipira ya tatu inaweza kuwa silaha kuu ya ushindi. 

Hata LeBron James hakuweza kuficha msisimko wake juu ya rekodi hii. Aliandika kwenye mtandao wa X (Twitter): “4K kutoka kwa Trey ni KICHAA!!! Hongera ndugu yangu.” 

Kocha wake, Steve Kerr, alitania kwa kusema: “8,000? Hatujui Curry ataishia wapi. Atazidi kusukuma mipaka!” 


ITAVUNJWA?

Sasa swali kuu linabak, Je, kuna mchezaji mwingine atakayefikia au kuvunja rekodi ya Curry? 

Mpaka sasa hakuna anayekaribia. Wachezaji wengine wakubwa wa NBA kama Ray Allen (2,973) na Reggie Miller (2,560) waliostaafu kabla ya Curry hawakuwahi kufikia hata 3,000, sembuse 4,000. 

Ikiwa Curry ataendelea kucheza kwa miaka 3-4 zaidi, huenda akavuka 5,000 mipira ya tatu, jambo ambalo litakuwa vigumu kwa yeyote kulifikia kwa miongo kadhaa.