Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Curry amshawishi LeBron kujiunga Warriors

NBA Pict

Muktasari:

  • Hakuna anayejua kwa uhakika kinachoendelea akilini mwa James kwa sasa. Akiwa na umri wa miaka 41, anaweza kuamua kustaafu na kuhitimisha kazi yake akiwa mmoja wa wachezaji wakubwa zaidi kuwahi kucheza mchezo huo.

NEW YORK, MAREKANI: WAKATI Fainali za NBA zikiendelea kushika kasi, macho mengi tayari yameanza kuelekezwa kwenye kipindi cha usajili wa wachezaji huru,jina kubwa linalozungumziwa ni LeBron James.

Hakuna anayejua kwa uhakika kinachoendelea akilini mwa James kwa sasa. Akiwa na umri wa miaka 41, anaweza kuamua kustaafu na kuhitimisha kazi yake akiwa mmoja wa wachezaji wakubwa zaidi kuwahi kucheza mchezo huo.

Hata hivyo, LeBron bado anaendelea kucheza katika kiwango cha juu, na bila shaka angependa kupata nafasi moja au mbili zaidi za kushinda ubingwa mwingine wa NBA kabla ya kutundika viatu. Swali kubwa ni kama anaamini kwamba Los Angeles Lakers ndiyo timu yenye uwezo mkubwa zaidi wa kumpa nafasi hiyo.

Kwa hali ilivyo, James angependa kubaki Los Angeles na kuepuka kuhamisha familia yake tena, huku Lakers wakiboresha kikosi chao. Lakini kuna nyota mmoja wa NBA ambaye anaweza kumbadilisha mawazo hayo.

NB 01

Curry na LeBron wanaweza kuungana?

Tangu Stephen Curry na LeBron walipocheza pamoja katika Olimpiki 2024 huko Paris, wazo la kuwaona nyota hao wawili wakicheza katika timu moja ya NBA limeendelea kuzungumziwa.

Wachezaji hao wawili wanaheshimiana, na mitindo yao ya uchezaji inaonekana kuendana vizuri kiasi kwamba wengi wanaamini wangekuwa washirika bora ndani ya uwanja.

Kwa mujibu wa mwandishi wa ClutchPoints, Brett Siegel, Curry anapanga kukutana ana kwa ana na LeBron kwa lengo la kumshawishi kujiunga na Golden State Warriors.

NB 03

Warriors wanaonekana kuwa tayari kufanya usajili mkubwa katika kipindi hiki cha wachezaji huru baada ya kukosa nafasi ya kucheza mchujo (playoffs) mara mbili ndani ya misimu mitatu iliyopita. Hakuna shaka kwamba kumpata LeBron kungekuwa moja ya hatua kubwa zaidi katika soko la usajili.

NB 02

Warriors hawatalazimika kutoa wachezaji wengi

LeBron hana mkataba wa msimu wa 2026/27, jambo linalomaanisha kuwa Warriors hawatalazimika kutoa fidia ya kubadilishana wachezaji au chaguo za draft ili kumpata.

Hata hivyo, ili kutengeneza nafasi ya mshahara wake ndani ya kikosi, kuna uwezekano mmoja kati ya Jimmy Butler au Draymond Green akalazimika kuondoka.

Iwapo LeBron na Curry wataungana, itakuwa moja ya ushirikiano mkubwa zaidi katika historia ya NBA, ukiwakutanisha wawili kati ya wachezaji waliotawala ligi hiyo kwa zaidi ya muongo mmoja na ambao wamekutana mara nyingi katika fainali za NBA wakiwa wapinzani wakubwa.

Kwa sasa, hatma ya LeBron bado haijulikani, lakini uvumi wa kuhamia Warriors unaendelea kupata nguvu kadiri kipindi cha usajili kinavyokaribia.